Kumbukumbu (Legacy) ya Dkt. John Pombe Magufuli
Mie sipendi mtindo wa kugombania madaraka ndio yaliyomzaa jiwe, mivutano ya akina Lowassa ndio watu wakapiga kura za hasira akapatikana jiwe, tushukuru msaidizi wake ni mtu wa kutulia, na kwa kuwa alikuwa hashauriki naamini msaidizi wake akuweza toa mchango wowote kwake, na alikuja mtambua, nae alikiri kuwa na pm walinyooshwa!
 
Magufuli alijiharibia mwenyewe mkuu. Aliweka siri jinsi hiyo miradi inavyotekelezwa wananchi tunaona matokeo tu. Ni rahisi mno kuchafuliwa/kuzushiwa kwa ya kweli au yasiyo ya kweli kwasababu wananchi hawajui kilichokua kinafanyika, pesa imetumikaje, kiasi gani kimetumika na hasara kiasi gani tumepata.

Badala yake aliyaweka kwapani kazi ikawa ni kusifia tu, wanasiasa wanalinda ugali wao ndugu yangu. Kina Ndugai hawa walisifia mpaka sifa zikawaishia. Wakaomba aongezewe muda na sifa kedekede hakuna anaekosoa wala kuhoji, leo hayupo wale waliosifia hatuwaoni wakileta mitazamo yao kuhusu hili badala yake ni wananchi wanatoa tu maoni yao lakini wao wamekaa kimyaa kama hawapo vile wameshindwa kumtetea walietaka aongezewe muda.

Hili bomu aliliandaa mwenyewe kama lisingelipuka sasa 2026.. lingelipuka tu wakati hayupo madarakani. Angekua muwazi haya yasingeongelewa kwa ukubwa kama hivi.
 
Mkuu, CAG kafanya kazi yake, Swali ni Je amefanya kwa weledi? Je amelenga kweli kuiendeleza nchi au kuendeleza mfumo. Jaribu kufikiria tu iwapo JPM angekuepo ingesomwa ripoti gani?
Mkuu, unataka CAG naye badala ya ukweli, aandike tu mapambio na propaganda kama TBC, na magazeti ya Habari Leo, Uhuru na yale ya Musiba?!!!
 
Mkuu, CAG kafanya kazi yake, Swali ni Je amefanya kwa weledi? Je amelenga kweli kuiendeleza nchi au kuendeleza mfumo. Jaribu kufikiria tu iwapo JPM angekuepo ingesomwa ripoti gani? Ninachotaka mjue ni hiki. Inukeni mdai mabadiliko ya Mfumo badala ya kushangilia kama kuku waliokatwa vichwa. Mimi nawaambia tena bila mifumo imara tutachezewa sana
Ile ripoti huwezi itengeneza ndani ya mwezi
 
ALIUA:

Azory Gwanda
Ben Saanane
Lwajabe
Aqwelina
Na mamia alitupa kwenye viroba.

Alienda Mtwara kunyang'anya korosho bila huruma,
Alivunja nyumba za wananchi wa Kimara na matusi juu,
Aliiba kura kwenye uchaguzi bila aibu,
Alikuwa anatembea na pesa za serikali kwenye mabegi wakati bajeti inapangwa na bunge,
Alihonga ukuu wa wilaya kwa mademu zake,
Alikuwa anamtaja Mungu lakini ukweli alikuwa ni shetani mkubwa!
 
Ziambie ndege zimtetee maana yeye aliona hivyo vitu ni vya muhimu kiliko maisha maisha binafsi ya watanzania
 
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
Achana hao na akina lema,hawana tena ushawishi wowote nchini,miradi yote aliyoiacha Magufuli imeshavuka 50%,hakuna wa kuizuia tena.miradi ikamilike wananchi wanufaike
 
Ile ripoti huwezi itengeneza ndani ya mwezi
Mkuu,Kuidoctor tu?Inawezekana kabisa.kwani JPM ana mwezi tangu amekufa?Unataka kusema kwamba CAG alijianda kusoma hii ripoti kwa JPM?
 
ALIUA:

Azory Gwanda
Ben Saanane
Lwajabe
Aqwelina
Na mamia alitupa kwenye viroba.

Alienda Mtwara kunyang'anya korosho bila huruma,
Alivunja nyumba za wananchi wa Kimara na matusi juu,
Aliiba kura kwenye uchaguzi bila aibu,
Alikuwa anatembea na pesa za serikali kwenye mabegi wakati bajeti inapangwa na bunge,
Alihonga ukuu wa wilaya kwa mademu zake,
Alikuwa anamtaja Mungu lakini ukweli alikuwa ni shetani mkubwa!
Alikuwa zao lamfumo mbovu
 
Anayemsulubu ni nani?
Au zile taarifa za CAG?
Ulitaka CAG aseme ATCL wanapata faida ya shilingi ngapi?

Asee hii nchi ni ngumu sana.Kwa watu wasiopenda ukweli na uwazi watakuunga mkono.

Ukweli lazima usemwe ili taifa lipone,maana haki huinua taifa.

