Kumbe dunia inaweza kuwa na njia fupi (shortcut) tukaachana na usafiri wa ndege

Kumbe dunia inaweza kuwa na njia fupi (shortcut) tukaachana na usafiri wa ndege

Kuna at least vitu viwili theory yao itakuwa proved wrong mapema sana kabla jimbi hajawika.

Cha kwanza ni kani au nguvu ya uvutano ya dunia. Ili theory yako iapply, unahitaji kutoka nje ya anga la dunia kwanza ili usiathirike na nguvu hiyo. Sasa gharama ya kutoka nje it is much viable kusafiri kwa muda mrefu from one point to another ndani ya anga la dunia kama ilivyo sasa.

Pili, motion ya dunia kwa maana ya rotation ni East-West direction. Theory yako ita-apply vipi South-North?
 
Ikiwa sasa unatumia saa 17 hadi 20 angani kwa ndege kusafiri umbali mrefu mataifa kwa mataifa!
Ipo siku wataalam watafanikisha kupata njia nyepesi ya kuitembelea dunia kwa muda mfupi sana wa dakika 20 hadi 25 tu
Nitaieleza dunia kwa mfano wa chungwa!
Kama tulivyowahi kujifunza huko zamani shule ya msingi kwamba dunia ina umbo la tufe (spherical shape)

Umbo hill ukiliweka kwa mfano wa chungwa na ukaamua kumenya baadhi ya maganda na mengine yakabakia! Ndivyo unaweza kusema kwamba, sehemu za maganda ya chungwa ambazo utaziacha kuzimenya kwa kufuata ramani ya dunia tuzifananishe na nchi kavu, sehemu zote ulizomenya tuziite bahari (maji)
View attachment 2458763
Takwimu zinadai ukiizunguka dunia (chungwa) yote (circumference) yaani kutoka tanzania non stop katika mstali mnyoofu hadi urudi tena tanzania ni takribani kilomita elfu 40 tu yaani 40075km

Umbali ambao unaweza kuufikia hata kwa gari dogo( hata magari ya kuagiza toka japani yatumika zaidi ya hizo kilomita)

Hivyo endapo utaamua kuishia nusu ya safari inamaanisha utakuwa umetembea 20037km tu katika mzunguko wa kuizunguka dunia kwa juu!

Mfano utokee Argentina upae kwa ndege hadi uchina tufanye iwe ni nusu ya safari, then ukiendelea mbele urusi upae kuizunguka dunia kama mlima hadi ufike tena Argentina utakuwa umefanya mzunguko wote!

Sasa basi kuepusha hayo yote! Tuamue kuitoboa dunia kama ambavyo tunaweza kulitoboa chungwa kutoka upande mmoja hadi mwingine patakiwa na umbali gani?

Ikumbukwe mfano wetu wa chungwa kuwa, palipo na maganda ndipo hapa ardhini tunapoishi, palipomenya ni maji na nyama ya chungwa iwe ni tabaka la ardhi

Hivyo basi tukitoboa dunia kwa mtindo huo inatulazimu tujue umbali huu wa tundu
View attachment 2458788View attachment 2458790
Na kwasababu umbali wa wa mzunguko tunao tunaweza kuutumia kupata eneo na kipenyo cha dunia ambacho ndilo tobo (tundu) lenyewe!

Hivyo kama dunia ina eneo la kilomita za mraba million 510, basi Eneo la dunia =pai mara kipeuo cha pili cha kipenyo,

Ambapo kipenyo halisi itakuwa sawa na kilomita 12762km umbali ambao ni kama kutoka Dar to bukoba mara 5 tu (to & fro) ambao ni umbali mfupi sana!

Hivyo umbali huo kama ukichorongwa ili kupata shimo (tunnel) kwa ule mfano wetu wa kutoboa chungwa!

Mathalani tobo lianzie ardhi ya Argentina huko lije kutokeza katika ardhi ya China maana yake umbali utakuwa ni 12762km tu!
Umbali huu ni mfupi sana!
View attachment 2458806
Sasa swali umbali huo kwenye shimo tutaufikia kwa muda gani kupita?

