Kuna hatari kizazi hiki kikaaminishwa kuwa Tundu Lissu ni moja ya Watu wabaya na sio wazalendo kwa Taifa

Kuna hatari kizazi hiki kikaaminishwa kuwa Tundu Lissu ni moja ya Watu wabaya na sio wazalendo kwa Taifa

Mimi si mwana CCM ila sikukubaliana na Lissu kabisa kwenye suala la kuwatetea Acacia kwenye makinikia pamoja na suala la kutetea ushoga.
1. Lakini makinikia yapo ndugu?

2. Lisu hajatetea ushoga, ispokuwa kasimama kama katiba YETU. Lisu amesema atatenda kwa mujibu wakatiba.

Hivi kuheshimu na kufuata katiba nikosa? Au hukuelewa? Au unazusha?
 
Always statements za Lisu ni facts

Ispokuwa wajinga hawamuelewi, I mean ccm.
 
Lissu anashutumu watu watatu kwenye tukio lake Magufuli (hayuko hai), Kipilimba (yupo nche ya nchi) na Makonda (kwa sasa ni raia wa kawaida).

Kitu gani kinachomzuia kurudi Tanzania mpaka aombe kuhakikishiwa usalama wake nani anaetaka kumdhuru; huyo Magufuli karibu baraza lake lote la mawaziri wamemgeuka kiutendaji na maoni. CCM ina watu wengine kabisa.

Kwanini Lissu bado anaogopa kurudi Tanzania ilo ndio swali au anaogopa usalama wa taifa kwa ujumla wao kutokana makosa anayoyajua yeye mwenyewe.

Wajinga bado wengi
Huu uzi unathibitisha ukweli wa madai ya Lisu
 
Always statements za Lisu ni facts

Ispokuwa wajinga hawamuelewi, I mean ccm.
Lissu hamna kitu kabisa kwenye kichwa chake kama alivyo jidhihirisha kwenye suala la 'MIGA'. Bungeni Prof. Kabudi alimwambia nitaleta matokeo yako hapa akakuja mkia na hajawahi kumjibu hadi leo. Si mwanasheria mzuri ila ni mpayukaji mzuri asiyekuwa na maarifa yoyote, ukiangalia rekodi yake ana kesi nyingi za kushindwa kuliko kushinda.
 
Mbona kimeshaaminishwa mkuu!! Soma tu comments za watu humu jamvini utajua kuwa watanzania siyo critical thinkers.
Nikiri kabisa Mimi si muumini wa siasa za upinzani lakini napenda haki na usawa udumishwe. Twende mbele turudi nyuma, hivi Kuna binadamu aliyefanyiwa ukatili kama Tundu Lissu. Naomba tuwe wa kweli jamani, tuwe wa kweli.

1. Kupigwa risasi, wahusika wasitafutwe.

2. Kuzuia fedha ya serikali iliyo stahiki yake asilate matibabu.

3. Kupiga waliokusanyana kumwombea.

4. Kukamata waliotaka kujitolea damu na kuwekwa ndani.

5. Kufutiwa posho zake zote kipindi yupo matibabu.

6. Kunyang'anywa ubunge.

7. Kuzuiliwa gari yake hadi leo isichukuliwe polisi.

8. Kuambiwa ni kibaraka wa mabeberu n.k.

Naomba tuwe wakweli hivi binadamu akifanyiwa haya yote anafanyaje jamani. Huyu mtu amekosa upendo kwa nchi yake. Yaani moyo wake umejeruhuwa sana.

Inahitaji kiongozi mwenye roho ya Mungu amrudishe huyu mtu kwa upendo afutwe machozi bado anaipenda Tanzania mno. Lakini kinyume chake wenye dola wanapiga kwenye mshono. Aiseee nimeamini duniani Ni mahali pabaya sana. Binadamu Ni mnyama mbaya mno Mungu atusaidie.
 
Wajinga bado wengi
Huu uzi unathibitisha ukweli wa madai ya Lisu
Lissu ni mpayukaji hana maarifa yoyote ila nyinyi nyumbu kawaaminisha ni kichwa. Kiboko yake Prof. Kabudi alimwambia bungeni alaleta matokeo yake ya chuo kama ataendelea na jeuri ya upayukaji, Lissu alikaa kimya na hajawahi kumjibu hadi leo.
 
Marehemu jingaman hakutaka mtu mwenye mawazo bora kuliko utopolo wake, alitaka jingamen wenzake ambao kila kitu ni kuitikia ndio!
Kumshabikia marehemu na chama chake cha majambazi kunahitaji kujitoa ufahamu na kujivika uchizi.
Hivi ni nani mwenye utimamu wa akili asiyetambua wizi uliofanywa na awamu ya5?
Utekaji na uuaji wa raia wasio hatia(mathalani Mheshimiwa Lissu aliokolewa na Mungu).
Uporaji wa fedha za wafanyabiashara,
Propaganda za kumsifia jingaman zilienda hadi kuanzishwa kwa somo jipya la kumsifia na kumtukuza kama muasisi wa mageuzi ya kiuchumi Tanzania na topics kadhaa za kuwasemea vibaya wapinzani wake.

