Kumekuwepo na Tishio la Kiusalama linalotokana na Mgogoro wa Mpaka Kati ya Tanzania na Uganda

Kumekuwepo na Tishio la Kiusalama linalotokana na Mgogoro wa Mpaka Kati ya Tanzania na Uganda

Migogoro ya mipaka Uganda mara ya mwisho tuliimaliza kwa vita, Waganda wakumbuke hilo pia.

Umemsikia Mama anasema hataki mchezo wa kuingiliwaingiliwa ovyo na watu wa nje?

We unaona akili zinamtosha yule?

Na akitoka yule tuna tumaini lolote?

On a serious note, mgogoro wa mpaka wa Malawi ni mkubwa kuliko huu, hii ni taharuki tu.
Wa ziwa Nyasa ndio chai yenyewe hii mingine ni mbwembwe tu
 
Check wanajeshi wa JWTZ wanavyodhalilishwa huko Rwanda👇👇

Jeshi la TZ linajuaga kupigana na raia tu wasio hata na wembe.
View attachment 3341263
Na huyu si kapteni kabisa huyu? Mkute baa sasa anavyotunisha misuli. Au boda ajichanganye achukue demu wake. Anakuja na wenzake kupiga mtaa mzima. Jeshi likiwa na uhusiano mbaya na raia hilo siyo jeshi tena. Mungu Awape busara vijana hawa maana ndiyo tegemeo letu la mwisho kama nchi. Na ni jeshi la sita kwa ubora duniani!
 
Na huyu si kapteni kabisa huyu? Mkute baa sasa anavyotunisha misuli. Au boda ajichanganye achukue demu wake. Anakuja na wenzake kupiga mtaa mzima. Jeshi likiwa na uhusiano mbaya na raia hilo siyo jeshi tena.
Ndicho wanachoweza. Kupiga raia wasio na mafunzo wala wembe
Mungu Awape busara vijana hawa maana ndiyo tegemeo letu la mwisho kama nchi. Na ni jeshi la sita kwa ubora duniani!
Jeshi la sita, hizo taarifa za mchongo.

Nilishangaa kuona msemaji wa JWTZ anasema eti tu-gugo😅😅😅


Anajua hizo taarifa za Google nani anaweka???
 
Ndicho wanachoweza. Kupiga raia wasio na mafunzo wala wembe

Jeshi la sita, hizo taarifa za mchongo.

Nilisha gaa kuona msemaji wa JWTZ anasema eti tu-gugo😅😅😅


Anajua hizo taarifa za Google nani anaweka???
Yani msemaji anatumia taarifa za google kurank jeshi la JWTZ..!?..NI hatari aisee
 
Halafu mnasema kwanini mwarabu ananunua silaha wakati hata vita hapigani

Jamani hata mataifa makubwa hayataki vita ila angalia wanavyotengeneza silaha
Na bajeti kubwa ya Ulinzi lazima

Wenzetu Kenya wanatengeneza bunduki na sasa wanazo pia pistols

Sisi tunaenda kuanglia awamu ya kwanza ya kivuko nani sijui
 
Katika taarifa ya hali ya ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi iliyowasilishwa katika taarifa ya bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ya mwaka 2025/26, Tanzania imeeleza kuwa kumekuwepo na tishio la kiusalama katika mpaka wa Tanzania na Uganda kutokana na mgogoro wa kimpaka."Hali ya usalama katika mpaka huu wenye urefu wa kilomita 397.8 ni shwari.

Hakuna tukio la kuhatarisha usalama wa nchi yetu," ilieleza ripoti hiyo ya Wizara."Pamoja na hali hii, kumekuwepo na tishio la kiusalama linalotokana na Mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Uganda.

Pamoja na jitihada za kumaliza mgogoro huu, bado serikali ya Uganda inaendelea kudai kuwa mpaka wake na Tanzania katika eneo la Kagera unapita katika 01° kusini mwa ikweta badala ya marundo ya mawe yaliyopo," taarifa hiyo inaeleza.

Wizara ilieleza zaidi kuwa mazungumzo yanaendelea chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Source: The Chanzo
Tuka mfurushe Nduli Museveni au?
 
Museveni mtu wetu tumemuhifadhi Upanga pale Mindu na Maliki anadaiwa bill za umeme na simu hajalipa mpaka leo na kakimbia mpaka bili ya taxi. Madereva wa Taxi wa zamani wa Muhimbili walikuwa wanamtafuta awalipe kawakimbia, hajamaliza madeni yetu, hakuna mgogoro hapo.
😃😃😃😃😃😃 Daaah
 
Uganda na Rwanda wakiamua this time ile Kagera ndani ya wiki tu itakuwa mikononi mwao.

Huku JWTZ saivi kazi yao ni kuchimba kokoto na kujenga fremu kwenye kambi zao za jeshi.

TISS ndo maiti kabisa saivi kazi yao ni kujikombokomba kwa CCM kuchukua kodi za Wananchi kuhonga Wapinzani ili kuviua vyama imara vyenye lengo la kuwakomboa kweli Watanzania kutoka kwenye umaskini.
 
Yani msemaji anatumia taarifa za google kurank jeshi la JWTZ..!?..NI hatari aisee
 
Kutokana na hulka ya siasa kwa sasa amani na usalama wa nchi hiiunategemea tuu autonomous ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Kiufupi mataifa yote dunian hasa yanayo pakana huwa wanapenda kuaa na access of power to each other. Hivyo ikipatikana gap lazima watu wanapenyeza monitors zao.
Hata sisii tanzania tunatamani tuwe na access ya kucontrol majirani zetu.

Vivyo hivyo hatasis kama wadau wameliona gap hawawezi liacha kivyovyote.
Mfano 1.
Hivyo tunavyokata viuno vya kupongeza wanasiasa kuna wanaotuchora udhaifu wetu na wanaweza kuwa wanasifa wazuri kuliko hata wazawa ili wapenye kwenye nyeti za taifa letu.

Mfano 2.Hii hulka ya kuhonga wapinzan ili wasilim siasa, maadui hawaioni kama tabia za CHADEMA(wapinzan) ila ni tabia za watz hivyo wanaweza nunua watu muhimu wenye kuwafanikishia agenda zao.
Hili suala la migogoro ya tz na majirani zetu sio jambo la kuchukulia poa kihivyo. Hasa kama ni jambo la kimkakati ya wanazengo basi turudi kwenye utimamu chaap,maana tutashangaa inakuwa from simple to complex, mara paaap! Mv bukoba imelalia upande.
 
Back
Top Bottom