Bila shaka kwenye shimo hilo hakutahitajika nguvu kubwa sana kusafiri, ni kitendo cha kujitupa tu kama shilingi shwaa kama jiwe kwa kutegemea nguvu ya gravitational!

Na kwakuwa wataalam wanasema speed hubadilika hewani kadri ya umbali kwa umbali huo ni takribani dakika 19 hadi 20 tu unakuwa umefika nusu ya dunia (katikati), na baada ya kufika nusu kipenyo cha shimo, speed itaongezeka zaidi hivyo hadi kufika upande wa pili itachukua jumla ya dakika 26 hadi 27 tu kuikatiza dunia katikati.

Bahati mbaya sana gravitational itakurudisha tena na tena kinyume chake (vice versa)

Uzuri wake tu ni kwamba umbali huu unafikika BURE pasipo kutumia ndege, Bali ni mseleleko wa nguvu ya dunia! (Hii ni kutokana na formula ya umbali ni sawa na nusu ya gravitational zidisha kwa kipeuo cha pili cha muda)

Lakini mawazo hayo ya kuitoboa dunia kupata njia fupi ya kutumia muda mfupi wa dakika 20 tu hayawezi kufanikiwa kwa sasa hadi pale teknolojia na vifaa vitavyoweza tumika kutobolea vitapatikana!

Kwa sasa haiwezekani kwasababu!

Tabaka la ardhi hii ukifanikiwa kuchoronga umbali wa 100km utakutana na joto la ajabu takribani sentigrade 280℅ na ukizidisha kuchoronga joto ardhi linasadikika linaweza kupanda hadi sentigrade 600% na zaidi, ukifanikiwa kuchoronga hadi katikati ya dunia utakutana na madini chuma ya moto zaidi ya sentigrade elf 10 na zaidi joto ambalo linaweza kuyeyusha hadi mtambo wako na wewe mwenyewe ukageuka uji! Hivyo hilo wazo la kuitoboa dunia litabakia kuwa kipengele!

Dunia ina mengi ya kuendelea kujifunza! Fundi samico tunajifunza mengi muda wa ziada tusipokuwa na kazi!

Fundi ujenzi na umeme Samico Tanzania ni jopo la mafundi wazoefu pia hatuchoki kujifunza mambo ya duniani

Tunajifunza namna mpya tofauti za kuondoa kero kwa wateja wetu kiufundi!
Namshukuru Mungu wateja wetu wengi tumewatatulia shida zao kwa gharama nafuu kabisa!

Ukitaka ramani za ujenzi tunachora pia kwa elfu 50 tu kwa chumba (hii ni bei ya nyumba zote ambazo siyo za ghorofa)

Matatizo ya ujenzi,wiring mbovu, upotevu wa umeme na umeme wa akiba sasa imekuwa historia kwa wateja wetu hususani kipindi cha mgao!

Unaweza kutupigia kwa +255711756341 au tembelea ukurasa wetu huko instagram @samico_tanzania
Kwa nini ushauri kitu ambacho unajua hakiwezekani? Serikali inapokataza bangi ni kuepusha watu na mawazo ya kibangi bangi kama yako
 
Nashangaa kwa ujuzi ulio nao bado hujauliza swali kwamba kama dunia ni tufe kama chungwa, kwa nini hatuanguki tunapotembea juu yake?

Na nikuulize swali, kama tukitobia dunia, na umeshasema Diameter ya dunia ni sijui 127,000km, basi tutasafirije hizo km 127000 kwa dakika 20 hadi 25 tu?

Swali jiingine, joto la volkano na geothermal vinatoka wapi?

Sasa tangulia katoboe, ila angalia hii picha hapa chini itasaidia kukupa ramani ya kutoboa

View attachment 2459015
Ukitumia formula ya falling object!
Ambayo
Umbali =0.5gt^2 note! g~9.8
Badilili hizo kilometa kuwa mita

Utapata muda t in second!

