AY 5225
JF-Expert Member
- Jul 16, 2023
- 542
- 1,239
Upo sahihi kwa kiasi kikubwa sana mdogo wangu. Nimependa sana unavyo jenga hoja. Ni generation z wachache sana ambao wanaweza kuwa na uwezo wa kujielezea kwa hekima wewe.
Itoshe kusema kwamba wewe ni Great Thinker.
Maxence Melo Muangalie huyu kijana ana kitu ndani yake.
Nakubaliana na hoja zako kwa kiasi kikubwa but kuna maeneo machache kuhusu hoja zako nataka kuyatolea ufafanuzi kidogo.
9. Sababu nyingine ya Life expectancy kuwa chini miongoni wa Genetation Z ni pamoja na poor life style kama vile ulevi, ngono zembe, utumiaji wa mihadarati n.k.
8. Life style ya Generation Z ipo heavily influenced with celebrities life style . Some of them are just smoking and drinking because they have learnt that their favourite celebrities are smoking and or drinking . Mfano Konde Boy etc. They think it is okay to smoke and drink kwa sababu favourite celebrity wao ana drink na ku smoke.
7. Poor health ni kwa sababu ya poor life style.( pia hapa sio tu kuwa blame generation z kwa sababu kama nilivyo sema kwenye bandiko langu awali life style ya Generation Z imekuwa programmed. So poor health inasababishwa pia na mambo mengine kama vile aina ya vyakula mfano G.M.Os na gadgets etc.
5.upo sahihi kabisa u guys are very reckless. Ur lives are moving in the direction of " I don't give a JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala" mentality.
3. Upo sahihi kabisa homosexuality ipo tangu Zamani lakini u guys tend to be more tolerant towards it.
Miaka ya 2000 mwanzoni vijana tulitoka Kinondoni kwenda Temeke kutafuta mademu sasa hivi unasoma mitandaoni vijana wa Gen z anajitangaza mtandaoni wanatafuta mabwana.
Kuna mtu mmoja alikuwa anasema kwa utani siku moja kwamba huu mmomonyoko wa maadili among Generation Z ni laana ya wazazi wa kizazi cha miaka ya sabini, themanini hadi tisini mwanzoni. Wazazi wetu walikuwa wanatuambia ; 1. Msivute bongi, tukawa hatusikii now Generation Z mnavuta unga. Wakatuambia acheni zinaa . Msifanye sex kabla ya ndoa( uhuni na umalaya)hatukuwasikia now Gen Z ni ushoga na usagaji. Msisikilize muziki wa Rap hatukuwasikia now Gen Z mnasikiliza Singeli na Amapiano.
Akasema laana ya Gen Z watoto wenu watakuwa wanauana kwa Risasi kama South Africa au Marekani... na nyie mtakuwa mnalalamika kwanini watoto wenu wanauana kwa sababu za ovyo
Kwenye kupima life expectancy sidhani kama nadharia ya vizazi inaingia kwakua wana'assume kwamba if all factors remain constant, basi watu hawa wana life expectancy ya miaka kadhaa. Mfano; life expectancy ya mTanzania as of 2022 ni miaka 66 regardless yupo kwenye kundi gani la jamii.
Kuna ule msemo wa Mwana FA kwamba "dunia haitosimama hata ukigoma kwenda nayo", nadhani ina maana sawa na "learn to surf or get carried away". Tolerance yetu na agenda za LGBTQ community nadhani mzizi wake ndo umepatikania huko. Kama mliotutangulia ambao ndio mnaoshikilia nchi katika nyanja zote kwa sasa mmeshindwa kuzuia hili tatizo, sisi tutafanyaje? Mnatulaumu bure tu kwakweli.
Angalau serikali ilichukua hatua ya kuzuia sites za pornography ambazo ukiniuliza mimi, nitasema ndio chanzo kikubwa cha watu ku'develop wild wild wild sexual fantasies na katika kutaka kuzijaribu ndo bendera inazidi kupepea. Lakini bila kuingia na kwenye content za wasanii, ni kazi bure. Weekend iliyopita niko zangu mtaani nazurula nikapita sehemu inapigwa Singeli hiyo aloooh! mbaya zaidi kundi la watoto wana'sing along word to word halafu nyimbo inazungumzia kwa mpalange sijui kumefanyaje.
Explicit contents na vulgarism kwenye nyimbo za Bongo fleva siku ni kawaida sana na wasanii wenyewe wengi wao sio hata Gen-Z. Leo tu kuna uzi nimeuona unazungumzia mstari wa G Nako kwenye Wapoloo, kina Zuchu, Mbosso, Harmonize, Rayvanny mpaka Diamond wote huwa wana lyrics za uchochezi za kufanya mtu ujihisi "left-out the new ways". NB: wote hawa ni millenials hivyo point ya kwamba wao ndo hu'influence tabia zetu inadhihirika hapa.
Tukiangalia historia yetu wanadamu, kadri miaka inavyokwenda ndio matendo mapya yanaongezeka. Yaani kama sisi Gen-Z tunaonekana wehu namna hii kwa sasa, ngoja Alpha waje kuchukua kijiti mbona tutajua hakuna tulichowahi kujua. Kwa sasa mtu ukiwaza dunia sana inavyoenda, suala la kupata watoto inabidi u'consider kulitoa kwenye bucket list kwakweli maana unaweza kuwa unatamani mwanao wa kiume aje kuendeleza legacy yako kumbe mwenzio anatamani akaolewe Canada.
By the way asante kwa hili darasa na compliments mkuu, ubarikiwe sana.