Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili huenda mwiko unaenda kuvunjika

Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili huenda mwiko unaenda kuvunjika

neno huru kwako lina maan a tofauti na maana halisi ya watu kuwa huru. Kwetu tuna umeme tangu mwaka juzi, lakini wewe unaongea umeme wa leo. Mpaka sasa hivi kuna vijana wana ajira za "fundi umeme" ambao wanatandika waya za umeme kwenye nyumba kwa malipo laki moja na nusu hadi laki mbili pamoja na gharama za vifaa. Wewe endelea kulala na kuota tu, wengine wameshaamka wako kazini sasa.

Mwaka jana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ndugu zako walichagua viongozi au walilazimishiwa viongozi na CCM kama vijiji vingine vyote nchini vilivyofanyiwa?
Bila dhulma, uonevu na kupora chaguzi CCM ishakataliwa nchini
 
nyie kaeni mnatiana ujinga,baada ya matokeo jiandaeni kuingia barabarani,nahisi hilo ndio la msingi kwenu kama mgombea wenu anavyowaasa.
 
Kijiji gani mkuu??acha kujifariji.huu ndo upinzani Original.ccm oyee
Mimi mwaka 2010 niliitangaza sana CHADEMA kijijini kwangu kwani nilichukua likizo kwenda kuhamasisha uchaguzi na kweli wananchi walikuwa na mwamko sana wakati huo. Wakati ule tulitoka kama 45% CHADEMA Vs 55% CCM. Lakini leo hii ni 100% CCM tu. Na sababu zake ni wazi kabisa.
 
Kwetu ni pazuri sana huenda kuliko kwenu; wako vizuri sana kibiashara, hawategemei pesa za mkato mkato ambazo ndizo zinazoliliwa na watu wengi hapa. Umewahi kuona watu wanaofanya biashara za kihalali wakililamika? Hii ya kupungua hela kwenye mzunguko ni jambo la muhimu sana kuimarisha uchumi. Mkapa aliimarisha sana mzunguko wakati wake lakini yaliyofuata ndiyo tunayokumbuka leo; kuna wakati inflation ilikuwa inapanda. Sasa hivi inflation imekuwa controlled tena kama alivyoacha Mkapa.

Sijui kama unajua kusoma graph!


View attachment 1574815

Sijui kama bado unaikumbuka picha hii pamoja na vikatuni vilivyofuatia

View attachment 1574817

Asante sana Kichuguu ukweli siku zote unathibitika! Asomae bila hila ataelewa tuu
 
Mimi mwaka 2010 niliitangaza sana CHADEMA kijijini kwangu kwani nilichukua likizo kwenda kuhamasisha uchaguzi na kweli wananchi walikuwa na mwamko sana wakati huo. Wakati ule tulitoka kama 45% CHADEMA Vs 55% CCM. Lakini leo hii ni 100% CCM tu. Na sababu zake ni wazi kabisa.

Nna uhakika wale wote uliowahamasisha 2010 uko nao ulipo na wana vikatio vilivyohakikiwa😃😃✔✔✔👍

Maana kuna ndugu zetu baada ya kupoteza 2010 walisema hawatapiga kura tena, hata vikatio hawana ila kwenye mikutano hawakosi😂😂😂
 
Kwa uelewa huu Tanzania tuna safari ndefu sana kuufuta ujinga. Hata mfano wa Maalim Seif umeusahau...tangu 2015 hadi leo hakuwahi kuwa raisi.
Unaelewa maana ya maajabu?
Hayo hufanywa na Mungu
Hukusikia Zimbabwe?
Mpk leo watu hamuamini lakini imeshatokea
HAYO NDIYO MAAJABU
 
Mbowe kaona Lissu anachangamsha genge tuu hawezi kushinda urais kaamua kuachana nae. Huyo atakuwa rais wa miga.
Pamoja na kumtoa dada kafara, maji yanazidi unga. Sijui nani atatolewa kafara kwenye ukoo kuikosoa hili jahazi.
 
Wasalam,

Pamoja na mazuri yote aliyofanya Mh magufuli bado wingu jeusi limetanda ndani ya ccm kutokana na uasi wa baadhi ya wanaccm.
Kuna kila dalili kwamba ccm inaenda kushindwa kwa fedhea ktk uchaguzi wa Oct 28.

Dalili moja mbaya ni kwamba wananchi ambao ni wapiga kura wamekata tamaa kutokana na ugumu wa Maisha na wengi wameapa kuikataa ccm Oct 28, huenda Tanzania ikaandika historian kwa Rais kuongoza kipindi kimoja cha miaka5.

Dalili zinaonesha Watanzania hawana imani na CCM pamoja na rais magufuli.

Maendeleo yana vyama.
Si kweli. Leta ushahidi
 
Mwaka huu Mzimu wa Lissu hautawaacha salama.
Lissu anatimiza wajibu wake kama RAIA mwema wa Tanzania, anakemea maovu na kutetea Uhuru wetu,Haki zetu ili tupate Maendeleo endelevu badala ya hata ya maboksi tunayoletewa na watesi wetu tupende tusipende.CCM Mpya ni shiiida!Tukiwaambia hatutaki ndege kwa sasa ndiyo wanaagiza zingine hadi tukome.
Watanzania wenzangu,Tusikubali Kudhulumiwa Kura zetu,Tuchague Viongozi na siyo Watawala.
 
Kwa uelewa huu Tanzania tuna safari ndefu sana kuufuta ujinga. Hata mfano wa Maalim Seif umeusahau...tangu 2015 hadi leo hakuwahi kuwa raisi.
Historia uvunjwa na historia mkuu.
 
Watakataje tamaa wakati kuna madege, mameli, mabwawa, mabarabara, madaraja, mareli na makodi mengi mengi...??
Hao wananchi hawaoni nchi ipo uchumi wa kati?
Mku hata Ethiopia hayo yote yapo lakini Waithiopia wanaikimbia Nchi yao kila siku.Ccm tulikosea sana kuwekeza kwenye vitu badala kuwapa Raia kile kinachohitajika kwa wakati na mahali husika pia makundi kwenye chama ni mengi hasa wale waliodharauliwa na viongozi huku nao wakiwa ni viongozi pia kwenye mashina na kata na wilaya haya yote ni shida kwa chama

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom