Kumbe Kenya kwa upande wa viwanja vya mpira wametuzidi?

Kumbe Kenya kwa upande wa viwanja vya mpira wametuzidi?

Umeona sasa, Sisi tunaongelea sasahv CHAN hii wewe unaongea habari ya vikiisha, mbona Taifa inafanyiwa Sana ukarabati lakini pitch bado ya kawaida Sana?
Binafsi, hata Pitch ya Kenya naona ni mbovu.

Pitch nzuri naona ni ya Uganda.
 
Hata baada ya HT,mabomba ya maji yamefunguliwa kwa Ben stadium sijawahi kuona hata ndoo za kumwagilia
 
Kenya viwanja vipo Nairobi tu nimeona juzi Mombasa wanalalamika kubaguliwa kwa kutokujengewa kiwanja kwetu kuna
Mkapa
Chamazi
Amani na ukiweka hiki kinacho jengwa Arusha.Kenya wana Talanta Moi na nyayo na vyote vipo Nairobi
Aman kipo nchi nyingine
 
Haya, taja viwanja vya Tanzania vyenye kiwango cha kuchezea CHAN, namimi nitaje vya Kenya
Kenya wana nyayo na kasarani,hivyo viwanja vimekarabatiwq tu lakini bado avijafikia viwango vya mkapa,kasarani wamekarabati kwa zaidi usd mln 40,viwanja vyao vyote vilikua avikidhi viwango vya Fifa,na ndio maana walikua wanatumia uwanja wa malawi na uganda kwa karibia miaka 2,hii Chan ilibidi ichezwe march ila ilisogezwa mbele sababu kenya viwanja vyao avikua tayari
 
Mpira naangalizia kijijini kwenu katavi ndanindani huko
Mpira unaangalizia wapi?

Mechi zote za Kenya nimeangalia, na pitch naaona ni mbovu tu kama ilivyo ya uwanja wa Rwanda, Pele.
 
Kenya wametuzidi mambo mengi sana yani ni aibu nchi kubwa kama Tanganyika tunakiwanja bora kimoja tu
 
Back
Top Bottom