Matendo yake yapo hai kupitia maendeleo aliyotuletea!! Achana na mengine mengi hilo la kuhamishia makao makuu Dodoma lililokuwa limeshindikana miaka nenda rudi linatosha kudhihirisha ushujaa na uzalendo wa hayati Magufuli!!
Kuhamia Dodoma yalikuwa ni maamuzi ya mwaka 1973 ...je hoja zile,zilikuwa valid kwa mwaka 2017!
 
Acha upuuzi wewe,kwanini tusimame kumtetea mtu ambae HATUJAONA MAZURI YAKE?,halafu kila mtu ana jicho lake,wewe ungeisemea nafsi yako kuwa unamtetea,siyo ulazimishe kila mtu asimamenae au nawe.
Wataalamu wanatuonesha madudu matupu kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka mwisho,yet unataka tusimame na mtu aliyeona UMASIKINI NI FAHARI kwa jina la UZALENDO hovyo hovyo?atutie umasikini na tumchekee,we vipi mjomba!.
 
Achana na maovu yake,tuzungumzie upande wa mema.
 
Mkuu,Huyu bwana alikuwa worst leader kwa sababu ya mfumo wetu.Je mfumo umebadilika kama bado ni ule ule jua kwamba bado unaimbishwa
Lissu alishasema mapema tulipata Rais wa ajabu kuwahi kutokea watu hawakumuelewa
 
Tatizo kubwa la JPM alitaka kuongoza nchi gizani. Kwamba yeye ndo anajua njia pekee. Ukitaka kuongoza kwa kuficha ficha mambo..haya ndo matokeo yake. Mpaka leo sielewi kwa nini JPM aliviona vyombo vya habari kama adui. Alitaka kucontol habari inayomfikia mwananchi. JPM alikuwa na mapungufu just like anyone else. Lakini ubabe wake ulikuwa na athari kubwa kwa mshkamano wa taifa. Aliasisi pia au aliendekeza siasa za visasi na ubabe. Kiongozi mzuri ni yule anayeheshimiwa si kuogopwa. JPM inspired fear!

Kama taifa tuna la kujifunza. Uongo na ghiriba havifai katika uongozi.

Apumzike!
 
Tumeshaona mauozo yake,lilikuwa Jizi
Mkuu, Mimi narudia tena!! Kuna mchezo mpya unapikwa. Tusikubali iwe ni RAHISI kwa nchi yetu kuyumbishwa na watu kwa matakwa yao. Natamani Mgome ili tuwekewe mifumo imara. Hii michezo hii tunachezewa sio kabisa.
 
Kama unajua ni mchafu unataka atetewe ili iwe nini,muiaji
Magufuli alikuwa mchafu kwa sababu mfumo wetu uliruhusu awe mchafu. Mfumo bado upo na uchafu bado unaendelezwa. Shtukeni.
 
Alimfukuza ASSAD kwakuwa hakutaka mauozo yake yajulikane au yajadiliwe akiwa hai,na ndiyo maana alikuwa akituma watu wampigie debe aongeze muda ili afie madarakani,na amefia bila kuongeza muda
 
Una haki ya kueleza hisia zako kwa yale yanayoendelea, lakini hoja kama zako hizi zitaleta maumivu kwako na watu mfano wako kwa kuwa upepo umeshageuka, la msingi jitayarishe kisaikolojia ili uwendo na upepo uliyopo, mzee wetu ameshatangulia na kuna mambo mengi tu mazuri alithubutu kuyatenda lakini inaonyesha kuna vitu vya msingi alivipuuzia ndivyo hivyo vinavyopoteza ile jitihada yake katika utendaji wake wa kazi.
Sisi binadamu ni viumbe tunaohitajiana sana na tofauti zetu za kifikra na mtazamo zisiwe uadui wa kudhuriana na kutoana roho, watanzania tunaishi pamoja kwa mapenzi na kushirikiana, tumejaribu kuondoa ukabila na ndiyo maana watanzania wengi wamechanganya koo zao, tumejaribu kuondoa udini na unakuta nyumba moja kuna waislamu na wakristo na hata wasiyo na dana wanaishi pamoja wanajumuika pamoja kwenye misiba yao na harusi zao na sherehe mbalimbali. Hivyo sisi watanzania tuwe na hadhari kwa watu ambao wanataka kutugawa na kutufarikisha kama watanzania wamoja.
Tulidhani vyama vingi vya siasa ni mtihani lakini kwa mambo yaliyotokea katika uchaguzi wa 2020 ni Mungu tu ndiye anayejua umeweza kusambaritisha upinzani kwa asilimia 95, lakini bado tunaona kuna tatizo katika siasa zetu na utekelezaji wetu wa mipango ya maendeleo. Basi ni vyema tukajua mwenendo waliyouchukua CCM katika kuliongoza nchi hii haufai, ikiwa tumekubaliana tuwe na mfumo wa vyama vingi vya siasa basi tu uheshimu mfumo huo, ikiwa tuna sheria tulizotunga kwa ajili ya utendaji haki basi tuzifuate kwani hakuna aliyekuwa juu ya sheria, dhulma isipewe nafasi hata kidogo kwenye jamii yetu, kwani unaweza kumdhulumu mtu leo na kesho ukaja kudhulimiwa wewe.
Mungu huwa hadhihakiwi, tunaambiwa tumtangulize Mungu mbele kwa kila jambo letu, halafu tunaona haki haitendeki, ubagazi unatamalaki hivi Mungu wa wanasiasa ndiye yule Mungu wa wenye imani zao za dini? Ikiwa kama huna dini basi huna hata aibu kwa binadamu wenzi wako?
 
Siwezi, mtu aligeuza nyumba za ibada kuwa majukwaa ya siasa
 
Mwizi anatetewa toka lini?muuaji loho mbaya chuki husda nk
 
Hakuna cha legacy wala mavi ya legacy muda umezugumza tumeona mchele ni upi pumba ni zipi watz waliishi kwa mateso yasiyoelezeka ndugu na ripoti ya CAG ndoo msumari muhimu na wa mwisho !!! Ukwapuaji wa pesa za watu benki,watumishi kuishi kitumwa miaka mitano bila ongezeko la mshahara,makato ya kikatili ya mikopo ya wanachuo,kuchota pesa bila idhini ya bunge,kujali chato bola kuangali maslahi ya nchi,ukabila na ukanda kweupeeeee.....nk !!! Mtatetea sana ila wenye akili wamejua kila kitu hata mwezi haujaisha kwa kifupi hasafishiki
 
Jipe moyo tuuu ila mungu anaipenda Tanzania
 
Tundu Lisu alijaribu kutukana legacy ya Nyerere akakutana na nguvu ya uma.

Hatokaa arudie tena.
Sio kweli hakutuna hata kidogo acha uongo sema alitukanaje sasa mungu wenu kafa vipi mchakato wa kuongeza muda!??
 
Aristotle aliulizwa kuhusu Plato (ambaye ni mwalimu wake) akajibu: "Plato is dear to us. And truth is dear too. Nay, truth is dearer than Plato"

Nitakujibu kama Aristotle alivyojibu:
Magu si pekee ni mpendwa kwetu, "ukweli" nao ni mpendwa kwetu vilevile. Baina ya hivyo viwili, "ukweli" kwetu ni mpendwa zaidi kuliko Magu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…