ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Hii ni hoja yangu tu si lazima kila mtu akubaliane nayo.naamini kuna dalili ambazo zinaweza kuonyesha moyo wa mtu unavutwa zaidi kumtafuta Mungu.
Ya kwanza ni pale unapokuwa peke yako hasa usiku. Unaweza ukawa unatembea au ukaamka ghafla bila hata kukusudia ukautazama mwezi bila sababu ukaanza kutafakari ukuu wa Mungu na jinsi ulimwengu ulivyo mkubwa. Kila nikipata hali hiyo nahisi kuna kitu kinavuta moyo wangu zaidi kumfikiria Muumba.
Ya pili ni kupenda sana kuangalia documentaries au video za wanyama, ndege Kadiri ninavyoziona ndivyo ninavyozidi kushangaa hekima ya uumbaji. Mara nyingi naishia kusema haya hayawezi kuwa tu yametokea bila mpangilio nadharia nyingine zote zinakosa nguvu naona kabisa hazipatani na akili.Mungu anamuita kila mtu kwa njia tofauti, ila hizi ni dalili mbili ambazo mimi nimekuwa nikiziona mara kwa mara.wewe je dalili gani au ishara gani hukufanya umfikirie MUngu at least dakika 3..