Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Wewe kijana nyuzi zako huwa za hovyo sana sana.
Zaidi ya viulizo vingi hamna kitu umeandika.
Ndugu yangu mambo yangu usipoyafanya ukaona kwa macho huwezi kunielewa
 
UKO SAHIHI, nyumba mbili nilizonazo hapa mjini pesa niliyotumia kujengea ningesema niwekeze naona ningekua mbali sana, NI Jana tuu nmetoka kuwaza na kusema SITAKAA NIJENGE TENA! hizi nilizonazo zinanitosha kwasasa nafocus na kutengeneza mzunguko WA pesa zaidi
 
Sema ukiwa na familia makazi ni muhimu sana.
Ingawa uliyosema ndio uhalisia wenyewe.

Kwanza ukiwa na hela unajenga unapopataka na nyumba unayoitaka. Na kwa muda unaopenda iwe imekamilika inakamilika..
 
Nikweli mkuu inachelewesha sana, Trump huwa hapangishi watu wa kipato cha chini ni sawa na wewe upangishe chumba cha 100K kwa 300K lakini pia kuna charges anaongeza mfano ataweka security ya kampuni yake mwenyewe utawalipa pia, ataweka waudumu wa kampuni yake wa kukusaidia chochote unachotaka ndani ya apartment yako utalipia pia na mazaga mengine kibao
Yaani atafanya biashara yake ndani ya apartment yako ndiyo maana anazikusanya yaani hakuachii kitu
Kwa hiyo unataka kuniambia Ili kufanikiwa, katika hii biashara yategemea mazingira uliomo,pia uwe na mtaji mkubwa au sio.
 
Hakuna biashara isiyoingiza faida. Tatizo watu wengi wakiambiwa kitu fulani kinalipa wanakurupuka kukifanya bila kufanya utafiti wa kutosha. Mfano mtu anajenga nyumba ya mil 50 chanika anlkitegemea imlipe.

Kwanza kabisa unatakiwa kuelewa kwamba majengo huwa hayapandi thamani, kinachopanda thamani ni ardhi(location) iliyobeba jengo.
Hivyo hakikisha thamani ya jengo unalojenga inaendana na location yake.

Pili kulingana na location unatakiwa kujenga jengo linaloweza kurudisha angalau 1% ya uwekezaji wako kwa mwezi. Mfano ukijenga nyumba ya mil 30 basi hakikisha umeijenga sehemu ambayo inaweza kukupa si chini ya 300k kwa mwezi.
 
Ona huyu mwenye nyumba uniambie anazeeka akiwa na stress ? Wewe ndio unachagua maisha yako uteseke ujanani au uzeeni.
 
Kama huna ujanja wa kuzungusha fedha, usiweke benki, wekeza kwenye assets. Ardhi uliyonunua m2 miaka miwili iliyopita, ukiuza sasa unapata faida kubwa kuliko benki.
 
Haina kufichaficha nilitumbukia biashara kachumbari kununua miti kuchana na kuuza, butchery, spea, pombe, cigarettes na takataka nyingine
Maisha nikuunga unga usifanye biashara moja changanya
Hakuna biashara moja itayokupa fedha nyingi ukitaka nyingi fanya bishara nyingi tofauti
Mambo mengi kweli hapo
 
UKO SAHIHI, nyumba mbili nilizonazo hapa mjini pesa niliyotumia kujengea ningesema niwekeze naona ningekua mbali sana, NI Jana tuu nmetoka kuwaza na kusema SITAKAA NIJENGE TENA! hizi nilizonazo zinanitosha kwasasa nafocus na kutengeneza mzunguko WA pesa zaidi
Nikweli boss, zungusha hela utapata ya kujenga nyingine tano, kodi inachelewesha sana kwa mtu mwenye haraka
 
Sema ukiwa na familia makazi ni muhimu sana.
Ingawa uliyosema ndio uhalisia wenyewe.

Kwanza ukiwa na hela unajenga unapopataka na nyumba unayoitaka. Na kwa muda unaopenda iwe imekamilika inakamilika..
Nikweli mkuu nyumba watakayoishi familia haingizi chochote bora iwe ya kawaida kwanza uendelee kuzungusha
 
Hakuna biashara isiyoingiza faida. Tatizo watu wengi wakiambiwa kitu fulani kinalipa wanakurupuka kukifanya bila kufanya utafiti wa kutosha. Mfano mtu anajenga nyumba ya mil 50 chanika anlkitegemea imlipe.

Kwanza kabisa unatakiwa kuelewa kwamba majengo huwa hayapandi thamani, kinachopanda thamani ni ardhi(location) iliyobeba jengo.
Hivyo hakikisha thamani ya jengo unalojenga inaendana na location yake.

Pili kulingana na location unatakiwa kujenga jengo linaloweza kurudisha angalau 1% ya uwekezaji wako kwa mwezi. Mfano ukijenga nyumba ya mil 30 basi hakikisha umeijenga sehemu ambayo inaweza kukupa si chini ya 300k kwa mwezi.
Nikweli mkuu, Chanika pale nn tatizo kila mtu anapasema vibaya
 
Chanika siyo tatizo, tatizo liko kwa wawekezaji. Ukitumia formula nzuri unapiga hela. Mfuatilie Issa tambuu
Nikana kwamba hawawekezi Chanika sio, nilipata taarifa kuwa Chanika mwisho Meru Petrol Station ndiye kaiweka pazuri pia kitendo cha Makamu wa raisi Mh Philip Mpango kuwa na familia pale ameipandisha hadhi
Pale Chanika mwisho wanaokula hela pale ni jenga uza
 
Back
Top Bottom