Kumbukumbu (Legacy) ya Dkt. John Pombe Magufuli
Matendo yake yapo hai kupitia maendeleo aliyotuletea!! Achana na mengine mengi hilo la kuhamishia makao makuu Dodoma lililokuwa limeshindikana miaka nenda rudi linatosha kudhihirisha ushujaa na uzalendo wa hayati Magufuli!!
Kuhamia Dodoma yalikuwa ni maamuzi ya mwaka 1973 ...je hoja zile,zilikuwa valid kwa mwaka 2017!
 
Acha upuuzi wewe,kwanini tusimame kumtetea mtu ambae HATUJAONA MAZURI YAKE?,halafu kila mtu ana jicho lake,wewe ungeisemea nafsi yako kuwa unamtetea,siyo ulazimishe kila mtu asimamenae au nawe.
Wataalamu wanatuonesha madudu matupu kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka mwisho,yet unataka tusimame na mtu aliyeona UMASIKINI NI FAHARI kwa jina la UZALENDO hovyo hovyo?atutie umasikini na tumchekee,we vipi mjomba!.
 
Tumtetee jpm Alie tutukana mbili Mara tatu kutwa?
Tumtetee jpm Alie ua ndugu zetu bila huruma kwa kiwatupa kwenye viroba na kuwatumia watu wasio julikana?

Tumtetee mtu ambae baada ya kutuma washenzi wakamuue lisu walimimina risasi 38, akamnyima fedha za matibabu stahili ya mbunge, akakataza watu wasiemde kumwona hospitali na hata tulipo taka kukusanyika kumwombea Lissu akakataza na hata tulipo vaa tshert za pray for Lissu akatukamata???

Tumwombee mtu Alie nyima maslahi ya wafanyakazi?
Tumwombee Alie bomoa nyumba dar na za Mwanza zilizo kua katika mpango huo akasema waziache kwa kuwa ni wapiga kura wake??

Magufuli alikua ni shetani anae tembea,
Mwizi Alie jifucha katika kichaka Cha uzalendo.

Tunamshukuru Mungu kutuondolea kansa hii Kama taifa.
KWENDA ZAKO MAGUFULI, HATUKUPENDI.
Achana na maovu yake,tuzungumzie upande wa mema.
 
Mkuu,Huyu bwana alikuwa worst leader kwa sababu ya mfumo wetu.Je mfumo umebadilika kama bado ni ule ule jua kwamba bado unaimbishwa
Lissu alishasema mapema tulipata Rais wa ajabu kuwahi kutokea watu hawakumuelewa
 
Tatizo kubwa la JPM alitaka kuongoza nchi gizani. Kwamba yeye ndo anajua njia pekee. Ukitaka kuongoza kwa kuficha ficha mambo..haya ndo matokeo yake. Mpaka leo sielewi kwa nini JPM aliviona vyombo vya habari kama adui. Alitaka kucontol habari inayomfikia mwananchi. JPM alikuwa na mapungufu just like anyone else. Lakini ubabe wake ulikuwa na athari kubwa kwa mshkamano wa taifa. Aliasisi pia au aliendekeza siasa za visasi na ubabe. Kiongozi mzuri ni yule anayeheshimiwa si kuogopwa. JPM inspired fear!

Kama taifa tuna la kujifunza. Uongo na ghiriba havifai katika uongozi.

Apumzike!
 
Tumeshaona mauozo yake,lilikuwa Jizi
Mkuu, Mimi narudia tena!! Kuna mchezo mpya unapikwa. Tusikubali iwe ni RAHISI kwa nchi yetu kuyumbishwa na watu kwa matakwa yao. Natamani Mgome ili tuwekewe mifumo imara. Hii michezo hii tunachezewa sio kabisa.
 
Kama unajua ni mchafu unataka atetewe ili iwe nini,muiaji
Magufuli alikuwa mchafu kwa sababu mfumo wetu uliruhusu awe mchafu. Mfumo bado upo na uchafu bado unaendelezwa. Shtukeni.
 
