Kumbukumbu ya moja ya tarehe mbaya kutokea (Worse Date Ever)

Kumbukumbu ya moja ya tarehe mbaya kutokea (Worse Date Ever)

Kipindi nipo Chuo siku hiyo kulikua na vimanyunyu nilitoka kwa mguu toka off-campus mpaka chuoni mwendo kama dakika 15 hivi kumfuata mrembo muda wote tunawasiliana na bibie.

Kufika namshtua nimefika anachungulia nje anaona vimanyunyu anasema hataweza kuja kuniona sababu ya mvua nywele zake zitaloa. Najaribu muelewesha lakini haelewi palepale nikamblock na kurudi zangu mdogo mdogo maghettoni, safari ya kurejea ilikua ndefu hiyo njia nzima nasonya na kutukana 😂😂😂
Na usikute wewe ndiye ulimpa hiyo hela ya salon 🤣🤣🤣
 
Mwaka 2009 wakati nipo kikazi Visiwani Zanzibar kuna mdada nilikutana nae yule dada bhana ni wa zenji ni swala tano haswa,kuna siku nipanga tukutane kwenye kamgahawa furani hivi aisee alikuja kavaa ijabu na nikabu juuu alafu ilikuwa night kiukweli nilikwazika mno tulivyoachana,

Nikamweleza sikupenda ulivyovaa wakati tuna date akaniomba nimsamehe date ya pilu ilifanyikia gest kiukweli siku hii nilimsaliti mke wangu na mwanamke wa kipemba kilichofanya nisiendelee nae tena yani tumetoka kudate faragha na nilikuwa nikipiga na withdraw ila cha kushangaza anasema ana mimba nilimblock pale pale mpaka leo hata sijuaigi yuko wapi yule binti.
Mtoto akija kufanikiwa ndio utataka uwe baba au sio?
 
Na hawa watoto wa kike ukiwatoa out daah! Umejiroga asee! Yaani hawaionei huruma pesa yako, wanaitafuna bila huruma.
Mimi tatizo huwa linalonikumba ni mawazo tu ya pesa nilizotumia kwenye date yaani kesho yake huwa nakosa raha sana!,ndio nikapata mbadala wake kwamba dating zote ziwe ghetto kwangu kuepuka gharama
 
Hahahaha I went out for dinner with a guy.
Tukaagiza vinywaji pale fresh tukisubiria chakula sasa.
Mimi nikaagiza makange ya samaki yeye akaagiza kuku.

Movie inaanza kwanza kwenye kiti kakaa hatulii, mara ajinyooshe , mara ajikunye, mara anyooshe miguu hadi inafika kwangu ananikanyaga anasema aah sorry bhana.

Mimi namuuliza tu "kila kitu kipo sawa"? Anasema ndio. Mara kila saa anauliza mambo mengine vipi lakini? Mara nimefurahi umekubali kutoka na mimi. Anarudia rudia kila dakika. Basi mimi nishakwazika ila najikaza tu.

Chakula si kikaja? Anakula kama ndama? Yaani ile tafuna khaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kama ng'ombe yaani yaani ni "kata kata kata nyam nyam nyamnm" halafu hiyo kuku anainyofoa vyofoa kama ana mapengo.

Halafu hatulii, mara akapiga glass na kiwiko cha mkono pombe ikamwagikia[emoji1787][emoji1787]. Nikasema hii kali.

Nilivyotoka hapo, nikamblock.
[emoji3][emoji3][emoji3] et mambo mengine vip
 
niko na mshkaji wangu kaita demu mahali pa starehe!!
jamaa alikuwa na hela siku hiyo akaona aite dem mkali huyo ili aoshe hapo.
nipo nae pale akanipa warning mapema kwamba bia ninywe za 1500 tu.ili nisimalize ela yke.

muda kidogo wakaingia mapisi mawili makali kinyama.

mi niko mkimya tuu nanyonya kilimanjaro.msela anapiga windok!
manzi wakaagiza savana mbili mbili kila 1.

jamaa kwa amri akaniambia nemda kaweke oda ya kuku pale na chips!

madem wako savana ya 12 jamaa windok3 mi kili3.msosi ukaja.

jamaa akajivunga kula kwamba ameshiba.mi nnajua hajala wala nini ni ile asionekane anapenda kula!hahaha.nikasema huyu leo nitamuoshea subiri.

Hapo nikaanza kula na wale madem huku tunapiga stori wanafurahia stori zng kinoma.jamaa ananiangalia jicho baya.hahaha mi ndo kwanza namenya tuu mapaja ya kuku.

wale mademu waligusa gusa tuu kisupa women ule msosi ukabak mwingi tuu.nikaita muhudumu aje aufunge na foil kisha aweke jikon isipoe.kwba tunakunywa tukiskia njaa tena tunauitisha.

madem wakamaliza savana zao za 16 pale wakaaga wanaenda kitchen then watatuchek mida hivi wakitoka.

wametoka pale tuu nikaita mhudum alete ule msosi.hata sijamaliza kuufungua jamaa akauvutia kwake alipiga ule msosi km katoka somalia vile.

hahahaha
 
Hahahaha I went out for dinner with a guy.
Tukaagiza vinywaji pale fresh tukisubiria chakula sasa.
Mimi nikaagiza makange ya samaki yeye akaagiza kuku.

