Kuna faida gani za nchi kuruhusu mataifa kuingia bila VISA?

Sio nchini Kenya tu nasema hivi huweza kuzuia watu kuzunguka kwenye ardhi hii hata uweke ukuta wa Trump

Wataingia tu, haya ni yenu tu kusema Wasomali magaidi ila hujui nani anashikilia Uchumi wa Kenya kwa sasa
Tembelea huko uone biashara zao na apartments wanazoshusha mpaka mkikuyu anaomba maji kwao apoze roho

Hapa 🇬🇧 nawaona Wahabeshi kila leo wanaingia na wanapita Tz mnawakamata wanahonga wanakuja huku kama wakimbizi
Nyie mmekalia ooh usalama
 
EAC HAKUNA VIZA KWA NCHI WANACHAMA. SO WAKENYA, WAGANDA, CONGO, RWANDA ETC HAWAHITAJI VIZA KUINGIA BONGO
 
gaidi akiomba visa kuna possibility akawa denied
Kuna mtazamo kuwa generation ya sasa inayo / inauwezo mkubwa wa kupata maarifa(knowledge), ila ina shida kubwa sana ya uelewa (comprehension).
 
Unapoambiwa free visa haimanishi utaingia kiholela bila ukaguzi au kujikalia tu.

Kitakachokosekana ni ile kulipia visa lkn ukaguzi na ufuatiliaji kuwa unafanya nini utafuatiliwa kama kawaida na lazima ueleze utakuwepo kwa muda gani.
Suala la visa free halihusiani na malipo .
Kinachokosekana ni ule mlolongo wa kwenda ubalozini kuomba kupewa visa .
Kuhusu muda ilo lipo wazi kwenye hizi nchi ambapo huombi visa ukiwa nchini kwako kinachofanyika unapofika mpakani anapewa entry permit on arrival ambayo Kwa nchi nyingi onalipiwa na Kwa nchi nyingi unaruhusiwa kukaa kwenye nchi hiyo si zaidi ya siku 90 na ni mpaka uonyeshe uthibitisho wa kuwa Na fedha za kutosha za kujikimu Na sehemu utakayofikia kama ni hoteli uonyeshe reservation document au kama una mwenyeji wako uwe na address take Na namba yake ya Simu ambapo wanaweza kumpigia Simu hapohapo kumuuliza kama kuna mgeni wake anatoka nje .
Mimi ilishanitoke nilikuwa nakwenda Gaborone nikaulizwa namba ya Simu ya mwenyeji wangu nikawapa wakampigia hapohapo mbele yangu wakaongea naye ndio wakanigongea entry permit ya siku 90 ingawaje niliwaambia nakaa wiki moja na niliilipia sio bure
 
naimani serikali inatambua uwezo wake visa sio kigezo kinaweza kumzuia mhalifu kuingia...tufahamishe kwanini tanzania iige kenya?? unataka kusema serikali ya tanzania haitambui kipi cha kufanya kwa maslahi ya taifa
 
Basi kusiwe na vitambulisho vyovyote nchini wala kusiwe na mapolisi maana majambazi yapo hata sasa ...viza inasaidia siyo kukamata wahalifu tu hata kuzuia watu kuwa wahalifu . Wewe akili yako ni sawa na kuku ...baba yako aliuza ng'ombe kuku somesha kumbe kauza ng'ombe kusomesha ng'ombe
 
Kwa nchi nyingi Visa ni sehemu ya mapato na wala haihusiani na usalama!
kwa sehemu kubwa ,visa ni sehemu ya vetting ya kiusalama , ili kupunguza uwezekano wa kuleta watu wasio sahihi nchini
nchi ambazo zina special arrangement ya kuto hitaji visa ,kuna mahusiano maalumu ya serikali mbili zinazoshirikana ,
 
Kwamba magaidi kukiwa na visa hawaingii!!!??? Sijui umetafakari kabla ya kuanfika!? Anyway...
kuna faida nyingi kiusalama za kuwa na visa requirements ,
kwanza magaidi kwa nchi makini hutambulika kabla hawajaingia nchi zao, mfano kuna watu wananyimwa visa za marekani kwa kua wanashida za kiusalama ,sasa bila visa restriction watu hao wangeweza kuingia nchi zao bila shida
hatuujui vizuri ugaidi ndio maana hatuelewi
 
when did Ruto say this? You are the serial liar yourself.
 
umeangalia upande mmoja wa shilingi, watu kuweza kuingia nchini kutumia mipaka isiyo rasmi haihalalishi kuondoa ulazima wa visa . kama umewahi kwenda marekani au UK ,visa zao zina chukua hadi mwezi kuzipata ,tena lazima uoneshe proof ya namna utakavyoishi nchini kwao , kuhalalisha watu kuingia nchini kiholela utakuaja kushtuka hata kazi za kuuza karanga zinafanywa na wachina ,na hutakua umelinda ajira za watu wako.
la pili fikiria kuhusu ujio wa majasusi wa kigeni ambao wengine wanaweza kuja kwa njia halali na wakadhuru watu wetu , kupitia balozi zetu watu hao wakiomba visa , screening ama vetting hufanyika kujua back ground za watu hawa
 
Jao wenye mtazamo huo wa ugaidi hawajielewi.
Tuelewe kwamba Kenya ishashambuliwa Na matukio ya kigaidi kulipo Tanzania kabla ya hapo
Marekani ni nchi ngumu kutoa visa Ila inashambuliwa Na magaidi.
Tanzania na marekani ni nchi mbili tofauti ,maadui wa marekani ni tofauti na maadui wa Tanzania
ilipotokea mashambulizi ya balozi za marekani DSM na Nairobi
fuatilia wahusika walikua watu wa nchi zipi , na nieleze kama huna hata visa restriction how easy itakua kwa watu wa namna hio kuifanya nchi yetu shamba la bibi
 
Ruto anatafuta publicity ,ana joto la kisiasa kwake , lakini ukweli ni kua kuondoa visa restriction ni kuondoa geti mlangoni
 
naimani serikali inatambua uwezo wake visa sio kigezo kinaweza kumzuia mhalifu kuingia...tufahamishe kwanini tanzania iige kenya?? unataka kusema serikali ya tanzania haitambui kipi cha kufanya kwa maslahi ya taifa
Visa ni first line of defence , ukienda balozi za UK na Marekani kuna maelfu ya watu wanakataliwa kwenda
wengine wana historia za ugaidi nk.
Ukiondoa visa restriction kwa nchi zote nchi yako inaweza kuwa terrorist hub
 
Unajua Europe ni free zone kwa hizo nchi zote. Na uturuki ni let say waarabu Kuna Kazakhstan etc but hatusikii hizo shida why Africa. Hapo Kenya ugaidi upo hata B4 hii free zone. Gaidi akiamua Kuja atafika tu iwe free zone au LA.
mwizi hauzuiwi na geti ,lakini tunaweka mageti ili kupunguza urahisi wa mwizi kukushambulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…