Alimfukuza ASSAD kwakuwa hakutaka mauozo yake yajulikane au yajadiliwe akiwa hai,na ndiyo maana alikuwa akituma watu wampigie debe aongeze muda ili afie madarakani,na amefia bila kuongeza muda
Mkuu, CAG kafanya kazi yake, Swali ni Je amefanya kwa weledi? Je amelenga kweli kuiendeleza nchi au kuendeleza mfumo. Jaribu kufikiria tu iwapo JPM angekuepo ingesomwa ripoti gani? Ninachotaka mjue ni hiki. Inukeni mdai mabadiliko ya Mfumo badala ya kushangilia kama kuku waliokatwa vichwa. Mimi nawaambia tena bila mifumo imara tutachezewa sana
 
Ni dhahiri kwamba JPM ameacha legacy kubwa ambayo haijawahi kufikiwa na kiongozi Tanzania. Sikatai kwamba JPM alikuwa na mapungufu.
Legacy aliyoaicha Magufuli imekuwa changamoto kwa viongozi waliyomtangulia lakini pia waliomfuatia. Waliomtangulia ni kama vile imekuwa fedheha kwao kwa maana matendo ya Magufuli yalifungua macho watanzania kwamba kumbe kuna viongozi hawakuwajibika ipasavyo.
Lakini kwa upande mwingine ni mtihani mgumu sana kwa viongozi waliopo sana kwa yaliyofanywa na JPM inahitajika kiongozi mwenye moyo wa uthubutu kuyaendeleza.
Watu wamejipima na kuona kwamba ni kazi sana. Na pengine watakuwa hawana credibility.
Kilichobaki sasa kuchafua legacy ili kuonyesha kuwa yaliyokuwa yakifanywa na magufuli ni upuuzi tu na haupaswi kuendelezwa.

Inanifikirisha sana kuona Prof anapinga mradi HEP? Eti umeme wa HEP utatuchelewesha. Taifa ili kuweza kuwa na uchumi wa viwanda lazima pawepo na umeme wa uhakika na nafuu. Uhakika wa umeme JNHP ni kwamba kutakuwa na bwawa kubwa ambalo litahakikisha kuwepo na maji ya kusukuma mitambo kwa muda wote ambapo mvua hazitakuwepo. Lakini unafuu wa umeme wa nguvu za maji ni kwamba hakuna nishati inayotumika zaidi ya maporomoko ya maji. Umeme unaotumia nishati kama gesi, petroleum, coal nk ni gharama kwa sababu kuu mbili mosi kwa ajili nishati husika ya kuendesha mitambo ya kufua umeme na pili mitambo kuhitaji matengenezo ya mara kwa kwa mara kutokana na joto. Kwa maana hiyo gharama huo umeme utakuwa juu tu.
Ajabu Professor mbobezi leo anataka tuamini kwa ujenzi wa mradi huo ni upuuzi.
Professor huyu huyu ni mojawapo wa walioshindwa kutuletea suluhisho la tatizo la umeme matokeo wakaishia kuliingiza taifa katika gharama kwa kuingia mikataba ya kitapeli.

Jambo jingine ni Bandari ya Bagamoyo, spika wa Bunge tunaona anataka kutuaminisha kuwa JPM hakushauriwa vizuri. Ndugai enzi za Magufuli aliwahi kukiri kwamba hakujua masharti ya mkataba huo. Sasa kama ameyajua kwa nini asiyeweke bayana? Tunajua umuhimu wa bandari ya Bagamoyo lakini hatuwezi kukubaliana na masharti yasiyo na manufaa kwa taifa letu. Ndugai kama mna hoja ya kutetea Bandari ya Bagamoyo mkataba uwekwe wazi. JPM alituambia masharti ya mkataba tukakubaliana naye kama ninyi mna mkataba wenye masharti tofauti na yaliyoainishwa na JPM uwekeni bayana. Vinginevyo Bandari Bagamoyo haipaswi kabisa kuongelewa.

