Kumbe wanawake wanapenda mahusiano yenye mikikimikiki

Kumbe wanawake wanapenda mahusiano yenye mikikimikiki

Nadhani mikiki inayozungumziwa hapa ni ile mwanaume anakua na mwanamke zaidi ya mmoja, kucheatiana mara kudhalilishana mara ukute vitu vya ajabu kwenye simu yake, hujakaa sawa condom kwenye gari,. mara uskie ana mchepuko mahali, muanze kurushiana vijembe na watu ( haki huu uswahili siuwezi ) ilimradi tu tafrani,. mda wote mwanamke inabidi upambane ili wewe uwe bora kuliko wengine na maugomvi yote ya namna hiyo,.

Napenda mwanaume wa kwangu pekeyangu, ambaye akisema kitu nafanya na mimi ananiskiliza,. Hiyo ukali ni personality tu na kwajinsi mimi nilivyo na mambo mengi mwanaume wangu lazima awe na sauti ili tuende sawa
Mwanaume asiye na sauti kwa maana ya bubu hamuwezi kwenda sawa...
 
Haya mambo yana root cause yake.. Sio kwa wanawake tu… Mtu yeyote aliyekulia kwenye chaos, peace inafeel like something is missing! Atatafuta excitement kwa kusababisha chaos, that’s not love.

However hata wanaume wameshazoeshwa heka heka, ukiwa mwanamke cool wanaona kama “you are not interested “
Inatokea kwenye family, hii huanza na wazazi wenyewe
Baadae mtoto anajikuta anatafuta the same chaos kwneye mahusiano. Asipopata anaacha na kwenda kwingine.

Ni tatizo kubwa mabalo linakuwa haliko addressed
 
sijajua kwa wengine,.

But To me kuna mifumo yangu ya maisha ambayo nimejitengenezea ,ninaiamini na ninayaishi tangu nikiwa mdogo ili mtu aweze kunishawishi kupita njia yake kwenye jambo lolote lile kama mwanaume anatakiwa awe na akili timamu, vitendo pamoja na mamlaka ( ukali pia kama itawezekana) ndipo tuende sawa..

kwangu nikisema mambo mengi unatakiwa utafsiri kwa namna hiyo
Haya sio mambo mengi, hii ni dalili kwamba wewe ni kichwa ngumu
 
Ni kweli wakuu huu uzi jamaa hajakurukupa mimi hapa tunaugomvi na mke wangu hatuongei karibu week na siku sasa. Chanzo ni kwamba ukianza kuongea nae kuhusu mambo ya msingi kama kutunza afya zetu na watoto wetu anakuwa km vile unamsimanga hata utumie lugha ya upole kivipi yeye hataki kukosolewa basi nimeamua kumpotezea nafanya mambo yangu kimya kimya nikitaka demu nachapa nje huko na sijari hata na yeye agawe huko atajua mwenyewe sitaki vita nyumbani kwangu. Juzi nilipika hajala kasusa tukala na vijana wangu wale ambao wananizoea sana niliwahi kuwambia humu km mnakumbuka. Jana nimemwona kapika tukala lakini sina habari nae najari damu yangu kwa 💯%
Tuishi nao kwa akili na sio hisia..
 
Tunaweza ku let go of traumas kwa kutoa machungu yaliyopo mioyoni mwetu, njia pekee ya kuondoa hayo machungu ni kuexpress jambo lililokutokea kwa mtu mwingine. Inaweza kuwa rafiki yako wa karibu au hata mzazi wako.

Pia tunatakiwa tusijilaumu kwa past yetu wenyewe tunatakiwa tuchukulie ile past kama fundisho.
Nashukuru sana mkuu.

Inaonekana kuna mahusiano kati ya kusema kitu kinachosumbua na kuondoka kile kitu.

Je kuexpress jambo hilo ni mara moja na kwa mtu mmoja pekee inatosha kuexptress ama ni lazima iwe kwa watu tofauti na iwe mara nyingi nyingi?
 
Nilikuwa natafuta hii comment, huu ndio msingi wa matatizo yote katika ukubwa wetu.

Ni chilhood experiences ambazo zinafanya wanawake au wanaume wabehave katika namna fulani.

