Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Wewe kijana nyuzi zako huwa za hovyo sana sana.
Zaidi ya viulizo vingi hamna kitu umeandika.
Ndugu yangu mambo yangu usipoyafanya ukaona kwa macho huwezi kunielewa
 
UKO SAHIHI, nyumba mbili nilizonazo hapa mjini pesa niliyotumia kujengea ningesema niwekeze naona ningekua mbali sana, NI Jana tuu nmetoka kuwaza na kusema SITAKAA NIJENGE TENA! hizi nilizonazo zinanitosha kwasasa nafocus na kutengeneza mzunguko WA pesa zaidi
 
Sema ukiwa na familia makazi ni muhimu sana.
Ingawa uliyosema ndio uhalisia wenyewe.

Kwanza ukiwa na hela unajenga unapopataka na nyumba unayoitaka. Na kwa muda unaopenda iwe imekamilika inakamilika..
 
Kwa hiyo unataka kuniambia Ili kufanikiwa, katika hii biashara yategemea mazingira uliomo,pia uwe na mtaji mkubwa au sio.
 
Hakuna biashara isiyoingiza faida. Tatizo watu wengi wakiambiwa kitu fulani kinalipa wanakurupuka kukifanya bila kufanya utafiti wa kutosha. Mfano mtu anajenga nyumba ya mil 50 chanika anlkitegemea imlipe.

Kwanza kabisa unatakiwa kuelewa kwamba majengo huwa hayapandi thamani, kinachopanda thamani ni ardhi(location) iliyobeba jengo.
Hivyo hakikisha thamani ya jengo unalojenga inaendana na location yake.

Pili kulingana na location unatakiwa kujenga jengo linaloweza kurudisha angalau 1% ya uwekezaji wako kwa mwezi. Mfano ukijenga nyumba ya mil 30 basi hakikisha umeijenga sehemu ambayo inaweza kukupa si chini ya 300k kwa mwezi.
 
Ona huyu mwenye nyumba uniambie anazeeka akiwa na stress ? Wewe ndio unachagua maisha yako uteseke ujanani au uzeeni.
Your browser is not able to display this video.
 
Kama huna ujanja wa kuzungusha fedha, usiweke benki, wekeza kwenye assets. Ardhi uliyonunua m2 miaka miwili iliyopita, ukiuza sasa unapata faida kubwa kuliko benki.
 
Mambo mengi kweli hapo
 
Nikweli boss, zungusha hela utapata ya kujenga nyingine tano, kodi inachelewesha sana kwa mtu mwenye haraka
 
Sema ukiwa na familia makazi ni muhimu sana.
Ingawa uliyosema ndio uhalisia wenyewe.

Kwanza ukiwa na hela unajenga unapopataka na nyumba unayoitaka. Na kwa muda unaopenda iwe imekamilika inakamilika..
Nikweli mkuu nyumba watakayoishi familia haingizi chochote bora iwe ya kawaida kwanza uendelee kuzungusha
 
Nikweli mkuu, Chanika pale nn tatizo kila mtu anapasema vibaya
 
Chanika siyo tatizo, tatizo liko kwa wawekezaji. Ukitumia formula nzuri unapiga hela. Mfuatilie Issa tambuu
Nikana kwamba hawawekezi Chanika sio, nilipata taarifa kuwa Chanika mwisho Meru Petrol Station ndiye kaiweka pazuri pia kitendo cha Makamu wa raisi Mh Philip Mpango kuwa na familia pale ameipandisha hadhi
Pale Chanika mwisho wanaokula hela pale ni jenga uza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…