Kulipa mamilioni kusomesha 'Generation Z' ni kama kucheza kamari!


Kwenye kupima life expectancy sidhani kama nadharia ya vizazi inaingia kwakua wana'assume kwamba if all factors remain constant, basi watu hawa wana life expectancy ya miaka kadhaa. Mfano; life expectancy ya mTanzania as of 2022 ni miaka 66 regardless yupo kwenye kundi gani la jamii.

Kuna ule msemo wa Mwana FA kwamba "dunia haitosimama hata ukigoma kwenda nayo", nadhani ina maana sawa na "learn to surf or get carried away". Tolerance yetu na agenda za LGBTQ community nadhani mzizi wake ndo umepatikania huko. Kama mliotutangulia ambao ndio mnaoshikilia nchi katika nyanja zote kwa sasa mmeshindwa kuzuia hili tatizo, sisi tutafanyaje? Mnatulaumu bure tu kwakweli.

Angalau serikali ilichukua hatua ya kuzuia sites za pornography ambazo ukiniuliza mimi, nitasema ndio chanzo kikubwa cha watu ku'develop wild wild wild sexual fantasies na katika kutaka kuzijaribu ndo bendera inazidi kupepea. Lakini bila kuingia na kwenye content za wasanii, ni kazi bure. Weekend iliyopita niko zangu mtaani nazurula nikapita sehemu inapigwa Singeli hiyo aloooh! mbaya zaidi kundi la watoto wana'sing along word to word halafu nyimbo inazungumzia kwa mpalange sijui kumefanyaje.

Explicit contents na vulgarism kwenye nyimbo za Bongo fleva siku ni kawaida sana na wasanii wenyewe wengi wao sio hata Gen-Z. Leo tu kuna uzi nimeuona unazungumzia mstari wa G Nako kwenye Wapoloo, kina Zuchu, Mbosso, Harmonize, Rayvanny mpaka Diamond wote huwa wana lyrics za uchochezi za kufanya mtu ujihisi "left-out the new ways". NB: wote hawa ni millenials hivyo point ya kwamba wao ndo hu'influence tabia zetu inadhihirika hapa.

Tukiangalia historia yetu wanadamu, kadri miaka inavyokwenda ndio matendo mapya yanaongezeka. Yaani kama sisi Gen-Z tunaonekana wehu namna hii kwa sasa, ngoja Alpha waje kuchukua kijiti mbona tutajua hakuna tulichowahi kujua. Kwa sasa mtu ukiwaza dunia sana inavyoenda, suala la kupata watoto inabidi u'consider kulitoa kwenye bucket list kwakweli maana unaweza kuwa unatamani mwanao wa kiume aje kuendeleza legacy yako kumbe mwenzio anatamani akaolewe Canada.


By the way asante kwa hili darasa na compliments mkuu, ubarikiwe sana.
 
Wewe generation Z, uko na akili kuwazidi wenzio wengi.

It's a simple fact, kila kizazi kinachofuatia ni matokeo ya vizazi vilivyopita. Generation Z wanaendeleza yale waliyokuta Millenials na generation X wanafanya.

Asante sana mkuu.
 
Hiz Mambo inategemea na wewe sio kizazi. Coz mtu huyo huyo aliyelelewa China au tuseme far East ni tofauti na aliyelelewa africa na ulaya na Amerika. Kinachotutesa hapa afrika ni kule kuacha tamaduni zetu na kukumbatia za kigen. Matokeo yake tunapokea uchafu wote mzima mzima. Kuhusu elimu broda lipa ada hata ya million 60 mzee achana na hiz elimu za kuwafanya vijana kujadili simba na yanga kila kukicha. Mtoto muandae akaajirike popote dunian tena kwa ushindan. Watoto wanaandaliwa tangu wakiwa wadogo kabisa. Pata muda wa kukaa na wanao kusali nao kama una biashara wakiwa wapo mapumziko kashinde nao kazin. Jifunze mila na destur zote nzur na pia waombe wanao na kuwatolea sadaka. Hakunaga kitu cha bahat mbaya dunian. Kila kitu hutokea kwasababu. Hakunaga kizazi kipya kuna uzembe mpya. Kuwa strict utazalisha bonge la mtu strong.
 
🤣🤣🤣🤣
 
Sahihi
 
Sahihi
 
Namba moja, umechemka, watoto wa UK, Australia, Ulaya, wanasoma shule nzuri sana, kuliko za kwetu, unataka kusema, kwa vile wamesoma shule nzuri, maisha Yao yataharibika?
Kumsomesha mtoto international school of Tanganyika, ili apate exposure ya dunia, na kumsomesha saint kayumba, wewe unaona kayumba ndio Bora?
Ili ufanikiwe maishani sio lazima usome kwa mateso, unatembea km 5,unakunywa uji usio na sukari, umewekwa chumvi, unatembea na fagio na kidumu cha kumwagilia maji!
Dunia ya kesho, itatawaliwa na tekinolojia, mtoto inabidi apewe skills na elimu Borasifundi
kayomuwezesha Kuta wala dunia na maisha yake,
Kuna u lazima gani kutesa mtoto ili ajue kufua blanketi kwa mikono, badala ya kumfundisha kutumia washing mashine, na ku I repair ikiharibika, mtoto awe na elimu Bora, ambayo ni applicable kwa maisha yake, ajue siasa, muziki,kilimo, driving, sio kutumia jembe LA mikono, wakati siku hiz zipo piki piki zinaweza kulima,
Kusema mtoto wa 2020,afundishwe kama sie wa 1990! Ni kukosa busara!
Ku na mashine zina pika wali,chapatti, ugari, samaki,
Sasa kwanini mtoto asifundishwe jinsi ya kutumia internet na kujifunza vitu mtandaoni,
Watoto watatu wanatembea kwa miguu,fagio na kidumu, vyoo vya shimo, darasani wapo 80,
Wengine watano wapo kwenye basi, full ac, watoto wanachezea IPads, shuleni vyoo vya ku flush, darasani wapo 25!
Bro wewe unasema wa kayumba ndio watatoboa maishani!
 