Jambo pekee ninalotarajia,ni hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika kufanya mambo hayo.Iwapo hatua hazitachukuliwa,basi hata maana ya kuyaweka wazi haya haitakuwepo
Kimsingi hatuna tatizo na CAG kuainisha ubadhirifu ili ufanyiwe kazi, bali tuna tatizo la kusukumia lawama zote kwa Magufuli na kutumia ripoti hii kutaka kuachana na miradi ya kutukwamua kiuchumi! Serikali yote itaponaje halafu asukumiwe lawama zote marehemu.
Mimi ningedhani serikali yote iwajibike kwa pamoja kwa kujiuzulu na uitishwe uchaguzi mkuu ili wananchi waamue!
 
I'm ready to be counted

Hawa watu wako na Agenda ya siri kina CAG na et al

Then madam ako driven na remote
 
Tumtetee jpm Alie tutukana mbili Mara tatu kutwa?
Tumtetee jpm Alie ua ndugu zetu bila huruma kwa kiwatupa kwenye viroba na kuwatumia watu wasio julikana?

Tumtetee mtu ambae baada ya kutuma washenzi wakamuue lisu walimimina risasi 38, akamnyima fedha za matibabu stahili ya mbunge, akakataza watu wasiemde kumwona hospitali na hata tulipo taka kukusanyika kumwombea Lissu akakataza na hata tulipo vaa tshert za pray for Lissu akatukamata???

Tumwombee mtu Alie nyima maslahi ya wafanyakazi?
Tumwombee Alie bomoa nyumba dar na za Mwanza zilizo kua katika mpango huo akasema waziache kwa kuwa ni wapiga kura wake??

Magufuli alikua ni shetani anae tembea,
Mwizi Alie jifucha katika kichaka Cha uzalendo.

Tunamshukuru Mungu kutuondolea kansa hii Kama taifa.
KWENDA ZAKO MAGUFULI, HATUKUPENDI.
Huyo shujaa wao nilimchukia kama kinyesi cha Gaidi.
 
Matendo yake yamtetee sio watu.
Matendo yake yapo hai kupitia maendeleo aliyotuletea!! Achana na mengine mengi hilo la kuhamishia makao makuu Dodoma lililokuwa limeshindikana miaka nenda rudi linatosha kudhihirisha ushujaa na uzalendo wa hayati Magufuli!!
 
Mkuu,Huyu bwana alikuwa worst leader kwa sababu ya mfumo wetu.Je mfumo umebadilika kama bado ni ule ule jua kwamba bado unaimbishwa
Mfumo ni ule ule

CCM ni ile ile , Furaha yangu itaongezeka maradufu siku CCM ikitolewa madarakani..
 
Niseme tu kuwa Mungu akusamehe maana hujui ulisemalo na hujui kuwa unacheza ngoma ambayo mpigaji wake humfahamu!
Mabeberu waña hasira na miradi ya kutukwamua dhidi ya utegemezi kwao! Wana hasira na mradi Wa Stigler's Gorge japo umekamilika kwa karibuni asilimia 50, watasema ni faida zaidi kuachana nao na kuwaza wa gesi wakati gesi tayari tulishawakabidhi mabeberu.
Wana hasira na reli ya SGR! bila aibu watakuambia achana mradi huo una gharama sana! Ninachomshukuru Mungu vibaraka wa mabeberu wamejitokeza hadharani na tumewafahamu! Kinachosikitisha ni kuwa ni wale wale waliokuwa wanamsifu enzi za uhai wake! Huo ni unafiki wa kiwango cha kuzimu! Niseme tu kuwa watanzania kwa ujumla wetu(ukiacha wachache walio vibaraka wa mabeberu na waumini Wa ufisadi) hatukubali! And do not underestimate us!
La mkuu wewe kiboko ...bado unstumia huu msemo ...Mabeberu!😂😆😂😆😊 Bila shaja wewe ni Mnyonge Mwandamixi Daraja la I
 
Si ndio nyie mnaojidanganya kwamba akifa mtu na legacy yake anakufa nayo? Watu wa aina yako mlijitahidi kumfuta Nyerere wee na nia yake ya kujenga nchi huru inayojitegemea, lakini wapi. Ndio maana tunasema msifurahi kupita kiasi, kufa kwa JPM si kufa kwa spirit au legacy yake.
Ninyi maccm si ndo mlikuwa mnasema Jiwe ndo rais bora zaidi, Tangia uhuru, Ndio shujaa wa Afrika kuzidi. nyerere, Nkuruma, Ghadafi n. K? Kwamba awamu ya tano Ndio awamu bora zaidi? Sasa leo mtulie matendo yake yanitetee
 
Pia kuna tofauti ndogo sana kati ya aliyeenda Shule na asiyeenda!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwisho wa kunukuu.
Elimu ya kutudumaza siyo kutufunua.
Na watawala hawawezi kutubadilishia mfumo, wanajua tutafuta viongozi, tutakataa mambo ya kutawaliwa.

Tutajua tofauti ya kuongozwa na kutawaliwa, na wanajua fika wakita kututawala tutawakataa.

Everyday is Saturday................................😎
 
Acha kushabikia Ujinga, Ndugu zako kule Kijijini wana life ngumu sana kwa sababu ya Sera za hovyo, wewe kuwa mjini ushajiona ume win sana acha ujinga sana wewe, angalia ndugu zako wanavyoteseka kule Kijijin kwenu
Ndugu zetu vijijini wanafurahi kufikishiwa HUDUMA ya umeme Wa REA, kufikishiwa huduma ya maji safi, kujengewa zahanati na vituo vya afya, elimu bure nk. Sema lingine!
 
Back
Top Bottom