Kuna kiashiria chochote cha tabia kwa mtoto anayenyonya kidole?

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Ndo hivyo wakuu, naomba nisaidiwe hilo!. Najua kuna wataalamu na wazoefu wa kung'amua tabia humu.
Mtoto ni wa kike, still todler (2+ yrs).

Mtoto huyu halali kama hajanyonya kidole chake gumba cha mkono wa kushoto huku mkono wa kulia akiutumia kumfinyafinya mama yake (au yeyote aliyemshika). Na sehemu anayopenda kumfinya aliyemshika ni kwenye kiwiko cha mkono.

Ukimtoa kidole hiko halali na lazime akupigie kelele za kilio. Huhakikisha analala nacho na muda pekee wa kuweza kumtoa ni wakati wa amelala fofofo!


 
Haina shida mkuu. Hiyo inaitwa sucking reflex ambayo ni hali inayoanzia tokea mtoto akiwa tumboni, huanza kuanzia mwezi wa tatu wa ujauzito.

Wataalamu wanasema hali hiyo hujijenga ili mtoto atakapozaliwa aweze kunyonya. Ndio maana ukiona viumbe hai wengi hawafundishwi kunyonya auto tu akiipata chuchu anafanya yake.

So wanasema kitu chochote kikigusa (hard palate) sehemu ngumu juu ndani ya mdomo hiyo suck reflex inatokea ana anajikuta ananyonya.

Hiyo hali inaweza kuendelea kwa mtoto mpaka miaka kadhaa hata baada ya kuacha kunyonya.

I stand to be corrected.
 
Hakuna shida hiyo ni tabia ambayo iko kwenye kizalia cha ukoo/familia.. In fact mtoto anayenyonya kidole sio msumbufu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Exactly,
 
Mdogo wangu anakaribia 18 yrs na bado ananyonya vidole
Tulipaka upupu, shubiri sijui alovera, pilipili tulifunga hadi plaster lakini hakuacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…