Kumbe Wakoloni walishajenga mabwawa ya umeme kama hili la Nyerere kwa kitambo sana!

Wakoloni wangeondoka Tanganyika 2000 leo tungekuwa na vini vya umeme wa nyuklia.
Walikuahidi hivyo wewe na wakakukabidhi kabisa mpangilio wa miradi waliyokuwa wamepanga kuitimiza wao?

Tuwekee hapa mchanganuo huo wa miradi waliyikuwa wamepanga kuiteke;eza ndani ya miaka sitini.
 
Hiyo miradi yooote haimsaidii mwananchi sababu bei ya umeme ipo juuu, haina afadhali kwetu sisi watu wa chini.
 
February sijamuona wala kumsikia miaka sasa: Kapotea au kapotezwa?
 
Tuache kusingizia watu wengine.Let us take full respondibility of our actions.Hao communists walikua wametushika akili??Sisi akili zetu zilikua wapi??Mbona China wao wapo na hizo siasa, tangu kipindi hicho lkn wamepiga hatua.
Haya vita vya kijinga tulivyoendekeza vyote ni shida ya communists??Uganda hapo, Kenya hawakua wajamaa wale wanatofauti na sisi??
Waafrika ni kama hatuna akili, hatuwezi jiongoza.
South Afrika baada ya weusi kushika madaraka, unaona kilichotokea??Hapo napo tuwalaumu comnunists.??Congo mpaka leo hawaelewani vizuri, madini yapo, ardhi ipo lkn maskini, Mobutu alikua ni communist na wenzake baada yake??Sudan wanatwangana mpaka leo, kuna communists huko.??
Haya Tz CCM wanavyoziba maskio na kuendekeza ubabe, kujimilikisha nchi, kukataa kuleta katiba bora,huku kukiendelea na mianya ya rushwa, ubinafsi, wizi, matumizi mabovu ya pesa, kutokuwepo kwa uwajibikaji- tukiendelea kuwa maskini, baada ya miaka 50 ijayo ambayo kwa siasa hizi za ccm, bado tutakua nyuma..NAPO TUTASEMA COMMUNISTS????Sisi watu weusi, TU WABINAFSI, hii dhambi itaendelea kututafuna mpaka milele, na tutaendelea kuwa wamwisho - just watch wanachokifanya CCM - eanatuamimisha tunaendelea na makofi kila siku, baada ya miaka 30 kutoka sasa, nchi za wenzetu zitakua mbali zaidi, then tutaanza kulaumu watu wengine.
 
Sometime huwa Waafrika tunajidharau sana. Tumechelewa ila hii project, reli tumepiga hatua ingawa tumechelewa.
Ili nchi iendelee lazima uwe na energy security, last mile road/ rail infrastructures na ujuzi (elimu)
sisi tulianza na siasa safi, viwanda na kilimo.
Kwa Marehemu JPM pamoja na dosari zake kiuchumi alikuwa sahihi katika mambo mengi likiwemo hili. bado tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye energy security na infrastructures.

Top Ten Hydropower Plants
    • Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) - Ethiopia: ~6,450 MW
    • Julius Nyerere Hydropower Dam - Tanzania: ~2,115 MW
    • Aswan High Dam - Egypt: 2,100 MW
    • Cahora Bassa Dam - Mozambique: ~2,070 MW
    • Gilgel Gibe III Dam - Ethiopia: 1,870 MW
    • Inga Dam Complex (Inga I & II) - Democratic Republic of the Congo: 1,775 MW
    • Kariba Dam - Shared by Zambia and Zimbabwe: 1,626 MW
    • Merowe Dam - Sudan: 1,250 MW
    • Tekezé Dam - Ethiopia: 1,200 MW
    • Akosombo Dam - Ghana: 1,020 MW
 
Yupo na babaake huko porini wanakula za mwisho mwisho( watu wazuri hawafi)
 
Yule mzee mpumavu nyerere aliekabidhiwa nchi ina uchumi kuzidi South Korea ndio alitutia umasikini ili atawale kwa miaka 25 kama dikteta uchwara
 
Kwahiyo mkuu kwakuwa hayo mabwawa yalishajengwa na wakoloni sisi tusijenge tuendelee kuangalia picha za wenzetu tu.
 
Ndiyo, Leo ndio ninajua kuna mabwawa ya megawatts 2,000 yaliyojengwa Africa miaka 60 iliyopita.
 
Lakini bado umeme unakatika mara kwa mara 🤣
Kuwepo kwa miradi ni jambo moja na kumanage miradi ni jambo lingine
 
Walikuahidi hivyo wewe na wakakukabidhi kabisa mpangilio wa miradi waliyokuwa wamepanga kuitimiza wao?

Tuwekee hapa mchanganuo huo wa miradi waliyikuwa wamepanga kuiteke;eza ndani ya miaka sitini.
Mipango miji, reli, mashule
 
Japo wakoloni walijenga bwawa Zambia miaka ya zamani, sidhani kama kuna shida Watanzania kufurahia kuwa na bwawa hilo sasahivi
Ni sawa na kusema Wasouth Africa wasishangilie kupata uhuru 1994 kwa sababu wenzao Tanganyika walishapata uhuru since 1961
 
Kweli imekaaje?ule uzinduzi wa kwanza umefutwa au ulikuwa nusu uzinduzi?
 
Wakoloni wangeondoka Tanganyika 2000 leo tungekuwa na vini vya umeme wa nyuklia.
Wakoloni wangebaki Tanzania ingekuwa na maendeleo lakini ambao wangefaidika na hayo maendeleo ni watu weupe
Ingekuwa kama South Africa, wazungu wangeishi vizuri kwenye neighborhood za kisasa na watu weusi ambao ndio wazawa wangeishi kwenye slums in large numbers kuliko ilivyo sasahivi
 
Wakoloni wangebaki wangeijenga nchi vizuri sawa ila kwa ajili ya watu wao tu. Sisi on the other hand tungekuwa na maisha magumu kama wasouth Africa
 
Lakini bado umeme unakatika mara kwa mara 🤣
Kuwepo kwa miradi ni jambo moja na kumanage miradi ni jambo lingine
Tupo vibaya sana kwenye kumanage vitu
Hata infrastructure za maji zipo majumbani mwa watu. Leo hii Tanzania karibia kila nyumba imeinstall mabomba ya maji, lakini maji hakuna. Kujenga miundombinu ni kitu kingine, na kuifanya ilete tija ni kitu kingine
 
Exactly
 
Wakoloni wangeondoka Tanganyika 2000 leo tungekuwa na vini vya umeme wa nyuklia.
Kwahiyo point yako bora ukoloni ungebakia au unataka ukoloni urudi tena?
Hata hizi barabara wakoloni walianza kuzilima so tusilime kwa kuwa wakoloni walianza au tusilime kuwasubiri wakoloni?
Kwani wakoloni walikuwa na Sgr? Mbona baada ya kuondoka wakoloni tumejenga Sgr au nayo tusingejenga kuwasubiri wakoloni?
Kwamba kwa kuwa jambo fulani wakoloni walilifanya basi nasi tusifanye au tusiboreshe?
Ndo maana wakoloni wakatuita watu weusi yaani mpaka bongo zetu ni NYEUSI.
 
Ethiopia ni balaa hao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…