Kuna lile jina halina maana mbaya ila hupendi mtu akuite. Litaje

Kuna lile jina halina maana mbaya ila hupendi mtu akuite. Litaje

Madam - toka msichana mdogo mpaka mama mtu mzima huwa inatokea randomly watu wananiita hivi. Sipendi, naona nazeeshwa 😩!
Hapo sindo wamekuheshimisha sasa, maana Madam imekaa (mwanamke aliyepevuka kiakili na kifikra, anayejiweza kimaisha, muonekano mzuri na mwenye kipato chake au kazi nzuri) ndo maana inaanziaga shuleni😄
 
Mtu ananiita mamtu!!!

Wanaume wanatongoza, wakichoka wanajifriend zone, wakichoka wanaanza upya mtongozo wakichoka wanajitoa 😄

Kwa shishi ni mtaani kwangu, mtu akiwa around ananiinvaiti tu, haihusiani na mahusiano.
Ktk vitu sinaga uvumilivu navyo basi ni kumtongoza mwanamke muda mrefu, mimi ninazo siku zangu 3 tu, za kuanzia kutongoza hadi kupata jibu. Zikivuka hizo na sijapata jibu lakueleweka basi najua kuwa nishatemwa. So, kama mwanamke atasema anizungushe ili ajue kama nipo serious basi mimi mtihani huo nafeli mapeema kabisa, kumbe mimi ndo mtu sahihi kwake ila mtihani wake atakuwa katoa nje ya syllabus😄
 
Habari wadau;;

Kila mmoja ana kile akipendacho na asichokipenda.
Siku hizi kumekuwa kunaibuka misemo na majina mbalimbali ktk jamii na yamekuwa yakitumika/kutumiwa.
Kuna baadhi ya majina kama udugu wangu, na mengineyo...

Sasa kuna jina ambalo mtu aweza kukuita ila ukajikuta tuu hupendi ijapokuwa halina tafsiri mbaya wala maana mbaya ila hupendi tuu, na ukiulizwa sababu waeza ukawa huna lakini hulipendi tuu.

Binafsi, sipendi mtu aniite MKUU.

Ile, sawa MKUU, Hakuna shida MKUU, habari yako MKUU.
Oyaa yaan hiyo inaniboaga kinyama, ila sijawah kuwakataza wanaoniita hvyo lakin wangejua tuu wangeacha.

Vipi kwa upande wako Mdau...
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom