Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilikuaje hadi akafikia hatua hiyo?Ndo hivyo wakuu, naomba nisaidiwe hilo!. Najua kuna wataalamu na wazoefu wa kung'amua tabia humu.
Mtoto ni wa kike, still todler (2+ yrs). Mtoto huyu halali kama hayanyonya kidole chake gumba cha mkono wa kushoto huku mkono wa kulia akiutumia kumfinyafinya mama yake (au yeyote aliyemshika). Na sehemu anayopenda kumfinya aliyemshika ni kwny kiwiko cha mkono.
Ukimtoa kidole hiko halali na lazime akupigie kelele za kilio. Huhakikisha analala nacho na muda pekee wa kuweza kumtoa ni wakati wa amelala fofofo!
Jaribu kuonyesha japo chembe ya ustarabuHao ndo wanakuja kuwa wanyonyaji vikojoleo
Ni jambo ambalo linanifikirisha sana masan hata first born wake yupo chuo lkn ananyonya kidole mpaka muda anajisahau kabisa, inasemekana hata mimi nilikuwa na tatizo hilo Ila fimbo na pili pili zilitumika haswa.
Nilijifunza chuoni hii kwenye saikolojia. Hiyo nguvu ya kunyonya huzaliwa nayo viumbe vyote vinavyonyonya. Ndiyo maana mbuzi, ng'ombe na nguruwe vikizaliwa tu hakuna mwalimu wa kumfundisha kunyonya. Wanyama pori ni zaidi huanza kunyonya ndani ya dakika 5 baada ya kuzaliwa. Nguvu hii huitwa libido energy au conscious activity kama sijasahau mana nimesoma zamani. Ni sawa na hamu ya kufanya mapenz Kwa wanyama huzaliwa nayo na hawafundishwi, paka, njiwa, kuku, huyo mtoto muda ukifika ataacha na akikua ataanza kufanya mapenz bila kuingia darasani kufundishwa. Mungu katuumba hivyo.Haina shida mkuu. Hiyo inaitwa sucking reflex ambayo ni hali inayoanzia tokea mtoto akiwa tumboni, huanza kuanzia mwezi wa tatu wa ujauzito.
Wataalamu wanasema hali hiyo hujijenga ili mtoto atakapozaliwa aweze kunyonya. Ndio maana ukiona viumbe hai wengi hawafundishwi kunyonya auto tu akiipata chuchu anafanya yake.
So wanasema kitu chochote kikigusa (hard palate) sehemu ngumu juu ndani ya mdogo hiyo suck reflex inatokea ana anajikuta ananyonya.
Hiyo hali inaweza kuendelea kwa mtoto mpaka miaka kadhaa hata baada ya kuacha kunyonya.
I stand to be corrected.
Umeelewa lakini?!!!WATOTO WA kileo wanalelewa kimayai sana.
ENZI zetu kidole kinapakwa pilipili siku mbili tu anaacha kunyonya.
KUPANGA ni kuchagua
Ahsante sana kiongozi!!Haina shida mkuu. Hiyo inaitwa sucking reflex ambayo ni hali inayoanzia tokea mtoto akiwa tumboni, huanza kuanzia mwezi wa tatu wa ujauzito.
Wataalamu wanasema hali hiyo hujijenga ili mtoto atakapozaliwa aweze kunyonya. Ndio maana ukiona viumbe hai wengi hawafundishwi kunyonya auto tu akiipata chuchu anafanya yake.
So wanasema kitu chochote kikigusa (hard palate) sehemu ngumu juu ndani ya mdogo hiyo suck reflex inatokea ana anajikuta ananyonya.
Hiyo hali inaweza kuendelea kwa mtoto mpaka miaka kadhaa hata baada ya kuacha kunyonya.
I stand to be corrected.
Ahsante sana mkuu Mshana!Hakuna shida hiyo ni tabia ambayo iko kwenye kizalia cha ukoo/familia.. In fact mtoto anayenyonya kidole sio msumbufu
Sent using Jamii Forums mobile app
🙏🙏Muache afikishe miaka 4 hivi,akiendelea na hiyo tabia!! Paka upupu kwenye kidole..
🙏🙏Kama ana miaka miwili ✅, miaka miwili mingine ikiongezeka tabia ikawa ni hiyo hiyo mounye kwa ukali
Dah, bro vp tena huyo?!!!🤣🤣🤣Hili jambo kuna muda nahisi kama ni ugonjwa, Bro wangu Ana miaka zaidi ya 40 lkn kuna muda anajisahau ananyonya kidole hasa akiwa peke yake.
Vp mkuu?!!
AhsanteHaina shida, akiongezeka miaka unaweza kumkataza polepole ataacha