Mie sipendi mtindo wa kugombania madaraka ndio yaliyomzaa jiwe, mivutano ya akina Lowassa ndio watu wakapiga kura za hasira akapatikana jiwe, tushukuru msaidizi wake ni mtu wa kutulia, na kwa kuwa alikuwa hashauriki naamini msaidizi wake akuweza toa mchango wowote kwake, na alikuja mtambua, nae alikiri kuwa na pm walinyooshwa!
 
Magufuli alijiharibia mwenyewe mkuu. Aliweka siri jinsi hiyo miradi inavyotekelezwa wananchi tunaona matokeo tu. Ni rahisi mno kuchafuliwa/kuzushiwa kwa ya kweli au yasiyo ya kweli kwasababu wananchi hawajui kilichokua kinafanyika, pesa imetumikaje, kiasi gani kimetumika na hasara kiasi gani tumepata.

Badala yake aliyaweka kwapani kazi ikawa ni kusifia tu, wanasiasa wanalinda ugali wao ndugu yangu. Kina Ndugai hawa walisifia mpaka sifa zikawaishia. Wakaomba aongezewe muda na sifa kedekede hakuna anaekosoa wala kuhoji, leo hayupo wale waliosifia hatuwaoni wakileta mitazamo yao kuhusu hili badala yake ni wananchi wanatoa tu maoni yao lakini wao wamekaa kimyaa kama hawapo vile wameshindwa kumtetea walietaka aongezewe muda.

Hili bomu aliliandaa mwenyewe kama lisingelipuka sasa 2026.. lingelipuka tu wakati hayupo madarakani. Angekua muwazi haya yasingeongelewa kwa ukubwa kama hivi.
 
Mkuu, CAG kafanya kazi yake, Swali ni Je amefanya kwa weledi? Je amelenga kweli kuiendeleza nchi au kuendeleza mfumo. Jaribu kufikiria tu iwapo JPM angekuepo ingesomwa ripoti gani?
Mkuu, unataka CAG naye badala ya ukweli, aandike tu mapambio na propaganda kama TBC, na magazeti ya Habari Leo, Uhuru na yale ya Musiba?!!!
 
Ile ripoti huwezi itengeneza ndani ya mwezi
 
ALIUA:

Azory Gwanda
Ben Saanane
Lwajabe
Aqwelina
Na mamia alitupa kwenye viroba.

Alienda Mtwara kunyang'anya korosho bila huruma,
Alivunja nyumba za wananchi wa Kimara na matusi juu,
Aliiba kura kwenye uchaguzi bila aibu,
Alikuwa anatembea na pesa za serikali kwenye mabegi wakati bajeti inapangwa na bunge,
Alihonga ukuu wa wilaya kwa mademu zake,
Alikuwa anamtaja Mungu lakini ukweli alikuwa ni shetani mkubwa!
 
Ziambie ndege zimtetee maana yeye aliona hivyo vitu ni vya muhimu kiliko maisha maisha binafsi ya watanzania
 
Achana hao na akina lema,hawana tena ushawishi wowote nchini,miradi yote aliyoiacha Magufuli imeshavuka 50%,hakuna wa kuizuia tena.miradi ikamilike wananchi wanufaike
 
Ile ripoti huwezi itengeneza ndani ya mwezi
Mkuu,Kuidoctor tu?Inawezekana kabisa.kwani JPM ana mwezi tangu amekufa?Unataka kusema kwamba CAG alijianda kusoma hii ripoti kwa JPM?
 
Alikuwa zao lamfumo mbovu
 
Kimsingi hatuna tatizo na CAG kuainisha ubadhirifu ili ufanyiwe kazi, bali tuna tatizo la kusukumia lawama zote kwa Magufuli na kutumia ripoti hii kutaka kuachana na miradi ya kutukwamua kiuchumi! Serikali yote itaponaje halafu asukumiwe lawama zote marehemu.
Mimi ningedhani serikali yote iwajibike kwa pamoja kwa kujiuzulu na uitishwe uchaguzi mkuu ili wananchi waamue!
 
I'm ready to be counted

Hawa watu wako na Agenda ya siri kina CAG na et al

Then madam ako driven na remote
 
Huyo shujaa wao nilimchukia kama kinyesi cha Gaidi.
 
Matendo yake yamtetee sio watu.
Matendo yake yapo hai kupitia maendeleo aliyotuletea!! Achana na mengine mengi hilo la kuhamishia makao makuu Dodoma lililokuwa limeshindikana miaka nenda rudi linatosha kudhihirisha ushujaa na uzalendo wa hayati Magufuli!!
 
Mkuu,Huyu bwana alikuwa worst leader kwa sababu ya mfumo wetu.Je mfumo umebadilika kama bado ni ule ule jua kwamba bado unaimbishwa
Mfumo ni ule ule

CCM ni ile ile , Furaha yangu itaongezeka maradufu siku CCM ikitolewa madarakani..
 
La mkuu wewe kiboko ...bado unstumia huu msemo ...Mabeberu!πŸ˜‚πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜†πŸ˜Š Bila shaja wewe ni Mnyonge Mwandamixi Daraja la I
 
Ninyi maccm si ndo mlikuwa mnasema Jiwe ndo rais bora zaidi, Tangia uhuru, Ndio shujaa wa Afrika kuzidi. nyerere, Nkuruma, Ghadafi n. K? Kwamba awamu ya tano Ndio awamu bora zaidi? Sasa leo mtulie matendo yake yanitetee
 
Pia kuna tofauti ndogo sana kati ya aliyeenda Shule na asiyeenda!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwisho wa kunukuu.
Elimu ya kutudumaza siyo kutufunua.
Na watawala hawawezi kutubadilishia mfumo, wanajua tutafuta viongozi, tutakataa mambo ya kutawaliwa.

Tutajua tofauti ya kuongozwa na kutawaliwa, na wanajua fika wakita kututawala tutawakataa.

Everyday is Saturday................................😎
 
Acha kushabikia Ujinga, Ndugu zako kule Kijijini wana life ngumu sana kwa sababu ya Sera za hovyo, wewe kuwa mjini ushajiona ume win sana acha ujinga sana wewe, angalia ndugu zako wanavyoteseka kule Kijijin kwenu
Ndugu zetu vijijini wanafurahi kufikishiwa HUDUMA ya umeme Wa REA, kufikishiwa huduma ya maji safi, kujengewa zahanati na vituo vya afya, elimu bure nk. Sema lingine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…