Kumbukumbu (Legacy) ya Dkt. John Pombe Magufuli
Aristotle aliulizwa kuhusu Plato (ambaye ni mwalimu wake) akajibu: "Plato is dear to us. And truth is dear too. Nay, truth is dearer than Plato"

Nitakujibu kama Aristotle alivyojibu:
Magu si pekee ni mpendwa kwetu, "ukweli" nao ni mpendwa kwetu vilevile. Baina ya hivyo viwili, "ukweli" kwetu ni mpendwa zaidi kuliko Magu.
Na hicho alichofanikiwa Plato kukiambukiza kwa Aristotle ndicho alichofanikiwa kukiambukiza Magu kwa mamilioni ya watanzania. Watu ni wa muda tu ila yale yaliyowatambulisha ni ya kudumu. Hivi we kwa akili yako unadhani maza atajiendeshea nchi anavyotaka kisa akufurahishe wewe? Na akitaka kuteleza hatutaruhusu tena nchi iende mikononi mwa wanyanganyi. Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania sie.
 
Kwasababu kuna watu WAPUMBAVU wanataka kuwapumbaza watu ya kwamba JPM hajafanya kitu. Tunataka kuwaambia yeyote anayefikiri hivyo, aitishe Uchaguzi Mkuu haraka halafu apande jukwaani aseme JPM hakufanya kitu, awe CCM au Upinzani aone kama atatoka jukwaani salama!!!
KUTOTOKA SALAMA JUKWAANI NDO KUNAONYESHA LEGACY? Usisahau kuwa hata wauza unga huwa wanapambana na wanaowavamia... Hata wezi huwa wanapambana na polisi.... Kwa hiyo kutotoka salama jukwaani siyo alama ya kuacha LEGACY.

Tunachosema hapa kwenye vitu vinavyoonekana amefanya, kuna wizi wa kutosha... SGR serikali imekosa kiasi gani cha fedha? Ndege zimetutia hasara kiasi gani? Tena ndege zikasemewa na uwongo kwamba mwaka 2018 ziliingiza faida, wakati cureent CAG kasema zimtia hasara ya 150B kwa miaka mitano mfululizo ukiwemo huo uliosemwa kuwa zilileta faida


Yeye mwenyewe majukwani alikuwa anaonyesha watangulizi wake hawakufanya lolote la maana... alisAhau kuwa hakurudia kujenga MUHIMBILI wa vile ilikuwepo... Hakurudia kuijenga UDSM kwa vile ilikuwepo, hakuijenga SUA kwa vile ilikuwepo... HAKURUDIA KUIJENGA UDOM KWA VILE ILIKUWEPO.. HAKUIJENGA KIHANSI KWA VILE ILIKUWEPO, HAKUIJENGA MTERA KWA VILE ILISHAJENGWA NA WATANGULIZI..Hakuijenga Ifunda tech kwa vile ilikuwepo, hakujenga alikosoma yeye kwa vile kulikuwepo
 
Hiyo chuki iko wapi?Kuandika legacy aliyoacha Magufuli ni chuki?Kwa hiyo watu wanapoandika vitabu vya legacy ambazo akina Idd Amini,Hitler,Mussolini na kadhalika walizoacha ni kwamba wanaonyesha chuki?Kwa hiyo historia za watu zisiandikwe kisa walitenda maovu?
Kwanza, kubali kwamba alitenda maovu, then tulinganishe na mazuri yake, halafu tuona mzani umeelemea wapi... HUWEZI NIIBIA 10M, halfu urudi mlango wa nyuma unipe pole ya 2M, halafu mimi nibaki nakusifia kwa roho nzuri.. wakati effectively umesepa na 8M zangu... HUO NI UJINGA.
 
Legacy aliyoacha Magufuli ni hii hapa:

1.Kuondoka duniani wakati hahitajiki.

2.Kuteka wapinzani wake kama akina Azory Gwanda.

3.Kutesa wapinzani wake kwa kuwaweka ndani kila siku.

4.Kuua wapinzani wake na wakosoaji wake kama akina Ben saanane na kuwapiga wapinzani wake risasi kama ilivyokuwa kwa Tindu Lissu.

