Hahahaha I went out for dinner with a guy.
Tukaagiza vinywaji pale fresh tukisubiria chakula sasa.
Mimi nikaagiza makange ya samaki yeye akaagiza kuku.
Movie inaanza kwanza kwenye kiti kakaa hatulii, mara ajinyooshe , mara ajikunye, mara anyooshe miguu hadi inafika kwangu ananikanyaga anasema aah sorry bhana.
Mimi namuuliza tu "kila kitu kipo sawa"? Anasema ndio. Mara kila saa anauliza mambo mengine vipi lakini? Mara nimefurahi umekubali kutoka na mimi. Anarudia rudia kila dakika. Basi mimi nishakwazika ila najikaza tu.
Chakula si kikaja? Anakula kama ndama? Yaani ile tafuna khaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kama ng'ombe yaani yaani ni "kata kata kata nyam nyam nyamnm" halafu hiyo kuku anainyofoa vyofoa kama ana mapengo.
Halafu hatulii, mara akapiga glass na kiwiko cha mkono pombe ikamwagikia[emoji1787][emoji1787]. Nikasema hii kali.
Nilivyotoka hapo, nikamblock.