Kumbukumbu ya moja ya tarehe mbaya kutokea (Worse Date Ever)

Unajua tunafeli pale tunaposhindwa kuongea unapopanga kukutana na mtu unayehitaji jambo na yeye muulize utakuja mwenyewe au na wenzako Majibu yake yatakupa uwanja wa wewe kukubali aje nao au umkatalie ila vijana wengi wanaona kama kuuliza ni kujiweka daraja la chini.

Nakumbuka miaka ya nyuma nikiwa nipo chuo nilipanga kukutana na mwanamke mmoja na nilimuuliza kama atakuwa mwenyewe au na wenzake na akanijibu atakuwa mwenyewe nikamwambia sawa, basi kesho yake nikafika sehem ya makutano nikaendelea kupiga vinywaji alipofika alikuwa mwenyewe ila baada ya muda akaita rafiki zake wawili nikawakaribisha vizuri sikuwa vibaya mfukoni nikawahudumia wote vinywaji na chakula wakati tunaendelea kupata chakula stor za hapa na pale nikamgeuzia kibao nkamwambia mbele ya rafiki zake kulikua na maana gani ya mm kupanga kukutana na ww tuwe wawili alaf uite rafiki zako hakuwa na majibu ila kuna rafiki yake anaonekana ana akili sana akaniambia shemeji samahani hatukujua kama mliplan kuwa wawili maana hajatuambia na yeye ndio katuita akiwa njiani mm nkawaelezea mazingira yote jinsi tulivyopanga kukutana na wale rafiki zake wakamwambia pale pale hakukua na haja japo shemej katuhudumia vizur ila angekua mtu mwingne angetukimbia nikawaambia bas mm nshasuuza nafsi yangu siku nyingine unaplan kukutana na mtu ni vyema ukazingatia makubaliano akawa amejiskia vibaya akaanza kulia akatoka na mwenzake mmoja akabaki yule mwenye akili Nkaomba namba hakusita kunipa na akaniambia napenda mwanaume anaeweza kujieleza bila kujali ataonekana vipi mbele za wanawake bas next time nkamtoa huyo rafiki mtu akaja peke yake na nikabadili gia juu kwa juu mjinga akaachwa penzi likanoga kwa rafiki mtu na yule dada alinipenda kwakua niliweza kuongea ukweli na kuwa muwazi
 
😂😂😂Mafile yaliyayuka wahudumu Mnawatesa sana🤣🤣🤣
 
Eeeeeeh ankooo unakula winga peupee 🤣🤣
 
Mi nilichogundua, sometime Hawa mademu huja na wenzao kwenye first date Ili kukwepa wasisukumiwe square pipe tu
 
Safi sana aisee....pia nimependa jinsi ulivyo muwazi. Ukapata na mdada mwenye akili.its good aisee.
 
😂😂😂Mafile yaliyayuka wahudumu Mnawatesa sana🤣🤣🤣
Sana....niligundua sometime wateja wanahamishia hasira au stress kwao. Wale wahudumu nliwaghasi sana. Bila sababu....na nilikuwa sikai nikatulia mezani...kumbe shida Files zote zimeliwa na Virus kichwani sina kitu so najibiziisha.
 
Sana....niligundua sometime wateja wanahamishia hasira au stress kwao. Wale wahudumu nliwaghasi sana. Bila sababu....na nilikuwa sikai nikatulia mezani...kumbe shida Files zote zimeliwa na Virus kichwani sina kitu so najibiziisha.
🤣🤣🤣🤣Sipati picha chumvi ingezid kidogo kwenye chakula ungehamia jikoni kabisa kupoteza mda😂😂
 
Sorry kama itakua nje ya mada...

Tulikua sehem na rafiki,tumesimama tunapiga stori,akapita mdada wa matikiti jamaa akaagiza,alivyokua anatafuna na kulifyoza hadi kinyaa,ni mara ya pili nimemfanza akaninunia mwaka mzima...

Wapili huyu ni staff senior kabisa,anakula ovyo sijapata ona,anatafuna kama mbwa koko,
Nilimfanza akasema ameshazoea awezi badilika.

