Watu awaamki asubuhi moja na kuambizana tu jamani enhe twendeni tukamtwange Gaddafi, Saddam, tuiwekee vikwazo Venezeula, etc; bila ya kujiridhisha matendo yao yatakuwa na asilimia kubwa ya public support ndani ya nchi husika na viongozi wa nchi jirani.
Sasa unapokwenda kuchukua kampuni iliyosajiliwa uingereza halafu it’s parent company ipo Canada, it’s board members are the sort of people raisi wa marekani anaweza wateua kushika nafasi sentive mpaka kesho including secretariat post; sio kwa sababu ya kufanya kazi Barrick la hasha ni kwa sababu washashika nafasi sensitive ndani ya serikali ya marekani kabla ya kwenda private kwa hiari na wanajua kutoa pressure serikali yao iingilie kati mambo yao.
Unadhani watu kama hao ukichukua kampuni yao wakitaka kukuadhibu wataingia tu mahakamani au watatoa pressure serikali yao ifanye jambo bila ya kujua ndani ya Tanzania wana public support kwanza; maana ni kweli mkataba wao ni wa kinyonyaji kwa muda mrefu sana.
Hiyo ndio ilikuwa kazi ya Lissu from the outset kuonyesha matendo ya serikali yana makosa kuwatengezea ACCACIA public support ata huko kwao wangeamua kuchukua hatua za kujibu mashambulizi wana baraka za watanzania kadhaa.
Na Lissu alishaanza kuwabeba wafuasi wa CDM na upinzani kwa wingi kwa kuuamisha umma mabeberu yangechukua hatua; wakulaumiwa ni Magufuli. Kila akiombwa Lissu acha hiyo michezo hasikii zaidi ya kujitapa tu mimi nilikuwa sijui huku na kule kutetea wananchi kabla yenu etc with his narcissistic comments.
Ni hivi ili jambo you ppl are beating round the bush, kulimaliza Lissu aende polisi; akifika huko akitoa ushirikiano wanaoutaka. Polisi wasipofanya kitu anaweza kuwa na hoja.
As yet anatuachia maswali kwanini ataki kwenda polisi ni kitu gani hasa kinachomfanya kuogopa kuitikia wito.
..Magufuli alikuwa akifanya vituko vingi sana na usipokuwa makini unaweza kutekwa akili zako.
..Chukulia hoja yake kwamba kuna "msaliti" anatuma txt kuomba data. Halafu akaendelea kudai mawasiliano kati ya "msaliti" na DEO MWANYIKA yamedakwa!!
..Halafu anaendelea kusema "msaliti" hatakiwi ku-survive, anatakiwa auwawe kama inavyofanyika kwa askari waliokengeuka wakiwa mstari wa mbele.
..Kwanza niulize hivi tume ya uchunguzi haikutafuta data toka kwa Accacia / Barrick wakati wakiandaa ripoti yao?
..Wakati wa majadiliano hakukuwa na ubadilishanaji wa data kati ya timu ya serikali na timu ya Accacia / Barrick?
..Sasa kwa akili za Magufuli huyu "msaliti" anastahili kuuwawa, lakini Deo Mwanyika mtumishi wa Accacia / Barrick anastahili kuishi, na kupitishwa kuwa mgombea ubunge wa CCM!!
..Je, wanaosema Magufuli ana faili Mirembe wanakosea?
..Jambo lingine ni suala la kuwafungia watendaji wa serikali waliokuwa wajumbe kwenye tume yetu ya majadiliano na Accacia / Barrick.
..Majadiliano yale yalifanyika kwa MIAKA MITATU mpaka kufikia conclusion. Je, Magufuli alikuwa kawafungia wajumbe wa tume muda wote huo?
..Tatizo ni kwamba Magufuli alikuwa anasema mambo ya UONGO ambayo hayapaswi kusemwa na kiongozi anayeheshimu wananchi wake.
..Ni bahati mbaya kwamba wale waliojenga ujasiri kumrudisha Magufuli kwenye mstari ndio hao mnaowaita wasaliti, na kuunga mkono wauwawe kinyama.
NB:
..Magufuli hakukamata kampuni yoyote ya mabeberu. Tayari alishanywea baada ya kukutana CEO wa Barrick.
..Na kama Barrick ni kampuni ya kibeberu ambayo ni hatari kwa usalama wetu, tujiulize aliyeileta hapa Tanzania ni nani kama sio CCM ya Magufuli na washirika wake?