Movie inaanza kwanza kwenye kiti kakaa hatulii, mara ajinyooshe , mara ajikunye, mara anyooshe miguu hadi inafika kwangu ananikanyaga anasema aah sorry bhana.

Mimi namuuliza tu "kila kitu kipo sawa"? Anasema ndio. Mara kila saa anauliza mambo mengine vipi lakini? Mara nimefurahi umekubali kutoka na mimi. Anarudia rudia kila dakika. Basi mimi nishakwazika ila najikaza tu.

Chakula si kikaja? Anakula kama ndama? Yaani ile tafuna khaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kama ng'ombe yaani yaani ni "kata kata kata nyam nyam nyamnm" halafu hiyo kuku anainyofoa vyofoa kama ana mapengo.

Halafu hatulii, mara akapiga glass na kiwiko cha mkono pombe ikamwagikia[emoji1787][emoji1787]. Nikasema hii kali.

Nilivyotoka hapo, nikamblock.
Nimecheka sana,inshort you have made my day.
 
Mambo mengine vipi lakini mtoto mzuri?[emoji2][emoji2]

Kilichokuwa kinapelekea yeye kuwa kwenye hiyo hali ni nini?

Mambo mengine vipi lakini?
 
1. Baada ya kunitafuta sana nikaona nimsikilize hata na hivyo nilikuwa bored! Tukapanga siku ya kuonana, cha kushangaza jamaa anang’ang’ania tuonane kuanzia saa5 usiku maana ndo ana muda (anakuwa katoka kazini) na sio kwamba tunaenda kwake au sehemu ya kificho. Nikasema sawa! Siku ya date nimejiandaa vizuri, baada ya kumuelekeza sana mpaka nilipo, hatimaye kufika na kuniambia yuko nje tayari! Kutoka nakuta kaja na eicher (daladala ya tegeta gerezani nadhani). Mhh nikatamani kutoa sababu ya uongo nirudi ndani ila jamaa akawa kama kitu cha kawaida mbona na amechangamka sana nikasema anyway na kujiandaa kote huku wacha niende tu!
Tukaelekea sehemu ya karibu tu maana sikutaka kwenda mbali na ile daladala! Kufika sehemu na baada ya kukaa huku nikitaka kumuuliza maswali mawili matatu, ghafla ananiambia mbona bado unatafuna big g? Nikamjibu si naweka mdomo fresh tu! Ghafla nashangaa mtu katoa kalamu na karatasi ‘minus 1’ yaani kwenye marks zangu keshapunguza moja! Ndipo nikajua nipo na chizi baada ya hapo nilimlima block[emoji18]
 
2. Siku ya birthday yangu! Tumeenda date sehemu akaniletea cake! Kufungua keki tayari imekatwa nusu, kuumuuliza akasema nyumbani kwao wamekata! Nikasema sio case, tukakata pale kidogo na kuendelea kula chakula kingine! Muda wa kuondoka nashangaa anaibeba keki yote! Vipi???? Eti anawapelekea ofisini kwake!!!! Eeh kwakweli kuna vitu vinashangaza, nae alikula block

3. Huyu alikuwa kawaida tu! Siku tunatembea ‘evening walk’ kuna watoto wakawa wanacheza wakikimbizana huku na huku na kule! Wakawa kama wanatusumbua lakini si ni watoto who cares??? Eeh mwenzangu uvumilivu ukamshinda akampiga mtoto mmoja kwenzi zito sana. Mimi na watoto wengine ikabidi tumshangae, huku aliyepigwa akilia! Jamaa hana habari. Kwakweli baada ya tathmini baadae nikaona nimblock tu.
 
Duh, mbona date zako za kiswahili sana. Mara upunguziwe maksi, mara keki nusu. Unawatoa wapi hao jamaa?
 
Duh, mbona date zako za kiswahili sana. Mara uounguziwe maksi, mara keki nusu. Unawatoa wapi hao jamaa?

Mkuu nashindwa kuelewa labda unisaidie kutafakari!

4. Huyu mwingine date ilienda vizuri kabisa! Maongezi yalikuwa mazuri tena intelligent! Everything was good ingawa kuna kitu ambacho alikuwa anafanya nikawa naona kama weird saingine naona kawaida (alikuwa akiangalia kifua changu sana). Baada kurudi nyumbani na kumtaarifu nimefika salama na kusema asante! Ndipo jamaa akaniuliza ‘kwa hicho kifua chako utaweza kuhimili maumivu kweli’???[emoji22]
 
Back
Top Bottom