Kumlipa Clinical Officer laki 6 sio haki hata kidogo

Kumlipa Clinical Officer laki 6 sio haki hata kidogo

Clinical officers wanafanya kazi kubwa sana kunusuru Maisha ya watu, kumlipa CO laki 6 ambayo ni sawa na Tsh elfu 20 kwa siku tena hapo bado makato sio haki hata kidogo.

Tukianza na sekondari, huyu Co alilipa ada kubwa tofauti na wanafunzi wengine wanaosoma michepuo ya biashara na sanaa.

Pia asilimia kubwa ya CO's wa sasa walipita ngazi ya advance na walilipa ada kubwa mno tofauti na michepuo mingine mf PCM, HKL, HGE, ECA nk.

CO hata Kwenda field tu analipia wakati fani zingine field hulipii Bali wewe ndiye unalipwa.

Serikali wajitahidi kumuongezea Hela CO angalau laki 8 kwa mwezi.
Tumeichagua na tumeipenda wenyewe, meza maumivu
 
Hahahahah akiacha kazi ndio ataona jinsi buku ilivyo na nguvu😅!

Kuikusanya laki 6 kwa hustling bila jasho na damu kukutoka sio masihara! Unahitaji so many sleepless nights to make that money unless otherwise uwe na mchongo umenyooka kuwa ukitia hela tu inaingiza hela.
Mkuu, mimi nimesoma Muhimbili. Nimemaliza 2016.

Yaani mfukoni hata 100 mbovu nilikuwq sina na uqezo wa kuipata sina. Nilitaabika sana.

Kila kijiwe cha waosha Magari ukienda kutafuta Kazi hupati, unakuta wamejaa, na unaambiwa kaongee na boss.

Huyo boss mwenyewe anakwambia andika jina hapo kwenye daftari tutakupigia.

Kuna siku nimewahi kwenda angalau niwe nawasaidalia kuosha magari bure tu ila wawe wananipa 1,000 ya kula lakini walikataa.

Maisha ni magumu jamani acheni.

Usione mtu ana familia yake wanakula kila siku ukaona ni mzaha🤣🤣
 
Hii tanzania mishahara nimidogo kwenye kila idara

Hebu mfikirie MD amesoma chekechea mpaka chuoni miaka 20 plus ...kutengeneza carier halafu unalipwa 1.48M per month na unafanya kazi masaa 8*6 *4 inakuwa ni saa 192......sasa chukua 1.48m gawanya kwa 192 utaona wanalipwa sh 7710 kwa saa.....yaaani unasoma miaka 20plus uje utengeneze 7710 kwa saa.......

Kama taifa inabidi tu wekeze kwa watu wanaodeliver......haiwezekani wanasiasa wanalipwa mishahara minono zaidi ya hawa raia
Kama mshahara mdogo jiajili nawe ajili watu uwalipe mishahara mikubwa
 
Mkuu game ni tuff kinyama aisee yani hela ya mtaani ni ngumu sana usione wale watumbuliwaji wanaolia na kufa na presha!

Wanajua moto wake ukifulia inakuwaje hapo kwa wife😅
 
Binadamu tunajisahau sana. Mara nyingi hata tukipata kidogo tunadhani tunastahili zaidi.

Leo mtu analipwa laki 6 analalamika lakini kuna watu wenye taaluma kama yake hawapati hata 100 mbovu🤣.

Maisha yasikie tu.

Unaweza kuona CO anafanya kazi kwenye NGO anakunja 3M ukatamani. Lakini acha kazi uone kama utaweza kupata hata hiyo laki 6 kwa mwezi.

Mimi nashukuru Mungu maisha niliyopitia yamenifunza kuangalia kila kitu kwa UHALISIA.

Kwenye maisha usipende sana kuishi kwa "INGELIKUWA HIVI, NINGE......."

Hicho unachokiona ndio halali yako kwa wakati huo.

Tembea mtaani uone watu wanarogana mpaka kwenye vibarua vya kulipwa 40,000 kwa mwezi.
Vita ya riziki sio vita ndogo mkuu! Its hard yani kutengeneza pesa sio swala dogo vita ni kali😂😂😂

Kwenye life bila kujifunza kuridhika ili uishi kwa ajili ya kuiona kesho yako utaishia kukufuru tu.!
 
Kuna graduate wanalipwa laki na nusu, wamekubali wanazikusanya ili wajipange mtu anaona laki 6 ndogo aanesotea kazi toka 2015 hajapata na ana Masters atasemaje?
Hahahahhahah kwa hali ya maisha japo hela haitoshi ila ni bora kupata laki 6 kuliko nothing!
 
Kama mshahara mdogo jiajili nawe ajili watu uwalipe mishahara mikubwa
Mkuu kujiajiri...na kumudu kuwalipa watu mishahara mikubwa inakuwa ngumu.....sababu serikali ndio single entity inayoweza kuajiri watu kwa mishahara mikubwa.....ambapo hawa waajiriwa wake wataweza kuspend ...ili na mm mwekezaji niweze kufaidika na kumudu kuajiru kwa ujira mkubwa.....
 
