Kumbe Tanzania ilikopa fedha World Bank kuendeleza bandari, DP World anakuja kutumia fedha hizo kufanya kazi ambayo Tanzania imeikopea fedha WB-SOMA


Huyo hapo Mrisho Mrisho akielezea kilichofanyika tayari bandarini mwezi Juni tu.

Sasa huyo Maria asijifanye anatoa siri kwa kitu kilichowazi na kimeelezewa na bandari yenyewe.
Sasa wewe unachomlalamikia Maria hapa ni kitu gani?

Amejisifu wapi?
 
Yaani mnyama tunamuwinda sisi, jasho linatutoka sisi, kisha DP World anakuja kutuconvince kuwa yeye ana kisu kilali zaidi tumuachie mnyama atatumegemea mapande ya nyama na sisi tunakubali. Kama huu siyo uzwazwa ni nini?

Siyo hapo tu hata Taifa gas anawekeza 200 million dollars Kenya lkn fedha ni ya kwetu sisi ndiyo tume guarantee mkopo maana yake ni kwamba akishindwa kulipa deni anayedaiwa ni Serikali ya JMTZ na siyo Taifa gas ingawaje faida inakwenda kwake na ajira Kenya, think about that kama siuo evil ni nini?
 
Una uthibitisho wa hili?
DP World wanafanya kazi Kwa maslahi ya kibiashara pekee..
Lengo kubwa ni ku control trade kupitia mikataba yenye ahadi hewa na zisizotekelezeka..

Silaha Yao kubwa ni mikataba mibovu yenye kuwalinda ,Kinyonyaji na kutisha nchi zinazoingia Kwa ushawishi wa ahadi kemukemu..
 
Haya Basi. Kumbe DPW walishaweka pua zao huko siku nyingi, wakisubiri tu wakati ili waje kijumla kutumbua!

Ila sasa jinsi walivyokuja, kufuatana na yale "makubaliano" wameona ni bora wazoe kabisa, na wala siyo kutumbua pekee!
 
Acha kuwa mmpumbavu... Unajadilije uafanisi ambao haujauona?, Tahira wewe.
Huna hoja.
Unazani DPW ndo wanaanza kufanya kazi za bandarini kwa mara ya kwanza hapa Duniani ?
kama huwajui sema tukupige shule uwajue. Nyie mnaviashiria vya ufisadi na mnajua kwa uwepo wa DPW hamtoiba kirahisi.
 
Asante.

Mwisho wengi wetu wataelewa tu namna ya haya mambo yanavyofanyika juu ya migongo yetu.
 
Possible

Lakini serikali yako ipo restricted ndio kwanza credit ratings wameipa B+ it’s a junk bond hakuna bank atakayokupa hela. Wewe unabaki na makusanyo yako, IMF, WB na donor countries; kama source yako ya revenue.

Sasa kama DPW anaweza pata mkopo huko shida yako ni good terms za ‘project agreement’ na transferable skills anazowaachia vijana wako nchini muda wake ukiisha na kuamua kutokuongezeka.
 
Wamekiweka kwenye maandishi ama mdomoni ili wakulainishe moyo wako. Usiwe biased. Huyo mkurugenzi anaweza akapigwa fungu la maisha milele atetee una uhakika
Yapo kwenye appendices 1 ya IGA uwekezaji watakaofanya DPW.
 
Whaat ?!!!!

Yaani undhani Serikali hii haikuopesheki; Unadhani Hao Walamba Asali wa Awamu hii huko wanakozunguka kila kona wanafanya nini ? Na since tuna asset za kufa mtu ambazo waasisi hawakutaka kuzifuja (unadhani kwanini baadhi ya watu walitoa tahadhari kwa kinachoendelea kwamba kuna siku tutaamka asubuhi tukute tumeuzwa)
 
Mkuu bado hujajibu swali langu!
Wanaohusika moja kwa moja na uendeshaji wa bandari wanapatikana kwa utaratibu gani?
 
Nimekuwa nauliza haya haya!
Kwanini baada ya kuwekeza zaidi ya Trillioni mbili za Kitanzania tena za mkopo tunaenda kuwagawia hawa Waarabu bandari yetu?

Kwa kweli mpaka kieleweke.
 
Hapana hao DP world wana kuja na mitambo yao pamoja na technology yao wana fanya oparation mantainance and investment manaake wata panua bandari iwe kubwa zaidi
Kwa hiyo serikali ilipoboresha bandari kwa mkopo wa IMF haikununua mitambo wala tekinolojia?
 

Naomba nikusahihishe kidogo konecranes ni kampuni ambalo inatengeneza na kuzalisha vifaa mbalimbali Kwa matumizi ya bandarini ikiwemo mobile harbor cranes [emoji911] za aina zote pamoja na rubber gantry crane (rtg) na pia wanajihusisha na mambo ya port solutions na kampuni hii ipo Finland na pia ipo kampuni nyengine inayoitwa kalmar ambayo hii pia inajihusisha pia na utengenezaji wa reach stacker,terminal tractor,straddle carriers,rmg crane, pia ipo kampuni kubwa kutoka China [emoji630] ambao ni wazalishaji wa crane za ZPMC ambazo ukienda hata huko Arab na bandari zetu za Africa zimejaa kibao cranes zake
 
Jamani huu mkataba alie nao anitumie niusome,ikibidi uwe umetafsiriwa kwa lugha yetu maridhawa.

Maana mpaka asaivi sijui kitu
 
Mkataba huu ukipitishwa naomba wananchi tuungane kuiweka CCM pembeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…