Bado tu hujamaliza hili mkuu, kwanini unaumia watu wakitumia hela zao na ambazo hujui wamezitafuta vipi??
Inatosha mwanao kusoma shule za kama so usi force tufanane. Mwisho wa yote hakuna atakae kuja kwako kuomba ada au hifazi siku mtoto akikwama
We mwenyewe unaonekana umezaliwa 1998
 
mfano familia zinazoishi kwenye majiji ni wapi mtoto atatembea kwa mguu kwenda shuleni na kurudi, huoni unahatarisha maisha ya watoto.., ndugu Mtanzania mjini siyo vijijini na pia kama nilisoma kwa shida haimaanishi ni watoto ama wadogo wetu nao wasome kwa shida. pia fuatilia vizuri hichi kizazi cha ushoga na mapenzi ya jinsia moja mbona wengi wao maisha ya kawaida sana, elimu yao ni hii hii ya Kayumba
 
Tunazungumzia hasa kwenye suala la maadili sio masuala ya teknolojia
 
Umeandika vema na hoja zinajieleza. Kongole
 
Umeichambua vizuri sana generation Z..na sikujua kirefu chake wala sikujua kuna next generation. Asante sana kwa elimu hii.

Hiki kizazi Z nilikisikia miaka kadhaa nyuma nikiwa kwenye training ya office yangu. Kampuni yangu ni ya kimataifa na ilikuwa ina plan kuajiri hii Z..

Kwamba waruhusiwe kupiga pensi, kuweka dreadrocks na mengineyo..sie wahenga tuliguna ila hatuna maamuzi na hatuna nguvu ya kushindana na dunia.
 
Mtoa mada kabla ya kutulaumu, ungeangalia kwanza nyinyi kama wazazi mliaandaa mazingira gani vijana wasifike hatua hiyo.

Swali lako wazazi unawaonea, Kwani tik tok ama technologia zinatengenezwa na wazazi ? Awa watoto wamezaliwa kipindi ambacho internet imeshatawala. Hivyo wamekuwa wakiwa wanatumia internet na social network zimeshajaa...huwezi fosi waishi kama wahenga waliozaliwa kipindi cha dark age

Binadamu ni product wa mazingira yake
 
Tunazungumzia hasa kwenye suala la maadili sio masuala ya teknolojia
Hoja yangu inagusa pande zote, kuanzia teknolojia mpaka maadili. Maadili mabovu ya sasa, ni muendelezo wa maadili mabovu ya kizazi kilichopita. Kama kizazi kilichopita kingeweka misingi imara ya kimaadili, kizazi hiki kisengekua hatari namna hii.

Lakini pia utandawazi unarahisha zaidi tabia mbovu kadri siku zinavyosogea. Zamani, ili mwanamke ajiuze, ilibidi ajipange barabarani au bar. Ila kwa sasa teknolojia imerahisisha mambo sana. Ni kugusa tu huko telegram na watsapp, unaletewa huduma popote ulipo!

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hapo sawa lakini sio mmbo ya matreni ya umeme hayahusiani na huu uzi
 
Tunazungumzia hasa kwenye suala la maadili sio masuala ya teknolojia
Yani katika watu ambao hawatakiwi kabisa kuzungumzia maadili ni wewe mharibifu mkubwa, wewe mwenyewe unasemaga kabisa kwamba huna mpango wa kuoa wewe wanawake unawachezea tu, na mbaya zaidi kila mwanamke unayelala naye lazima umshawishi muende kwa mpalange

Na kuna uzi mmoja niliona umecomment kutetea biashara ya ukahaba isizuiwe, sasa mnataka maadili halafu serikali ikichukua hatua ya kuzuia mambo yanayovunja maadili mnalaani tena, mimi nilifikiri watu kama ninyi ndio mngekuwa wa kwanza kuacha na kukemea maovu hayo yote

Lakini matokeo yake mnajifanya mnajali maadili kumbe ninyi ndio wa kwanza kuyaharibu, huku mkileta visingizio vyenu vya kipumbavu eti kwanini mwanamke naye akishawishiwa akubali such a stupid argument, hii nchi kuna watu ni wanafiki sana asee
 
Kuna mtu juzi kasema alifukuzwa nyumbani akapewa Gari na Laki 9 cash lakini anasimulia kw machungu sana kwamba aliteseka sana ndani ya miezi miwili.

Huyu mtu ana sifa zote ulizoandika hapo juu.
Ila sina uhakika alizaliwa mwaka gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…