Kumbe Wakoloni walishajenga mabwawa ya umeme kama hili la Nyerere kwa kitambo sana!

Kumbe Wakoloni walishajenga mabwawa ya umeme kama hili la Nyerere kwa kitambo sana!

Basi tungepigania kuwa na haki na usawa tu na watu weupe badala ya kuwaondoa kabisa na sisi kuchukua usukani wakati tulikuwa hatuwezi. South Africa leo hii ndio nchi pekee yenye kinu pekee cha nuclear barani Africa kinachozalisha umeme mkubwa karibia sawa na hili bwawa na kimejengwa na makaburu.
Mimi siafiki kabisa kuwabakisha wakoloni. I'm glad tuliwafukuza, Just because watu waliotake over walikuwa idiots it doesn't mean walikosea kufukuza wazungu.
Inabidi tuwe na developed black nation, so the option ni kubuild nchi, kufight na corrupt regime kama hizi za CCM na hatupaswi kukata tamaa kufanya hayo kuliko kuwaza eti tungekuwa na wazungu watujengee nchi.
Sisi wenyewe ndio tunapaswa kujenga nchi zetu. Na Tanzania inapendeza ikiwa 99% black. Sasa tunapaswa ku figure out what next. It's so annoying jinsi watu wanavyotaka kujengewa kila kitu na wazungu
South Africa wako na wazungu wao, inatosha
 
Tupo vibaya sana kwenye kumanage vitu
Hata infrastructure za maji zipo majumbani mwa watu. Leo hii Tanzania karibia kila nyumba imeinstall mabomba ya maji, lakini maji hakuna. Kujenga miundombinu ni kitu kingine, na kuifanya ilete tija ni kitu kingine

Miundo mbinu ya usambazaji umeme ipo tayari kutoka JNHPP?
 
Wakati sisi leo mwaka 2026 tunasherehekea kwa shughuli kubwa uzinduzi wa bwawa la Nyerere, Wakoloni wazungu wa Uingereza walishajenga bwawa kama hilo miaka 60 iliyopita kwa jirani zetu Zambia ( Kariba Dam), 1960 na Wareneo walijenga kama hilo Msumbiji (Cahora Bassa Dam) mwaka 1979 !
Hoja yako ni nini, sasa??
 
Hivi unajua Tanzania inanunua megawatts 100 kutoka Ethiopia.

Umeme unapitia border ya Namanga mpaka Arusha
Ilikiwa inanunua mpka Zambia na Uganda.

Kwenye usafirishaji wa umeme, muna kitu kinaitwa RESISTANCE.

Kadri umeme unavyosafiri kwenda mbali ndivyo unapoteza nguvu, na hivyo kukatika katika.
 
Ilikiwa inanunua mpka Zambia na Uganda.

Kwenye usafirishaji wa umeme, muna kitu kinaitwa RESISTANCE.

Kadri umeme unavyosafiri kwenda mbali ndivyo unapoteza nguvu, na hivyo kukatika katika.
Hii naielewa mkuu,
Najua wananunua ili wapate nafuu ya nishati...
Kusafirisha umeme kutoka Chalinze-Dom-Singida-Arusha...umeme unapungua sana njiani
 
Wakati sisi leo mwaka 2026 tunasherehekea kwa shughuli kubwa uzinduzi wa bwawa la Nyerere, Wakoloni wazungu wa Uingereza walishajenga bwawa kama hilo miaka 60 iliyopita kwa jirani zetu Zambia ( Kariba Dam), 1960 na Wareneo walijenga kama hilo Msumbiji (Cahora Bassa Dam) mwaka 1979 !
Kifupi kabisa.
1. Mradi wa umeme wa JNHP ni hatari zaidi kwa ecosystem (upstream & downstream) kuliko faida yake kwenye kuzalisha umeme.

2. Pamoja na mradi wa JNHP still bei ya umeme itaendelea kuwa juu nchini Tanganyika.

3. Mradi wa upigaji! Wakubwa wamejipigia fedha za umma kama kawaida yao.
 
Hakuna maendeleo ya viwanda bila nishati endelevu na ya uhakika. Kujenga hili bwawa, tumechelewa sana. Tulitakiwa kujenga miaka ya 80.

Hizi thermal power plant haziwezi kukwepeka, ila zina gharama kubwa sana za uendeshaji.

Namsifu sana marehemu Rais wetu JPM kwa uthubutu wake. Bila kuwa na maono na kuamua kutosikiliza makelele ya watu, ikiwemo hao wanaozindua mradi mara mbili mbili, hilo bwawa lisingejengwa
Ni sahihi mkuu, je ule wimbo wa uchumi wa gas, sijui umeme wa gas uliishia wapi? Kumbuka chama hiki hiki kilisema 2013/14 tatizo la umeme wa maji ni mabadiliko ya tabia nchi, na Magufuli alikuwa humo humo kimya kabisa. Na walisema umeme wa gas utazalisha 5,000m yaani mwingi kuliko huu wa maji wa 2,115m.