5.Kuua uhuru wa vyombo vya habari.

6.Kuua uhuru wa kujieleza kwa wananchi kama vile kufungia mitandao ya kijamii kama twitter na kukamata wanaotumia mitandao mingine kumkosoa.

7.Kuiba kura kwa kutumia Polisi,jeshi,TISS pamoja na tume ya uchaguzi.

8.Kuua biashara za watu kupitia sera mbovu za uchumi.

9.Kudanganya katika takwimu za ukuaji wa uchumi wa nchi.

10.Kuweka mihimili yote mitatu mfukoni mwake,yaani mhimili wa urais,bunge na mahakama.

11.Kuua uchumi wa nchi kupitia sheria mbovu za uwekezaji.

12.Kuua watu kwa Corona kupitia leadership negligence.

13.Kuhakikisha kuwa akina Ben Saanane na Azory Gwanda walikipata cha mtema kuni.

14.Ukabila kwa kuhamishia rasilimali nyingi za nchi katika wilaya ya Chato na kujaza wasukuma serikalini.

15 Ukanda kwa kupeleka SGR mwanza wakati siyo economic viable zone.

16.Ubaguzi wa rangi kwa kuwakandia wanawake weusi.Imagine mtu anafanya ubaguzi wa rangi karne ya 21!Is this not insane?

17.Kugandamiza demokrasia kwa kukataza vyama vya upinzani kufanya siasa wakati CCM kufanya siasa ni ruksa.

18.Kunyanyasa malaika-watoto wa kike wasirudi shule wakipata mimba.

19.Ufisadi wa kutisha kwa kufanya miradi mikubwa bila budget kupita bungeni.

20.Wizi wa kutisha wa mali ya uma kupitia kampuni yake ya Mayanga constructions LTD.Mfano uwanja wa Chato umetengenezwa na kampuni hii bila tenda kuitwa.

21.Kubambikizia kesi za kuhujumu uchumi wapinzani wake nchi nzima na kuwatupa korokoroni bila dhamana.

22.Kugushi report ya CAG ya hasara za mabilion za ndege za ATCL na kuilazimisha ATCL watoe gawio fake kwa serekali.

23.Kupora utajiri halali na wa jasho wa matajiri wa Tanzania kwa kuwabambikizia kesi fake za kuhujumu uchumi na kuwalazimisha wakiri makosa ya uwongo kisha kuwafilisi mali zao.

24.Ufisadi na wizi wa kutisha kama ulivyoibuliwa na CAG mara baada ya dikteta kufa.

Hakika hautakuwa rahisi kuifuta hii legacy.
 
Hivi report imesema fedha zimeliwa na Magufuli? Hata Magufuli akiwa bado hai report zilitoka na hati chafu zilikuwepo. Si Uongozi wa Magufuli tu, Marais wote kuanzia Mkapa. Kumekuwa na report za hati chafu.
Naona nguvu nyingiiii inatumika kumchafua. Hao waliofanya matumizi mabaya si wapo wakamatwe. Mfano Kigwa wa utalii. Kama unakumbuka Magufuli alimuonya Jafo kuhusu usimamizi wa matumizi ya fedha serikali za mitaa. Hakuna jipya.
Miaka yote pesa zimekuwa zikipigwa sana, hakuna kitu cha ajabu, ila upekee wa hii ripoti ya 2019/2020, imeonyesha kuwa kumbe licha ya majigambo yote ya meko kuwa hakuna pesq inayoliwa zilikuwa ni propaganda tu?na toka meko ameingia madarakani ofisi ya CAG, ilikuwa inafanya kazi ktk mazingira magumu sana, hata bajeti yake ilipunguzwa sana.kwani hakutaka uwazi ktk serikali yake, mwaka juzi CAG, aliposema kuwa 1.5trilioni hazijulikani matumizi yake, nini kilitokea?mala ngapi alikuwa akituaminisha kuwa ndege zilikuwa zinaleta faida?!suala la upigaji haliwezi kuisha bila mikakati mipya tena kwa sasa napendekeza itumike njia ya REAL TIME, kila mwezi fanyike ukaguzi!!tatizo la mwenda zake alifikilia kufanya mambo gizani ndio dawa ya kuonekana kuwa hakuna ubadhirifu kumbe ndio balaaa!!huyo kigwangala unayemsema kwani ripoti ya mwaka 2018/2019, ilionekana amepiga pesa MEKO alimfanya nini??NASEMA HIVI KTK AWAMU AMBAPO KUNA UFISADI WA KUTISHA UMEFANYIKA NI HIYO YA MEKO.
 