Pamoja na kwamba huyu muharibifu hayupo lakini ameacha waharibifu waliorithi nyendo zake, yafaa kuwaondoa kabisa kwenye uso wa siasa
Nimependa "Jingaman".
 
Nikiri kabisa Mimi si muumini wa siasa za upinzani lakini napenda haki na usawa udumishwe. Twende mbele turudi nyuma, hivi Kuna binadamu aliyefanyiwa ukatili kama Tundu Lissu. Naomba tuwe wa kweli jamani, tuwe wa kweli.

1. Kupigwa risasi, wahusika wasitafutwe.

2. Kuzuia fedha ya serikali iliyo stahiki yake asilate matibabu.

3. Kupiga waliokusanyana kumwombea.

4. Kukamata waliotaka kujitolea damu na kuwekwa ndani.

5. Kufutiwa posho zake zote kipindi yupo matibabu.

6. Kunyang'anywa ubunge.

7. Kuzuiliwa gari yake hadi leo isichukuliwe polisi.

8. Kuambiwa ni kibaraka wa mabeberu n.k.

Naomba tuwe wakweli hivi binadamu akifanyiwa haya yote anafanyaje jamani. Huyu mtu amekosa upendo kwa nchi yake. Yaani moyo wake umejeruhuwa sana.

Inahitaji kiongozi mwenye roho ya Mungu amrudishe huyu mtu kwa upendo afutwe machozi bado anaipenda Tanzania mno. Lakini kinyume chake wenye dola wanapiga kwenye mshono. Aiseee nimeamini duniani Ni mahali pabaya sana. Binadamu Ni mnyama mbaya mno Mungu atusaidie.
Wenye roho ya shetani pekee ndio wamemfanyia ubaya,na kumsemea ubaya,na wale bendera fuata upepo wanaoamini katika roho mbaya, kutofuata wala kupenda kuona haki ikitendeka.
 
Watu wajinga ndio wataweza kudanganywa.
Mzarendo gani,huyu aliyekuwa anakaa upande wa mabeberu kutishia serikali kuwa tutashitakiwa miga,mala tutanyorewa na vipande vya chupa pasipo maji, mzarendo gani anayeweza kukaa upande wa maadui wa taifa.Lissu ni kibaraka tu.
 
IMG_20210715_093732.jpg

Mtanzania wa Aina yake mwenye upendo na nchi yake na ni mzalendo haswa, Ila ukiwa kibaka wa Taifa huwezi mwelewa huyu jamaa
 
Always statements za Lisu ni facts

Ispokuwa wajinga hawamuelewi, I mean ccm.
Wewe nawe hujitambui. Rekodi ya Lissu kwenye kesi ni ushahidi tosha ni mpayukaji hana maarifa yoyote, ana kesi nyingi za kushindwa kuliko kushinda, wakati mwenzake Kibatala ana kesi nyingi za kushinda kuliko kushindwa.
 
Wewe nawe hujitambui. Rekodi ya Lissu kwenye kesi ni ushahidi tosha ni mpayukaji hana maarifa yoyote, ana kesi nyingi za kushindwa kuliko kushinda, wakati mwenzake Kibatala ana kesi nyingi za kushinda kuliko kushindwa.
Wenye roho mbaya mkimwona najua dhamira zinawasuta,ila hapa najua hamwezi kusema.
 
Mbona kimeshaaminishwa mkuu!! Soma tu comments za watu humu jamvini utajua kuwa watanzania siyo critical thinkers.
Ila bado naimani na Rais Samia, wakati fulani ukifanikiwa kumrejesha mtu kama huyu kwenye hali yake unakuwa umeponya mioyo ya Watu wengi Sana kwa maramoja. Mama bila kujali makosa ya mwana wa Tanzania huyu tafadhali mrejeshe kwenye hali yake nimegundua Kuna space kwenye ubongo wa Lissu inahitaji upendo wa nchi yake kabisa na si kwa mwingine ikitoka kwa Rais itakuwa dawa na mwanzo mpya kwa Tanzania yenye matumaini.....huyu mtu kakosa upendo wa nyumbani jamani.
 
Ukweli ni kwamba Tanzania watu wenye Akili, weledi na misimamo thabiti hupigwa vita na wajinga wengi waliomo CCM
Hilo la Lissu kuonewa watu wanalijua sana tatizo ni wale wasiopenda kukosolewa watakupiga teke hata ukiwaambia shati lako kanyea kunguru, wataenda hivohivo wakikutukana badala ya kulifuta.
 