Je tungetumia hizo 7.4t tusingeweza kupata umeme mwingi kwenye bomba la gas ambalo tayari liko hapa Dar?
 
Ndio maana nakuambia huwezi kufananisha immigrants na local people

Kwanza South Africa wazungu wameijenga sana na uchumi wa South Africa ni very diverse kuanzia kwenye mining, manufacturing, banking, retail, logistics, tourism, technology nk na ndio kinavuta immigrants kukimbilia Afrika Kusini.
Mtu anaweza kuzaliwa Nigeria au Kenya, akaishi mazingira nafuu, akapata elimu, akawa skilled au tu akawa na ambition lakini nchi yake haina diverse economy kama South Africa so anaona ni heri aende South Africa, na pia kuna kitu immigrants wanacho; pressure ya "I have to make it", so wakienda South wanakuta hizi opportunities inakuwa easy ku pursue

Sasa ongelea majority of local South Africans. Hawa ni complete different people from immigrants. Hili ni kundi la watu ambalo limeishi enzi za apartheid ambako watu weusi walitengewa maeneo duni ya kuishi mbali na miji iliyojengeka vizuri, hata leo hii unaona Apartheid effect in South Africa unakuta mji umeendelea kama Cape Town af nje kidogo kuna township masikini za watu weusi. Na South Africans hawakuchagua kuishi kwenye mazingira duni ila system iliwalazimisha wake huko. Ni vigumu sana mtu aliyekulia mazingira yenye shule dhaifu, unemployment kubwa, transport expensive, industries chache, crime nyingi, poor networks, family yenye poverty akafanana na immigrant kutoka Kenya au Tz. Never hao sio watu sawa na it's so unlikely that people in black communities of South Africa waka pursue opportunities the same kama immigrants hata kama opportunities zipo hapohapo South Africa

So point yangu ni kuwa kama wakoloni wangebaki Tanzania, uchumi ungekuwa mkubwa yeah, lakini sisi ndio tungekuwa kama Black South Africans leo kutokana na many factors. On the other hands, immigrants kutoka nje ya Tz wangekuja Tz kufuata uchumi mkubwa na opportunities ila watz wangekuwa wanahangaika na basic things kwanza hata before kuenjoy hizo opportunities.

Immigrants hawatokei kwenye community zilizoishi kwenye system ya apartheid, ni different people from local South Africans.

lkn usisahahu kwamba hao unaowaita locals wa south afrika ni communists kama tu ndugu zao wa rest of afrika pia, mwafrika communists anafundishwa kuanzia utotoni kwamba capitalism ni adui yake, hivyo hao weusi wa south afrika wanaipinga capitalist south afrika na wanataka kuibomoa, imagine wanataka kubomoa the most developed country in afrika, wanataka kwenda style ya zimbabwe cha ajabu wazimbabwe wenyewe wameikimbia communist ya mugabe zimbabwe na kukimbilia south afrika halafu communsits wa sa wanataka kuigeuza sa zimbabwe, again nime-oversimplify lkn hao "locals" ndiyo wanaotaka ku-destroy south afrikan capitalistic economic system iliyofanya south kuwa south afrika, wote wanapigia kura communist anc.

hivyo hayo maisha blacks wa south afrika wanayoishi ndiyo wanayoyataka kwa maana wana-reject capitalism again nime-oversimplify najua kwamba its more complicated than that, lkn elite wa anc wanaowadanganya ni kama tu ccm politburo wa tanzagiza wao ni mabilionea ila "locals" wanaishia kwenye lindi la umaskini, weusi wa south afrika wanaweza pia kuchagua da (demoncratic allience) inayoongoza Cape town angalia cape ilivyo vizuri kulinganisha maeneo ya anc ...
 
Hii naielewa mkuu,
Najua wananunua ili wapate nafuu ya nishati...
Kusafirisha umeme kutoka Chalinze-Dom-Singida-Arusha...umeme unapungua sana njiani
Ila kwasasa wanajenga MSONGO mkubwa wa 400KV ambao unasafirisha umeme mwingi, nadhani wataacha kununua.
 
Kutaka kununua umeme Ethiopia inaweza kuwa kwa ajili ya manufaa ya watu wachache kwenye system. Huenda wameona kuna namna rahisi ya kuiba hela wakianza kufanya hivyo maana CCM na ufisadi ni kama pete na kidole
Ila kuhusu umeme unaozalishwa Tz kutosha baada ya bwawa la Mwalimu Nyerere kukamilika ni sahihi. Tena ilipaswa umeme usambazwe na ushuke bei ila for some reasons sidhani kama CCM watafanya hivyo
Hii ya umeme wa Ethiopia..ni hasa kwa matumizi ya Arusha na Kilimanjaro...
Umeme kutoka Rufiji mpaka Kaskazini..ni parefu na umeme unapotea mwingi njiani
 
Ila kwasasa wanajenga MSONGO mkubwa wa 400KV ambao unasafirisha umeme mwingi, nadhani wataacha kununua.
Wameingia mkataba, hawawezi...