Ndio maana ni muhimu sana kumuoa mwanamke ambaye baba yake anafanana tabia na wewe muowaji, hii itawafanya wanandoa wadumu sana kwa sababu mara nyingi mtoto wakike hudumu na mwanaume anayefanana tabia na baba yake.
Hii discussion ni ngumu sana, Asante kwa insight yako.

We fall in love with what’s familiar to us. And if familiarity feels like dysfunction, pain, or emotional confusion we will mistake those things for passion. Ndio maana they keep following their passion , chasing drama, chaos etc
 
Baada ya zaidi ya miaka kama 14 nikitoa huduma inayohusiana sana na wanawake — kuwahudumia katika mazingira mbalimbali ya kijamii na kiafya — nimekuja kugundua jambo moja ambalo haliniingii vizuri akilini, lakini kila siku ushahidi wake unazidi kujionyesha: WANAWAKE WENGI HAWAPENDI MAHUSIANO YENYE UTULIVU. Ndio, nasema hivi kwa sababu kwa macho yangu mwenyewe, masikio yangu binafsi, na ushuhuda kutoka kwa mamia ya wanawake niliowahudumia kwa miaka yote hiyo, nimeona na kusikia vilio vya ajabu ajabu.

Wanawake wengi — hasa walio kwenye umri wa miaka 30 na kuendelea — wamewahi kuwa kwenye mahusiano mazuri, yenye amani na utulivu, lakini kwa namna fulani wanayaacha au wanayasababisha yavunjike. Ukiwauliza kwa nini, hakuna sababu ya msingi wanayoweza kutoa. Mwingine atasema “nilimchoka”, mwingine “hakuni-excite”, mwingine “yule alikuwa mpole sana”, au “sijui tu... sikuwa na furaha.” Lakini huwezi kupata majibu ya msingi au yenye mantiki ya kweli. Unagundua kwamba wamejizoesha mahusiano yenye mikikimikiki — ugomvi, drama, kulia kila wiki, kuchunguzana simu, kulazwa na presha ya mapenzi.

Kuna wanawake niliowahi kukutana nao, ambao ni warembo, wenye kazi nzuri au biashara, wenye malengo maishani, lakini mpaka sasa wana miaka zaidi ya 10 kwenye safari ya kutafuta mwenza wa kudumu. Wengi wana watoto, lakini hawako kwenye ndoa, na bado wanaendelea kulia, “wanaume hawaeleweki” au “sijampata yule wa kunistahili.” Lakini ukiwa karibu nao, unagundua kwamba mara nyingi wao wenyewe ndio chanzo cha machungu yao.

Inauma kusema, lakini ni kweli: baadhi ya wanawake hawataki mahusiano yenye utulivu kwa sababu hawajazoea. Wamezoea giza kiasi kwamba mwanga unawaumiza macho. Wamezoea vurugu kiasi kwamba amani inawapa wasiwasi. Wamezoea kusumbuliwa kiasi kwamba wakipewa mapenzi ya kweli wanahisi hawastahili au wanadhani kuna kitu kinajificha.

Mwanamke ni kiumbe kisichoeleweka......
Hii ni wazi. Mmoja alinambia.. 'mapenzi bila lies hayanogi'
 
Ukiona ndoa Haina changamoto basi nyie mtakuwa mnaishi mbinguni au rafiki yenu shetani 100%
 
Si ndio mliambiwa mkae nao kwa akli au?

Ukiona mwanamme unapata tabu kwa mwanamke wa aina hio basi ujue huna akili, waache wenye akili wakae nao kwa akili.
Ndio maumbile yetu kupelekeshwa na hisia sana, hilo halikwepeki.... hormones zinatufanya tuwe na mood swings....sio maskhara mwili kupata changes kila mwezi zaidi ya mara 2 au 3 inakuwa kama kichaa
Acha kabisaa..umepita mle mle...
 
Halafu unakutana naye Akiwa ametoka huko anarudi na kusema bbe, nakupenda, nikupe French kissing - kumbe akina Pdiddy wamemnywesha mkojo wa kutosha na ametumia mdomo wake kuwalamba makalio Yao… hii kesi imenifanya niwe na kinyaa sana na hawa viumbe.
Mhh kumbe ndo yaliyojiri kwny kesi ya pididi....aiseee
 
Back
Top Bottom