Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Mambo si ndo hayo, ingekuwa ni kodi za jengo angepata wapi hiyo 15m watu wengi ni woga unawamaliza wanakimbilia assets
Sasa nakuelewesha ndugu yangu Nyumba haijengwi kwa ajili ya kukusanya kodi. Bali kwa ajili ya kuombea mikopo banki pale unapohitaji mtaji wa kufanikisha ishu yako ya haraka. Kama wewe ni mfanyabishara mkubwa ukawa na shida ya ghafla ya m 100 kama hauna nyumba unafanyaje? Hapo ndio ma- donn wa mjini wanakuja kukupiga bao. Kuhusu Tolu mmiliki wa bucha alikuwa na nyumba tatu nzuri hapa town Na kikjijini kwao Iringa alijenga nyumba nzuri sana ya kisasa.
 
Wewe ndio umeongea cha maana kuna watu wana idea nzuri ya maana ila hawawezi kupata mtaji. Ila kuna watu wana assets anaweza kupewa mkobo hadi wa billioni mbili within two days. Kuhusu mikopo nimeshuhudia mambo mengi sana. Kuna wakati nilikuwa naona client anajenga hoteli amekopa banki na banki hio hio imeikopesha kampuni inayomjengea client. Kuna watu walianzisha biashara mpya kariakoo wakongwe wenye majumba wakachukua mkopo na kwende kuchukua mzigi mara kumi ya wao wakateka soko. Unadhani wangewekeza bondi wangeweza, Kaeni karibu na watu wa wizara ya atdhi iuna miradi kibao ya kuboresha unaweza ukajua wapi kutakuwa hot cale ndani ya miaka mitano ijayo. Kuna watu walinunua survey, sinza na maeneo ya karibu mwaka 1996 maana mipango ya kujenga mlimani city iliikuwa ndiyo inaanza. Vijana wanaogopa vitu vigumu lakini jua amua uteseke leo au uteseke uzeeni. Ukijibana na kununua sehemu ya potential ni rahisi kutoboa. Kule Mbeya kuna sehemu inaitwa Iwambi kuna jamaa zangu kibao walipawahi mapema sana. Ni kuishi na watu vizuri tu. Ipo mifano mingi sana kuanzia Goba, Mbweni hadi Kinyerezi. Sasa ni mwwendo wa kuamka na kutambua sehemu nyingine zinazochipukia. Namalizia kwa kusema Hakuna bishara unaweza kufanya bila ya kumiliki au kuitumia ardhi. Kama hiyo biashara ipo naomba je uilete hapa na unieleweshe.
Zipo nyingi ngoja waje
 
Kama umekusudia kumsaidia MTU inatakiwa utaje na mradi unaozungushia pesa yako hiyo utakuwa umetusaidia kwa kiasi kikubwa.
 
Mimi nahangaika hapa kumbe napoteza nguvu zangu bure 😅😅😅😅😅apaa Jamiiforum Ptuu !!!
Huyo achana nae kwasababu anafikiri wanaodai haki ni mafukara
Huwezi kuacha kudai chenji ya 200 kwasababu eti una laki moja
 
Kuna mzee alinunua kiwanja 600,000 huko Daslamu nasikia alikiuza 370m+ sijui nilitaka kusema nini🐼
Kilichomsaidia ni roho ya subra, kwa mwenye haraka ya pesa hawezi kusubiri muda wote huo
Kuna watu wana haraka ya pesa anataka pesa ya moto kabla haijapoa mfano mm huwa siwezi kufanya uwekezaji wa muda mrefu
 
Ndio maana wazungu wengi hawajihangaishi kujenga.

Wazungu wengi ulaya na Amerika wanaishi kwenye apartments.

Pia wengi wana nunua nyumba na kulipa mortgage.

Wanao jenga ni wachache sana.

Wao muda mwingi ni kufanya kazi, wakipata fedha ni kula bata na kusafiri.

Waafrika ndio wanajihangaisha kujenga wakihofia eti watoto watalala wapi.

Kwa wazungu, mtoto akishafika umri wa kujitegemea anaenda kwenye apartment yake na yeye. Akapambane kulipa bills.
Sasa hao wanaoje ga apartments ni watu gani?
Na mfumo wa huko ni sawa na wa huku bongo amabpo mtoto kamaliza chuo ana dgree lakini kazi anakija pata baada ya miaka 5 ya msoto kitaa
 
Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri mkubwa, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Mimi Mr Why nataka nishare experience yangu ya umiliki wa nyumba na ardhi

Nimemiliki nyumba na ardhi kwa muda mrefu lakini havikunipa fedha za kutosha

Mwanzo nilidhani kuwa na nyumba au ardhi ni utajiri lakini baada ya kumiliki mzunguko wa fedha ulikufa kabisa kwa maana kwamba baada ya kununua hizi assets fedha nyingi ziliishia kwenye ujenzi huku nyingine zikiishia kwenye ardhi nilimaliza ujenzi lakini sikubakiwa na kitu, mzunguko wa fedha ulikatika kabisa nikawa sawa na fukara

Nilijiuliza maswali mengi kwamba kabla ya kumiliki hizi assets hela ile nilikuwa nikiizungusha nikaona nimepatia maisha manake hela unaiona mkononi

Baada ya kununua assets hela ikakata fedha yote ikalala kwenye majengo na ardhi

Nilidhani majengo yangeniingizia fedha za wapangaji lakini fedha ilikua kidogo sana nikapiga hesabu ni lini majengo hayo yatanipa fedha sawa na niliyojengea nikagundua hamna kitu

