Kuna faida gani za nchi kuruhusu mataifa kuingia bila VISA?

Kuna faida gani za nchi kuruhusu mataifa kuingia bila VISA?

Sio nchini Kenya tu nasema hivi huweza kuzuia watu kuzunguka kwenye ardhi hii hata uweke ukuta wa Trump

Wataingia tu, haya ni yenu tu kusema Wasomali magaidi ila hujui nani anashikilia Uchumi wa Kenya kwa sasa
Tembelea huko uone biashara zao na apartments wanazoshusha mpaka mkikuyu anaomba maji kwao apoze roho

Hapa 🇬🇧 nawaona Wahabeshi kila leo wanaingia na wanapita Tz mnawakamata wanahonga wanakuja huku kama wakimbizi
Nyie mmekalia ooh usalama
 
Mchakato wa kupatikana VISA unaweza kua na mlolongo mrefu mpaka ukaleta dosari.

Mfano. Taratibu za kupata VISA ya Marekani zinaboa sana kama ulikua una plan kwenda vaccation tu unaweza kata tamaa.

Sijajua taratibu za kupata VISA ya kwetu hapa bongo/Kenya
EAC HAKUNA VIZA KWA NCHI WANACHAMA. SO WAKENYA, WAGANDA, CONGO, RWANDA ETC HAWAHITAJI VIZA KUINGIA BONGO
 
Unapoambiwa free visa haimanishi utaingia kiholela bila ukaguzi au kujikalia tu.

Kitakachokosekana ni ile kulipia visa lkn ukaguzi na ufuatiliaji kuwa unafanya nini utafuatiliwa kama kawaida na lazima ueleze utakuwepo kwa muda gani.
Suala la visa free halihusiani na malipo .
Kinachokosekana ni ule mlolongo wa kwenda ubalozini kuomba kupewa visa .
Kuhusu muda ilo lipo wazi kwenye hizi nchi ambapo huombi visa ukiwa nchini kwako kinachofanyika unapofika mpakani anapewa entry permit on arrival ambayo Kwa nchi nyingi onalipiwa na Kwa nchi nyingi unaruhusiwa kukaa kwenye nchi hiyo si zaidi ya siku 90 na ni mpaka uonyeshe uthibitisho wa kuwa Na fedha za kutosha za kujikimu Na sehemu utakayofikia kama ni hoteli uonyeshe reservation document au kama una mwenyeji wako uwe na address take Na namba yake ya Simu ambapo wanaweza kumpigia Simu hapohapo kumuuliza kama kuna mgeni wake anatoka nje .
Mimi ilishanitoke nilikuwa nakwenda Gaborone nikaulizwa namba ya Simu ya mwenyeji wangu nikawapa wakampigia hapohapo mbele yangu wakaongea naye ndio wakanigongea entry permit ya siku 90 ingawaje niliwaambia nakaa wiki moja na niliilipia sio bure
 
Nimeona Rais wa Kenya Ruto amefuta visa entry requirement kwake.

Kuna faida yeyote ya kiuwekezaji?

Je dola 20 au 50 zilikua kikwazo kuingiza watu nchini?

Kwamba kuna wawekezaji serious walishindwa kwenda Kenya kwa kukosa dola 30?

Hii kwangu naiona kama njia ya kukaribisha magaidi nchini Kenya na sio njia au jambo zuri la kuiga Tanzania? ukifanya hivyo, kesho uhamiaji watajaa wasomali maelfu kwa kigezo cha utalii tutaingiza magaidi nchini.
naimani serikali inatambua uwezo wake visa sio kigezo kinaweza kumzuia mhalifu kuingia...tufahamishe kwanini tanzania iige kenya?? unataka kusema serikali ya tanzania haitambui kipi cha kufanya kwa maslahi ya taifa
 
Lugha yako uliyo itumia hapo linakudhihirisha ww ni mtu gani.

Hivi hiyo visa ina saidiaje kudhibiti uharifu kwa nchi kama Tz ambayo kila mwaka watu kutoka nchi jirani wanaingia na kutoka kiholela kupitia mipaka isio rasimi na wengine wanaishi kabisa tena bila kubugudhiwa na mamlaka?

Visa ipo kisheria lakini kusema eti visa ndo ina ifanya Tz kuwa salama ni hoja ya kipumbavu.
Hao magaidi hawana muda na Tz kwa sababu hawana maslahi yeyote ya kutushambulia na pia hatujawahi kuwachokoza.
Basi kusiwe na vitambulisho vyovyote nchini wala kusiwe na mapolisi maana majambazi yapo hata sasa ...viza inasaidia siyo kukamata wahalifu tu hata kuzuia watu kuwa wahalifu . Wewe akili yako ni sawa na kuku ...baba yako aliuza ng'ombe kuku somesha kumbe kauza ng'ombe kusomesha ng'ombe
 
