kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
- Thread starter
- #81
Simba walitoa mlio hata baada ya Tabora kufungwa, wakatoa mlio baada ya Singida kufungwa, wakatoa mlio kwa Coastal na JKT. Kwanini ushahidi hautoki? na sio mwisho wataendelea kulia kama ng'ombe.Mngeanza nyie kwanza Simba kuonesha mfano kisha kuja kuleta ushahidi kuwa serikali iliingilia kati kuzima tuhuma za rushwa za Yanga. Maana hata nyie Simba viongozi wenu waliwatuhumu wachezaji wenu kupokea rushwa katika kipigo cha goli tano lakini cha ajabu mashabiki na viongozi wakatulia tu kimya, pasipo kuonesha kuwa wana nia ya dhati kukomesha rushwa kwa kufungua kesi juu ya hao wachezaji wake.
Mashabiki mmekuwa kama mwanamke anayenyanyaswa na mumewe ndani ya nyumba na hana pa kukimbilia anabaki kulia lia tu kila siku. Kungekuwa na ukweli wa hizi tuhuma lazima ingepelekwa ushahidi kwenye mamlaka husika, au mnataka kusema Simba na Yanga zinapendana sana kiasi kwamba wanalindiana siri?
Aishi Manula, Igonga na Chama walikula rushwa Simba ipigwe 5; mbona ushahidi hautoki?