Na hata kule Kagera wataendelea kununua umeme Uganda...

Huu wa Rufiji...kwa wakati huu..wanafikiria wajaribu kuuzia Zambia....

Pia Pwani na baadhi ya mikoa Kuna viwanda vikubwa vinajengwa... Kuna migodi mikubwa inajengwa Mbeya na Geita...umeme matumizi yake yataongezeka sana...

Hivyo najua Kinyerezi III ipo njiani megawatts 1,000 ...hii ni lazima ianze kujengwa ndani ya miaka 3 ..

Tukikaa kwa kuzubaa ...miaka 6 ijayo mgao wa umeme huu hapa...
 
Hii ya umeme wa Ethiopia..ni hasa kwa matumizi ya Arusha na Kilimanjaro...
Umeme kutoka Rufiji mpaka Kaskazini..ni parefu na umeme unapotea mwingi njiani
Kutoka Kilimanjaro, Rufiji ipo karibu kuliko Ethiopia
 
Mkuu ni kawaida sisi tupo nyuma kidogo.

Kama umewahi kuangalia move inaitwa HEAT ya mwaka 1995 utaona mule kuna treni ya umeme inapiga kazi na inaonekana ilijegwa miaka kibao(1950 au 60).

Vipi hapa kwetu train ya umeme imekuja muda gani?
Rekebisha hapo uliposema tupo nyuma kidogo.
 
Wakoloni wangeondoka Tanganyika 2000 leo tungekuwa na vini vya umeme wa nyuklia.
Na dar ingepangika vyema sana, sio kwa barabara hadi majengo. Viwanda vya kusukumiza mahitaji yetu ya muhimu vingekuwa vingi sana.
 
Kutoka Kilimanjaro, Rufiji ipo karibu kuliko Ethiopia
Ethiopia wanatuma umeme Kenya kwa gharama zao...pamoja na upungufu wa huo umeme utakao tokea

Umeme unatumwa Tanzania kutoka Kenya...maeneo ya Kajiado..kuja Tanzania kwa kipimo tulichokubaliana..

Hata Zambia wakitaka megawatts 300... Ni lazima tutume umeme wa ziada megawatts 330...ili kule Zambia wapate kipimo tulichokubaliana...

Umeme unaopotea njiani ..ujue ni Hela au gharama za ziada
 
communists walidanganya sana waafrika, kama tusingewasikiliza communists leo hii tungekuwa mbali sana. maputo ilikuwa inaitwa "rio of afrika" kwa jinsi ilivyokuwa inachuana na rio ya brazili zilifanana karibia kila kitu kabla ya communists kuchukuwa na kuharibu kila kitu, lobito angola was riviela kabla ya vita ya communists iliyoharibu angola kabisa.

kwanza karibia kila kitu tunachokifanya leo plan iliwekwa na wazungu, hata hili bwawa la Nyerere plan ya kulijenga ilikuwepo tangia enzi za wajerumani, cha ajabu communists walikuja wakabomoa trajectory iliyokuwepo tuliokuwa tunaenda nayo sasa miaka 60 imepita ndiyo tunataka kurudia kule kule ambako tulikukataa miaka 60 iliyopita wakati dunia imesha move on ...
Inasemekana Mjerumani aliipenda saana Tanganyika.
 
Wameingia mkataba, hawawezi...
Mauzinao ya umeme soyo kwamba mkataba lazima utekelezwe. Unanunua tu kama nyanya na kulipa au kutonunua.

Ndio maana hata YZ, inauza Kenya.

Na hata kule Kagera wataendelea kununua umeme Uganda...
Wameshasaini mkataba wa kuunga Kagera kwenye grid.
Huu wa Rufiji...kwa wakati huu..wanafikiria wajaribu kuuzia Zambia....

Pia Pwani na baadhi ya mikoa Kuna viwanda vikubwa vinajengwa... Kuna migodi mikubwa inajengwa Mbeya na Geita...umeme matumizi yake yataongezeka sana...
Ndio maana JNHPP haitokiwi kuwa kwamba ndio tumefika. Lazima miradi iongezeke tusirudi kwenye mgawo.
Hivyo najua Kinyerezi III ipo njiani megawatts 1,000 ...hii ni lazima ianze kujengwa ndani ya miaka 3 ..

Tukikaa kwa kuzubaa ...miaka 6 ijayo mgao wa umeme huu hapa...
Ndio.maana mimi sikubaliani na wanaosema bei ya imeme ishuke.

Ninachotaka TANESCO watumie hizo pesa kujenga miradi zaidi.

Tunahitaji miradi mikubwa ya GESI, NUCLEAR na Geothermal.
 
Back
Top Bottom