Watatu ni mdada mrembo hasa,
Nilikutana nae mjini ni binti wa chuo mwaka 3,niliomba namba,tuliongea mengi,kesho wake nikamwomba tutoke na marafiki zangu kwenye chakula cha jioni.

Mdada ni mzuri marafiki zangu wote walinipongeza....
Aibu ilipoanza,nilitegemea atakuwa msikilizaji,matokeo yake ye ndio mjuaji,kila mada anadaki anachangia,chakula kilipokuja alikua anatafuna kama mbuzi,na anatafuna uku anaongea #aibu, hatulii kila saa anaminyaminya simu,kashawazoea marafiki zangu kama wanafahamiana miaka 7 nyuma,yeye anaongea pumba wakati wote,hana hekima,simu yake haishi kuita kila bada ya dk5 na anapokelea hapo hapo,mara wachambane na mashoga zake,mara huyu bodaboda wangu ananipigia sijui anataka nini....

Ilikua aibu kuu.
 
Uzi pendwa kama hizi huwa zinatembea sana kuliko zile za kupinga tozo.

Nawasubiri wazee wa kutunga stori za uongo na kweli waje wavamie huu Uzi. Wanatunga sasa hivi.
@mpwayunguvillage Njoo huku
Za tozo zinakuwa eneo lake...utazikuta kule. We huwa unapinga tozo hata ukiwa kifuani pa demu wako au kama we ni Ke jamaa yako akiwa nyuma yako anakukamua unapinga tozo? Kila jambo na wakati wake...
 
😂😂😂kunawatu wanatafuna kama manyani🤣🤣
 
Kasheshe
 
Nyingine ni miezi miwili ago nlienda Mkoa flani.basi nikamkumbuka binti mmoja ambaye tulikutana naye facebook toka mwaka 2009 tukawa friends. Kumbe baadaye akawa amepangwa kikazi huo mkoa.

Basi nilipoenda nikamweka sawa....nikambembeleza sana tuonane anipe game. Bint alikuwa anaonekana mrembo sana. Yaani ukicheck picha zake...hatari sana.

Basi siku hiyo akakubali tukale nyama choma sehemu. Nikaenda akaja hiyo sehemu... Kumcheck...daahh.... Vidole vimekomaa...usoni hayupo soft vile anavyoonekana.

Miguuni vidole kama tangawizi. Mbaya zaidi anaongea acha. Ana majidai ya kipuuzi kuwa anapata shida sana pale mkoani. Ye amezoea Dar kwenda maeneo ghali. Kule anaona kama ni bush. Anateseka sana.

Maneno mengi akipokea simu ni kuwachamba wateja wake ambao anawauzia vitu online... Anasema "mimi unajua sina mbambamba wala mbembembe..." Mi hata sielewi hayo maneno maana yake nini.

Yule dada alikuwa anaongea sijapata ona.maneno tu ya kiswazi mara anawagombeza wahudumu, mara anawafokea...mimi ndo nampoza na kuwaomba msamaha wahudumu. Tulipomaliza nikamwambia nina dharura nataka fika sehemu then nitamtafuta jioni.

Akanifuata hadi kwenye gari akaingia amekaa kushoto. Nami nimeshawasha gari. AC inapuliza tu. Amekaa anataka apige stories. Nikamkumbusha nawahi sehemu mara moja. Akaniambia kwani hatuwezi enda wote...nikamwambia hapana nitarudi....demu bado analeta stories hapo sasa kidogo nikakaza. Akashuka shingo upande.

Nlipoondoka nilikimbiza gari utadhani atanifukuzia. Nikarudi hotel nikazima na simu. Usiku nakuja washa simu msg kama zote. Sikujibu akaendelea akaona sina mwelekeo. Akaja laumu sana kuwa nlikuwa namtaka kimapenzi halafu nimechenga....

Mimi na mademu waswahili mbalimbali kabisaa....
 
[emoji16][emoji16]iyo ya kushuka na watoto ni noma[emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…