Badili second kuwa dakika ndo utapata muda huo! Kwamba endapo zikafanyiwa kazi changamoto za joto, na kusiwepo kuzuizi basi Dakika 20 tu zinatosha kutoka upande mmoja kwenda mwingine!
 
Kwa nini ushauri kitu ambacho unajua hakiwezekani?
Waliobuni drone walifeli mara 100 kuipaisha! Leo ndo inatumika kurekodi matukio hadi kwenye mpira!

Kuwaza siyo dhambi! Tumelemazwa sana na hesabu za haiwezekani!

1-2 tuliamishwa haiwezekani! Lakini baadae tukajifunza kumbe inawezekana!

Hapo kinachoferisha ni namna na kifaa gani wanaweza kutumia kisiweze kuathilika na joto Kali na presha Kali kutoka Inner core!

Yamkini kunaweza tokea madini magumu zaidi kutoka sayari nyingine wakaja yatumia kama nyenzo! Lakini kwasasa ni terrible idea ambayo ni ngumu sana!
 
Sijasoma yoote.. Ila nimemkumbuka captain moudy physics kwenye SIMPLE HARMONIC Motion
 
Ukitumia formula ya falling object!
Ambayo
Umbali =0.5gt^2 note! g~9.8
Badilili hizo kilometa kuwa mita

Utapata muda t in second!

Badili second kuwa dakika ndo utapata muda huo! Kwamba endapo zikafanyiwa kazi changamoto za joto, na kusiwepo kuzuizi basi Dakika 20 tu zinatosha kutoka upande mmoja kwenda mwingine!
Kwa hiyo kwa acceleration ya gravity ya 9.81 M/S2 uta cover distance ya 127,000km in 20 minutes?
Diameter of earth = 12,742,000,000m
Acceleration = 9.81m/s2
Falling object (initial velocity is zero)

(Final velocity)squared = 2 x g x D (g = accltn, D = earth diameter)
V suared = 2 x 9.81m/ss x 12,742,000,000m
Final Velocity = Square root of (2 x 9.81 x 12,742,000,000)
= 499998m/s = 1,799,992.8 km/hr

Kwa hiyo, ili kitu kianguke kwa free fall kumaliza Diameter ya dunia from zero speed, assumption ni kwamba kiatamaliza dunia kikiwa na speed ya 1, 799,992.8 km/hr

Hapo siingizi theory ya terminal velocity.

Sasa lets say average speed ni (initial velocity na final velocity )/2 = 899,996.4 km/hr

Kwa hiyo kusafiri kwa kukatisha ndani ya dunia from one end to the other time ni

t = d/v = 12,742,000/899,996.4 = 14.16 hrs

Lakini suala ni kamba, achilia mbali joto la earh core, umeona speed unayotakiwa kusafiri? 899,996.4 km/hr
 
Kwa walioisoma yote, huyu ni Genius au ni Bangi???
Huyu genius kuliko magenius wote, mada nzima ni umehitimishwa na tangazo la biashara ambalo akiwasilisha kwa njia ambayo wengi wataisoma , nimevutiwa sana nao kwa kweli
 
Kwa hiyo kwa acceleration ya gravity ya 9.81 M/S2 uta cover distance ya 127,000km in 20 minutes?
Diameter of earth = 12,742,000,000m
Acceleration = 9.81m/s2
Falling object (initial velocity is zero)

(Final velocity)squared = 2 x g x D (g = accltn, D = earth diameter)
V suared = 2 x 9.81m/ss x 12,742,000,000m
Final Velocity = Square root of (2 x 9.81 x 12,742,000,000)
= 499998m/s = 1,799,992.8 km/hr

Kwa hiyo, ili kitu kianguke kwa free fall kumaliza Diameter ya dunia from zero speed, assumption ni kwamba kiatamaliza dunia kikiwa na speed ya 1, 799,992.8 km/hr

Hapo siingizi theory ya terminal velocity.