Yapo mengi nitaendelea lakini kwa sasa naweka kituo.
Una haki ya kueleza hisia zako kwa yale yanayoendelea, lakini hoja kama zako hizi zitaleta maumivu kwako na watu mfano wako kwa kuwa upepo umeshageuka, la msingi jitayarishe kisaikolojia ili uwendo na upepo uliyopo, mzee wetu ameshatangulia na kuna mambo mengi tu mazuri alithubutu kuyatenda lakini inaonyesha kuna vitu vya msingi alivipuuzia ndivyo hivyo vinavyopoteza ile jitihada yake katika utendaji wake wa kazi.
Sisi binadamu ni viumbe tunaohitajiana sana na tofauti zetu za kifikra na mtazamo zisiwe uadui wa kudhuriana na kutoana roho, watanzania tunaishi pamoja kwa mapenzi na kushirikiana, tumejaribu kuondoa ukabila na ndiyo maana watanzania wengi wamechanganya koo zao, tumejaribu kuondoa udini na unakuta nyumba moja kuna waislamu na wakristo na hata wasiyo na dana wanaishi pamoja wanajumuika pamoja kwenye misiba yao na harusi zao na sherehe mbalimbali. Hivyo sisi watanzania tuwe na hadhari kwa watu ambao wanataka kutugawa na kutufarikisha kama watanzania wamoja.
Tulidhani vyama vingi vya siasa ni mtihani lakini kwa mambo yaliyotokea katika uchaguzi wa 2020 ni Mungu tu ndiye anayejua umeweza kusambaritisha upinzani kwa asilimia 95, lakini bado tunaona kuna tatizo katika siasa zetu na utekelezaji wetu wa mipango ya maendeleo. Basi ni vyema tukajua mwenendo waliyouchukua CCM katika kuliongoza nchi hii haufai, ikiwa tumekubaliana tuwe na mfumo wa vyama vingi vya siasa basi tu uheshimu mfumo huo, ikiwa tuna sheria tulizotunga kwa ajili ya utendaji haki basi tuzifuate kwani hakuna aliyekuwa juu ya sheria, dhulma isipewe nafasi hata kidogo kwenye jamii yetu, kwani unaweza kumdhulumu mtu leo na kesho ukaja kudhulimiwa wewe.
Mungu huwa hadhihakiwi, tunaambiwa tumtangulize Mungu mbele kwa kila jambo letu, halafu tunaona haki haitendeki, ubagazi unatamalaki hivi Mungu wa wanasiasa ndiye yule Mungu wa wenye imani zao za dini? Ikiwa kama huna dini basi huna hata aibu kwa binadamu wenzi wako?
 
Siwezi, mtu aligeuza nyumba za ibada kuwa majukwaa ya siasa
 
Mwizi anatetewa toka lini?muuaji loho mbaya chuki husda nk
 
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
Hakuna cha legacy wala mavi ya legacy muda umezugumza tumeona mchele ni upi pumba ni zipi watz waliishi kwa mateso yasiyoelezeka ndugu na ripoti ya CAG ndoo msumari muhimu na wa mwisho !!! Ukwapuaji wa pesa za watu benki,watumishi kuishi kitumwa miaka mitano bila ongezeko la mshahara,makato ya kikatili ya mikopo ya wanachuo,kuchota pesa bila idhini ya bunge,kujali chato bola kuangali maslahi ya nchi,ukabila na ukanda kweupeeeee.....nk !!! Mtatetea sana ila wenye akili wamejua kila kitu hata mwezi haujaisha kwa kifupi hasafishiki
 
Si ndio nyie mnaojidanganya kwamba akifa mtu na legacy yake anakufa nayo? Watu wa aina yako mlijitahidi kumfuta Nyerere wee na nia yake ya kujenga nchi huru inayojitegemea, lakini wapi. Ndio maana tunasema msifurahi kupita kiasi, kufa kwa JPM si kufa kwa spirit au legacy yake.
Jipe moyo tuuu ila mungu anaipenda Tanzania
 
Tundu Lisu alijaribu kutukana legacy ya Nyerere akakutana na nguvu ya uma.

Hatokaa arudie tena.
Sio kweli hakutuna hata kidogo acha uongo sema alitukanaje sasa mungu wenu kafa vipi mchakato wa kuongeza muda!??
 
Aristotle aliulizwa kuhusu Plato (ambaye ni mwalimu wake) akajibu: "Plato is dear to us. And truth is dear too. Nay, truth is dearer than Plato"

Nitakujibu kama Aristotle alivyojibu:
Magu si pekee ni mpendwa kwetu, "ukweli" nao ni mpendwa kwetu vilevile. Baina ya hivyo viwili, "ukweli" kwetu ni mpendwa zaidi kuliko Magu.
 
Back
Top Bottom