Ardhi ile nikajiuliza je nikifanya kilimo itarudisha? Nikagundua hamna kitu
Nikajiuliza je nikiuza itarudisha ile fedha? Nikagundua hamna kitu
Niligundua ardhi inapanda kidogo kidogo pia nikagundua wanunuzi wa ardhi wengi wanakuwa na hela kidogo ambazo zinapelea kidogo katika zile ulizonunulia, sana sana wanalia kupunguziwa kwa mtu mwenye uhitaji wa hela ya haraka unaanguka

Nikajiuliza je nikichukulia mikopo benk italipa? Nikagundua hamna kitu fedha ambazo benk ingenipa ni sawa na lita moja ndani ya lita tano kwahiyo ni sawa na kufaidisha bank

Basi nikakwama sana kifedha ingawa watu walipokuwa wakiona assets zangu walidhani mimi ni tajiri kumbe hamna kitu

Nikachukua uamuzi mgumu sana wa kupiga bei assets zote na kutumia ile fedha katika mizunguko yangu

Ingawa niliogopa sana nikiwaza nimejiangusha lakini nilikaza roho sawa na paka

Mwisho nilipata fedha zenye thamani ya kumiliki mara mbili ya assets nilizokuwa nazo mwanzo kwasababu nilipozungusha fedha zile nilipata mara mbili ½ ni kwasababu ya kuwa na roho ya paka, ukiwa mwoga hii kafara hutaiweza

Mpaka sasa sioni kama assets inaweza kunipa hela kwa haraka wala sina mpango wa kumiliki assets kwasasa nimegundua assets zinalaza hela afadhali nimiliki hela kuliko assets kwasababu fedha nitazungusha navyotaka mimi

Nikagundua kuwa woga ni adui wa mafanikio ningekumbatia woga mpaka sasa ningekuwa na zile assets kidogo za mwanzo

Je umeshapitia hii experience yangu? Je ulichukua hatua gani
Mkuu unazungumzia assets au liability maana unalaumu assets ila unasahau kwmb wewe bnafs hukuchagua biashara sahihi kwa mtaji uliokuwa nao
 
Mkuu unazungumzia assets au liability maana unalaumu assets ila unasahau kwmb wewe bnafs hukuchagua biashara sahihi kwa mtaji uliokuwa nao
Mwanzo wazo lilikuwa assets baadae nikafanya liability na mimi bahati mbaya ni mtu wa haraka nataka pesa ya moto siwezi kusubiri uwekezaji unaochelewa kuzaa, napenda kuzungusha haraka
 
Mr why ni kweli usemalo,uwekezaji wa majengo ukitegemea hela ya wapangaji,unapata hela ndogo na kwa mda mrefu sana,,lkn navyoona mimi si mbaya ukawekeza ktk hayo majengo lkn isiwe kwa asilimia kubwa, asilimia kubwa wekeza katika mzunguko mkubwa,utatoboa pia kimaisha,
Lkn pia naomba kujua ilikuwaje mtu kama Trump amepata faida kubwa kwa uwekezaji wa majengo?,je amefanyaje?,hadi kuanzisha biashara ingine tokana na hayo majengo (kama sijakosea).
 
Mwanzo wazo lilikuwa assets baadae nikafanya liability na mimi bahati mbaya ni mtu wa haraka nataka pesa ya moto siwezi kusubiri uwekezaji unaochelewa kuzaa, napenda kuzungusha haraka
Sa hukuwa na mtaji wa kueleweka na wala hukuchagua biashara sahihi so usidanganye watu humu kwmb biashara hiyo hailipi ksa wewe ilikushnda sbb hata nikikuliza hapa ulijenga nyumba ngapi na wp na kodi ulikuwa unalipisha kiasi gn hebu jbu hayo maswali tuone
 
Mr why ni kweli usemalo,uwekezaji wa majengo ukitegemea hela ya wapangaji,unapata hela ndogo na kwa mda mrefu sana,,lkn navyoona mimi si mbaya ukawekeza ktk hayo majengo lkn isiwe kwa asilimia kubwa, asilimia kubwa wekeza katika mzunguko mkubwa,utatoboa pia kimaisha,
Lkn pia naomba kujua ilikuwaje mtu kama Trump amepata faida kubwa kwa uwekezaji wa majengo?,je amefanyaje?,hadi kuanzisha biashara ingine tokana na hayo majengo (kama sijakosea).
Nikweli mkuu inachelewesha sana, Trump huwa hapangishi watu wa kipato cha chini ni sawa na wewe upangishe chumba cha 100K kwa 300K lakini pia kuna charges anaongeza mfano ataweka security ya kampuni yake mwenyewe utawalipa pia, ataweka waudumu wa kampuni yake wa kukusaidia chochote unachotaka ndani ya apartment yako utalipia pia na mazaga mengine kibao
Yaani atafanya biashara yake ndani ya apartment yako ndiyo maana anazikusanya yaani hakuachii kitu
 
Sa hukuwa na mtaji wa kueleweka na wala hukuchagua biashara sahihi so usidanganye watu humu kwmb biashara hiyo hailipi ksa wewe ilikushnda sbb hata nikikuliza hapa ulijenga nyumba ngapi na wp na kodi ulikuwa unalipisha kiasi gn hebu jbu hayo maswali tuone
Nyumba za kupangisha nilijenga Goba na Mbezi Luis hela za wale wapangaji zisingeweza kunifikisha popote kwa mtu mwenye kichaa cha hela ya haraka hela ya moto huwezi kuvumilia
 
Back
Top Bottom