Kuna mahali karoti moja inauzwa shillingi mia tatu Tanzania hii!

Dar es Salaam na sehemu nyingine za miji sasa hivi karoti moja inauzwa shillingi mia tatu, wakulima wenye akili wangeachana na kulima mahindi na mihogo badala yake walime karoti wapige pesa za haraka haraka za maana.
 
Shilling mia moja.
Huku kwetu uswazi gengeni ukitoa 2,000/- unapata nyanya 5pcs,vitunguu 5pcs,hoho 5pcs,karoti 5,pilipili mbuzi 2! Kuna mtu nilikuwa nae akauliza huyu anapata faida kweli? Nikamjibu na hapo katupiga sisi kaonq maboss. Kifupi bei za bidhaa zinategemea location. Bei ya Masaki sio sawa na Mbagala.
 
Mbagala mnauziwa mabaki baada ya vilivyo Bora kuchukuliwa, zile nyanya na karoti tepetepe ndembendembe zimejaa makovu haswa.
 
Hii nchi tulishaambiwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Huo ni urefu wa kamba ya mlima karoti, Acha nao wale kwa urefu wa kamba yao.
 
Ni wakati wa mkulima kuchangamkia zao la karoti.
 
Sahihi, bei ziategemea location!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…