Kwa nchi nyingi Visa ni sehemu ya mapato na wala haihusiani na usalama!
kwa sehemu kubwa ,visa ni sehemu ya vetting ya kiusalama , ili kupunguza uwezekano wa kuleta watu wasio sahihi nchini
nchi ambazo zina special arrangement ya kuto hitaji visa ,kuna mahusiano maalumu ya serikali mbili zinazoshirikana ,
 
Kwamba magaidi kukiwa na visa hawaingii!!!??? Sijui umetafakari kabla ya kuanfika!? Anyway...
kuna faida nyingi kiusalama za kuwa na visa requirements ,
kwanza magaidi kwa nchi makini hutambulika kabla hawajaingia nchi zao, mfano kuna watu wananyimwa visa za marekani kwa kua wanashida za kiusalama ,sasa bila visa restriction watu hao wangeweza kuingia nchi zao bila shida
hatuujui vizuri ugaidi ndio maana hatuelewi
 
hujui ruto ni mpenda sifa na populist?

jamaa ni demagogue to the core

ni professional serial lier!

yaani anadanganya eti "GRAMMY" watafungua studio Kenya za kufanya movie production kiasi kwamba hajui GRAMMY haijihusishi na movie production at all

huyu jamaa na pepo la uongo na populism

na cha ajabu Kenyans hua they believe what this lunatic says
when did Ruto say this? You are the serial liar yourself.
 
Ndo maana nime kuuliza kuwa lini visa ikazuia gaidi?
Kila mwaka maelfu ya raia kutoka nje wanaingia nchini kwa kutumia mipaka isiyo rasimi na wanaishi ndani ya nchi bila vibari vyovyote wakiwemo hao wasomali.

Ukiona hao unao waita magaidi hawaishambulii Tz haimaanishi kuwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu ya visa ,bali ni kwa sababu mashambulizi yao dhidi ya Tz hayana masilahi yeyote kwao na pia Tz hatujawahi kuwachokoza.
umeangalia upande mmoja wa shilingi, watu kuweza kuingia nchini kutumia mipaka isiyo rasmi haihalalishi kuondoa ulazima wa visa . kama umewahi kwenda marekani au UK ,visa zao zina chukua hadi mwezi kuzipata ,tena lazima uoneshe proof ya namna utakavyoishi nchini kwao , kuhalalisha watu kuingia nchini kiholela utakuaja kushtuka hata kazi za kuuza karanga zinafanywa na wachina ,na hutakua umelinda ajira za watu wako.
la pili fikiria kuhusu ujio wa majasusi wa kigeni ambao wengine wanaweza kuja kwa njia halali na wakadhuru watu wetu , kupitia balozi zetu watu hao wakiomba visa , screening ama vetting hufanyika kujua back ground za watu hawa
 
Jao wenye mtazamo huo wa ugaidi hawajielewi.
Tuelewe kwamba Kenya ishashambuliwa Na matukio ya kigaidi kulipo Tanzania kabla ya hapo
Marekani ni nchi ngumu kutoa visa Ila inashambuliwa Na magaidi.
Tanzania na marekani ni nchi mbili tofauti ,maadui wa marekani ni tofauti na maadui wa Tanzania
ilipotokea mashambulizi ya balozi za marekani DSM na Nairobi
fuatilia wahusika walikua watu wa nchi zipi , na nieleze kama huna hata visa restriction how easy itakua kwa watu wa namna hio kuifanya nchi yetu shamba la bibi
 
USA na nchi za magharibi unaomba visa unatoa hela ukinyimwa hela imeenda, hebu fikiria hicho kitega uchumi wamejiwekea hawa jamaa cha kula pesa kiulaini

Watu wangapi wanaoomba na kukataliwa ni kama pata potea katika elfu huenda kumi wakapewa
Labda Ruto ana sababu zake ngoja wakenya waje
Ruto anatafuta publicity ,ana joto la kisiasa kwake , lakini ukweli ni kua kuondoa visa restriction ni kuondoa geti mlangoni
 
naimani serikali inatambua uwezo wake visa sio kigezo kinaweza kumzuia mhalifu kuingia...tufahamishe kwanini tanzania iige kenya?? unataka kusema serikali ya tanzania haitambui kipi cha kufanya kwa maslahi ya taifa
Visa ni first line of defence , ukienda balozi za UK na Marekani kuna maelfu ya watu wanakataliwa kwenda
wengine wana historia za ugaidi nk.
Ukiondoa visa restriction kwa nchi zote nchi yako inaweza kuwa terrorist hub
 
Unajua Europe ni free zone kwa hizo nchi zote. Na uturuki ni let say waarabu Kuna Kazakhstan etc but hatusikii hizo shida why Africa. Hapo Kenya ugaidi upo hata B4 hii free zone. Gaidi akiamua Kuja atafika tu iwe free zone au LA.
mwizi hauzuiwi na geti ,lakini tunaweka mageti ili kupunguza urahisi wa mwizi kukushambulia
 
Back
Top Bottom