Kizazi cha sasa taarifa zinatafutwa/zinapatikana kwa njia nyingi tofauti tofauti. Watu hawawezi kusikiliza propaganda za mashetani/ccm wakaziamini.

Na hivi wameanza kupoteana huyu Mungu aliye mkuu kuliko ufalme mwingine wowote, aliymponya mja wake, kuna siku atawaaibisha waliotenda uovu ule. Walaaniwe wao na kizazi chao.
Hatasalia hata mwovu mmoja bila kuumbuka
 
Watu awaamki asubuhi moja na kuambizana tu jamani enhe twendeni tukamtwange Gaddafi, Saddam, tuiwekee vikwazo Venezeula, etc; bila ya kujiridhisha matendo yao yatakuwa na asilimia kubwa ya public support ndani ya nchi husika na viongozi wa nchi jirani.

Sasa unapokwenda kuchukua kampuni iliyosajiliwa uingereza halafu it’s parent company ipo Canada, it’s board members are the sort of people raisi wa marekani anaweza wateua kushika nafasi sentive mpaka kesho including secretariat post; sio kwa sababu ya kufanya kazi Barrick la hasha ni kwa sababu washashika nafasi sensitive ndani ya serikali ya marekani kabla ya kwenda private kwa hiari na wanajua kutoa pressure serikali yao iingilie kati mambo yao.

Unadhani watu kama hao ukichukua kampuni yao wakitaka kukuadhibu wataingia tu mahakamani au watatoa pressure serikali yao ifanye jambo bila ya kujua ndani ya Tanzania wana public support kwanza; maana ni kweli mkataba wao ni wa kinyonyaji kwa muda mrefu sana.

Hiyo ndio ilikuwa kazi ya Lissu from the outset kuonyesha matendo ya serikali yana makosa kuwatengezea ACCACIA public support ata huko kwao wangeamua kuchukua hatua za kujibu mashambulizi wana baraka za watanzania kadhaa.

Na Lissu alishaanza kuwabeba wafuasi wa CDM na upinzani kwa wingi kwa kuuamisha umma mabeberu yangechukua hatua; wakulaumiwa ni Magufuli. Kila akiombwa Lissu acha hiyo michezo hasikii zaidi ya kujitapa tu mimi nilikuwa sijui huku na kule kutetea wananchi kabla yenu etc with his narcissistic comments.

Ni hivi ili jambo you ppl are beating round the bush, kulimaliza Lissu aende polisi; akifika huko akitoa ushirikiano wanaoutaka. Polisi wasipofanya kitu anaweza kuwa na hoja.

As yet anatuachia maswali kwanini ataki kwenda polisi ni kitu gani hasa kinachomfanya kuogopa kuitikia wito.

..Magufuli alikuwa akifanya vituko vingi sana na usipokuwa makini unaweza kutekwa akili zako.

..Chukulia hoja yake kwamba kuna "msaliti" anatuma txt kuomba data. Halafu akaendelea kudai mawasiliano kati ya "msaliti" na DEO MWANYIKA yamedakwa!!

..Halafu anaendelea kusema "msaliti" hatakiwi ku-survive, anatakiwa auwawe kama inavyofanyika kwa askari waliokengeuka wakiwa mstari wa mbele.

..Kwanza niulize hivi tume ya uchunguzi haikutafuta data toka kwa Accacia / Barrick wakati wakiandaa ripoti yao?

..Wakati wa majadiliano hakukuwa na ubadilishanaji wa data kati ya timu ya serikali na timu ya Accacia / Barrick?

..Sasa kwa akili za Magufuli huyu "msaliti" anastahili kuuwawa, lakini Deo Mwanyika mtumishi wa Accacia / Barrick anastahili kuishi, na kupitishwa kuwa mgombea ubunge wa CCM!!

..Je, wanaosema Magufuli ana faili Mirembe wanakosea?

..Jambo lingine ni suala la kuwafungia watendaji wa serikali waliokuwa wajumbe kwenye tume yetu ya majadiliano na Accacia / Barrick.

..Majadiliano yale yalifanyika kwa MIAKA MITATU mpaka kufikia conclusion. Je, Magufuli alikuwa kawafungia wajumbe wa tume muda wote huo?

..Tatizo ni kwamba Magufuli alikuwa anasema mambo ya UONGO ambayo hayapaswi kusemwa na kiongozi anayeheshimu wananchi wake.

..Ni bahati mbaya kwamba wale waliojenga ujasiri kumrudisha Magufuli kwenye mstari ndio hao mnaowaita wasaliti, na kuunga mkono wauwawe kinyama.

NB:

..Magufuli hakukamata kampuni yoyote ya mabeberu. Tayari alishanywea baada ya kukutana CEO wa Barrick.

..Na kama Barrick ni kampuni ya kibeberu ambayo ni hatari kwa usalama wetu, tujiulize aliyeileta hapa Tanzania ni nani kama sio CCM ya Magufuli na washirika wake?
 
Back
Top Bottom