Hii tanzania mishahara nimidogo kwenye kila idara

Hebu mfikirie MD amesoma chekechea mpaka chuoni miaka 20 plus ...kutengeneza carier halafu unalipwa 1.48M per month na unafanya kazi masaa 8*6 *4 inakuwa ni saa 192......sasa chukua 1.48m gawanya kwa 192 utaona wanalipwa sh 7710 kwa saa.....yaaani unasoma miaka 20plus uje utengeneze 7710 kwa saa.......

Kama taifa inabidi tu wekeze kwa watu wanaodeliver......haiwezekani wanasiasa wanalipwa mishahara minono zaidi ya hawa raia
Uko sahihi kabisa.

Na ndio maana mimi huwa nawahurumia watu waliosoma CO private halafu wakaenda MD private. Sioni kama inawalipa.

Maana ada ya CO kwenye vyuo vya private siyo chini ya 2M kwa mwaka, miaka 3 ni sawa na 6M

Ukitoka hapo uende MD private ada siyo chini ya 4M kwa mwaka, miaka 5 ni sawa na 20M.

Maana yake unatumia zaidi ya 26M kusoma.

Na MD ni level ya chini sana, siyo kwamba utakuwa umemaliza.

Na system za serikali ( kama mshahra wako unatoka hazina, ukifikisha miaka 60 tu, system inakutema nje ).
 
Mkuu game ni tuff kinyama aisee yani hela ya mtaani ni ngumu sana usione wale watumbuliwaji wanaolia na kufa na presha!

Wanajua moto wake ukifulia inakuwaje hapo kwa wife😅
Hii game ngumu....mfumuko wa bei hauendani na mishahara....so inawaumiza hata wafanya biashara coz people wont spend what the dont have
 
Hao hao form 4 failures waliopata div.3 na 4 ndio unataka walipwe zaidi?

Si haki kabisa kuwapeleka watu wenye ufaulu mdogo kushughulika na usalama wa Afya zetu.Serikali komesheni huu upuuzi.

mkuu sifa za form 4 ni entry tu,utaalam unakwenda kuupata huko ndani.

utabibu sio ualimu wa hesabu.
 
Hahahahhahah kwa hali ya maisha japo hela haitoshi ila ni bora kupata laki 6 kuliko nothing!
Unajua nini kazi ni mbaya ukiwa nayo unaona kazi gani hii haifai mshahara mdogo makasiriko kibao n.k lakini unasahau wakati unaiomba hiyo kazi mikono ilikuwa nyuma tena kwa unyenyekevu unaomba uipate hiyo kazi sasa umeizoea kazi unaanza kuidharau ooh mshahara mdogo n.k sasa acha kazi uone kazi kupata kazi
 
Kuna graduate wanalipwa laki na nusu, wamekubali wanazikusanya ili wajipange mtu anaona laki 6 ndogo aanesotea kazi toka 2015 hajapata na ana Masters atasemaje?
Mkuu acha kabisa kuna dr analopwa 450k eti hajapata ajira....hii nchi inahitaji revamping
 
Mkuu game ni tuff kinyama aisee yani hela ya mtaani ni ngumu sana usione wale watumbuliwaji wanaolia na kufa na presha!

Wanajua moto wake ukifulia inakuwaje hapo kwa wife😅
Mkuu, mimi wakati wa kazi ya ulinzi, sometimes ukiwa unatembea zako kuelekea lindoni unakutana na watu wanaoendesha GUTA kabeba bonge la mzigo

Unabaki kujisemea tu, jamani hata hata kama kazi ya ulinzi ni ngumu ila kuna watu wanapata PESA kwa mbinde mnooop🤣🤣🤣
 
Hizo 26m unazirudisha vipi? Huo uwekezaji hauendani na mafanikio
Uko sahihi kabisa.

Na ndio maana mimi huwa nawahurumia watu waliosoma CO private halafu wakaenda MD private. Sioni kama inawalipa.

Maana ada ya CO kwenye vyuo vya private siyo chini ya 2M kwa mwaka, miaka 3 ni sawa na 6M

Ukitoka hapo uende MD private ada siyo chini ya 4M kwa mwaka, miaka 5 ni sawa na 20M.

Maana yake unatumia zaidi ya 26M kusoma.

Na MD ni level ya chini sana, siyo kwamba utakuwa umemaliza.

Na system za serikali ( kama mshahra wako unatoka hazina, ukifikisha miaka 60 tu, system inakutema nje ).

Tatizo wengi wetu tunataka tuajiriwe na serikali, na ajira za serikali kupata siku hizi ni shughuli
Mkuu hata mimi naonelea serikali haina uwezo wq kuwaajiri vijana wote....lakini private nao no wachache na uchache wao kwa upande mmoja ulisababishwa au unasababishwa na our gov
 
Back
Top Bottom