Kama unavyoinjoi fly over kenge wewe
Unaona jinsi ulivyo mjinga. Akili imejaa matusi tu. Mawazo yako finyu ni kwamba Tanzania nzima ina fly overs. Kwetu hatuhitaji hata hiyo fly over, tunahitaji dawa hospitalini, madawati shuleni na kodi rafiki na upendo wa ndugu, utu, kuheshimiana na kutopigana marisasi. Sawa wewe ndugu? ila sina uhakika kwa akili zako kama utaelewa chochote hapa. Hizo mbwembwe za fly overs ni huko kwenu tu.
 
Kwani huyu mwendazake unayempigania ana legacy ipi? Ya kupiga watu risasi? ya kutumia kibabe fedha za serikali kununua ndege nyingi zinazoliingizia hasara Taifa? Kutumia fedha za serikali kujenga kwao? Legacy ipi? Au hujui hata maana ya legacy?
Utashangaa jitu kama hili kila siku linapita ubungo interchange huku limekenua meno na halikumbuki hata zuri moja alilofanya Jpm.
 
Utashangaa jitu kama hili kila siku linapita ubungo interchange huku limekenua meno na halikumbuki hata zuri moja alilofanya Jpm.
Juzi gani kafanya yule katili shetani. Watu wengi wameumizwa kwa sababu yake. Mungu hadhihakiwi
 
Utashangaa jitu kama hili kila siku linapita ubungo interchange huku limekenua meno na halikumbuki hata zuri moja alilofanya Jpm.
Zuri gani kafanya yule Ibilisi? watu wengi wameumizwa sana na hili li jamaa. Mungu anajua kututetea watu wake.
 

Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine
 
Mbowe kabla hata ya kujisafisha na uongo wake wa kulewa na kuangushwa na konyagi kisha kulitangazia taifa kwamba amepigwa na wasiojulikana, amekuja na igizo jingine kwamba alifilisiwa na akaunti zake zote zilifungwa na TRA!!

Kama ni kweli alikuwa wapi kuyasema haya? Badala yake akawa anaitisha press conference akiwa amevaa gloves feki huku akiwa amejifungia kwenye lockdown hewa.

Ina maana Mbowe alikuwa tayari kuita waandishi wa habari na kuwaelezea alivyokimbia bunge na kwenda lockdown uchwara kuliko kuwaelezea alivyofungiwa akaunti zake zote ikiwemo ya mshahara?

Mbowe hili ni taifa la watu wanaojitambua na kamwe hutafanikiwa kwenye hiyo biashara yako mpya uliyokula 10% ili ulete chanjo ya corona nchini.
 
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche, Lema, Lissu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege.

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe, itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima Watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa

Hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni Watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea.
Muda utaongea. Hayati Magufuli kaondoka kishujaa.
 
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche, Lema, Lissu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege.

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe, itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima Watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa

Hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni Watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea.
Mmeng'ang'ania sana legacy ya Mwendazake idumu.Ikiwa ilikuwa njema,hakuna haja ya kutumia nguvu kuilinda.Itasimama kwa nguvu zake.Kama ni legacy dhaifu,iliyoharibiwa na utawala wakikatili,itayeyuka hata mkitumia jeshi kuisimika.
 
Hivi unajua hakuna aliyeijenga nchi hii kama mjerumani.legacy yake iko wapi

Hivi unajua kaburu alivyoijenga South Afrika au hujui

Hayo madude yamejengwa kwa damu na machozi ya Watanzania

Baya moja hufuta mazuri 100
Mjerumani amejenga nini mpaka ukifnanishe na mkaburu wa S.A ambaye anaishi pale mpaka leo? no naonaga waTanzania wengine ni kama mna ukichaa tu
 
Back
Top Bottom