Sasa lets say average speed ni (initial velocity na final velocity )/2 = 899,996.4 km/hr

Kwa hiyo kusafiri kwa kukatisha ndani ya dunia from one end to the other time ni

t = d/v = 12,742,000/899,996.4 = 14.16 hrs

Lakini suala ni kamba, achilia mbali joto la earh core, umeona speed unayotakiwa kusafiri? 899,996.4 km/hr
Angalia hapo hesabu zako hazija kama vizuri, pia! Kumbuka kwenye falling object gravity inabadilika kulingana na altitude!

Terminal velocity tumia kwenye speed zinazohitaji nguvu ya kinetic!

Kwenye falling object majibu sahihi utayapata kwa kutumia gravitational, time na distance

Mtu anaepaa kwa ndege unaweza zunguka nusu ya dunia kwa saa 15 hadi 20 halafu iweje kitu kinachodondoka kwa free fall kitumie saa 14hr kupita shortcut?

Kumbuka speed ya gravitational inaongezeka mara mbili zaidi inapofika nusu ya umbali
 
Acceleration iko pale pale bali velocity ndio inaongezeka. Terminal velocity ni concept kwamba acceleration "g" inakuwa haina effect tena ya kuongeza velocity ya falling object kwa hiyo object ina attain maximum possible velocity
 
Trip ya ndege tola Dubai hadi Sydney ni masaa 15. Sasa hiyo dunia unayozunguka kwa ndege kwa masaa 15 hadi 20 ni ipi? Fanya hesabu. Tafuta umbali wa mzunguko wa dunia halafu tumia average speed ya ndege 800km/hr
 
Anachokuambia mwenzako ni kweli kwamba " g" varies with altitudes , , ndani ya uso wa dunia au nje ya uso wa dunia, labda u-assume kwamba "g=9.81ms²" ni Constant in both cases.
 
Mkuu tumia hesabu! Kama nusu mzunguko wa dunia ni kilometers elfu 20 ndege ambayo inatembea 900~1200km/hr itakatiza anga kwa muda gani?
Achana na ndege za abiria zinazotua kusubili abilia! Hizo ni kama daladala za angani!
 
Anachokuambia mwenzako ni kweli kwamba " g" varies with altitudes , , ndani ya uso wa dunia au nje ya uso wa dunia, labda u-assume kwamba "g=9.81ms²" ni Constant in both cases.
Sawa, lakini hiyo effect nyie mnaongelea kwenda juu. Hapa tunaongelea ku-drop kitu toka juu kwenda chini shimoni, uki-assume kuwa ili uende upande wa pili wa dunia "unatumbukia kwenye shimo" kwa hiyo "g" itaongezeka badala ya kupungua.

In reality, at some point hata "ukitumbukia" kwenye shimo ili uende nchi iliyo upande wa pili wa dunia, at some point itabidi "upande juu" kwa kuwa ule upande wa pili utochomoza toka ndani ya shimo kwa kwenda juu. Complicated.
 
Mkuu tumia hesabu! Kama nusu mzunguko wa dunia ni kilometers elfu 20 ndege ambayo inatembea 900~1200km/hr itakatiza anga kwa muda gani?
Achana na ndege za abiria zinazotua kusubili abilia! Hizo ni kama daladala za angani!
Okay. Basi kuna kipmo cha earh hapo juu nimekosea. Diameter of earth =km? Hesabu yote itabadilika
 
Sawa, lakini hiyo effect nyie mnaongelea kwenda juu. Hapa tunaongelea ku-drop kitu toka juu kwenda chini shimoni, uki-assume kuwa ili uende upande wa pili wa dunia "unatumbukia kwenye shimo" kwa hiyo "g" itaongezeka badala ya kupungua.

In reality, at some point hata "ukitumbukia" kwenye shimo ili uende nchi iliyo upande wa pili wa dunia, at some point itabidi "upande juu" kwa kuwa ule upande wa pili utochomoza toka ndani ya shimo kwa kwenda juu. Complicated.

Ni hivi; g=9.81m/s² at the Earth surface, above or below the Surface g varies, above the surface it varies linearly and below the surface (underground ) it varies slightly exponentially.

Recall, high school Advanced physics.
 
Back
Top Bottom