Kumbe kuoa ni kugumu hivi? Aisee mniombee niko hoi bin taabani

Kumbe kuoa ni kugumu hivi? Aisee mniombee niko hoi bin taabani

Hivi nyie wana mliokaa kwenye ndoa zaidi ya miaka kumi mmefanyeje aisee? Yaani sio poa wakuu yaani niko hoi bin taabani ndiyo kwanza ndoa yangu ina wiki mbili tu aisee najihisi kuchoka na kukata tamaa wakuu

Majukumu yamenizidi, nakosa uhuru wa kuamua mambo yangu eti lazima mshirikishane wote kwenye nyumba yaani hapa nipo hoi bin taabani fanyeni wana wajamii forum mninusuru mambo sio poa niko chupli chupli mambo yamekwama wakuuu

Ndiyo kwanza nina miaka 27 yaani naona mambo yamenielemea majukumu yanakuwa mengi sana na wakuu naombeni msaada wenu
Mnawahi kuoa mapema hivo mnakimbilia nini?😀😀.miaka 27 bado sana aisee
 
umewahi kuishi mwezi mmoja au miwili mfululizo na uliyemuoa kabla hamjaoana!?
Kwamba ukiishi naye huo muda ndio kusema? Kwamba ndoa yako haitakuwa na changamoto? Hamna lolote zaidi ya kutenda tu dhambi.

Ndoa ni takatifu na utakatifu ni wa Mungu na malaika zake, shida inakuja pale unapotaka kutumia akili zako kwenye ndoa, lazima ufeli tu, jikabidhi kwa Mungu nyuzi kama hizi zitapungua sana.
 
Ulitumwa na nani!?,umewahi kuishi mwezi mmoja au miwili mfululizo na uliyemuoa kabla hamjaoana!?, Au mlikuwa mnaviziana mpewe baraka za kijinga na jamii!?, Tatizo la ndoa linaanzia pale mnapopanga kuoana kwa kuiridhisha jamii na mbwembwe nyingi. Ila ukiishi na mtu bila masharti na mikakati mingi ya ndoa au msukumo kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki mnaishi vizuri tu tena kwa muda usiojulikana.

Ila mkianza mipango ya ndoa ikawa mingi ndo tatizo linapoanzia. Miaka 27 ulikuwa unawahi nini!?.., kama unaishi kijijini ni sawa hata ukiwa na miaka 23 tu. Ila kama ni msomi na upo town 27 unajitafutia matatizo. Muda sio mrefu utaanza kulaumu wazazi, ndugu na jamaa, baadae serikali mwisho kabisa utaanza kuilaumu CCM, nawaona humu kila lawama ni kwa CCM[emoji1787]
[emoji1][emoji1][emoji2960]
 
Taratibu mkuu!

Shida ni majukumu au shida ni kushirikishana kwenye kufanya maamuzi?

Haukua na majukumu kabla ya ndoa? Haukutegemea kua na majukumu baada ya ndoa? Haukutegemea kwamba kutakua na kushirikishana mambo yanayohusu familia?

Unataka kuishi maisha ya mtu alie single wakati uko ndani ya ndoa? Ulilazimishwa kuoa? Ulikua unawahi nini kuoa wakati bado haujakomaa kiakili? Ulidhani kuoa ni kupata papuchi ya bure tu kila siku?


Umekuja huku kutafuta sababu ya kumkimbia mkeo na kukwepa majumu? Ulitegemea tutakuunga mkono katika hilo?

Tulia na mkeo na upambane na majukumu kiazi wewe!
[emoji1][emoji1][emoji2960]
 
Hivi nyie wana mliokaa kwenye ndoa zaidi ya miaka kumi mmefanyeje aisee? Yaani sio poa wakuu yaani niko hoi bin taabani ndiyo kwanza ndoa yangu ina wiki mbili tu aisee najihisi kuchoka na kukata tamaa wakuu...
Ulikuwa hujui. Ni nidhamu tu na busara vinavyoweza kukusaidia si maombi mwanangu. Kwani ulivyooa uliomba kwanza?
 
Tuliza boli wewe, kwanza una kiherehere cha kuo mapema, utachoka haraka, ungesubiri ugonge 30 ndio uoe. Sasa hapo mkeo anafanya kazi gani? Kama hana kazi ni mama wa nyumbani tu umekwisha. Kila siku utaombwa hela za matumizi mpaka ukome. Na kama ni muajiriwa/mjasiriamali utategewa utoe hela za matumizi fumili hela ya mwanamke ni yake ila ya kwako ni yenu. All in all we ni baba hela yako ndiyo inatakiwa kutoka kila siku bila kujali mkeo naye anayo akipenda atakusaidi majukumu
 
Back
Top Bottom