Kuna mambo nilikuwa nafanya wakati wa ujana yananitesa

Kuna mambo nilikuwa nafanya wakati wa ujana yananitesa

Mkuu kinyeo kipi chako au? Mbona wabongo mna roho chafu hivyo….behave
Pole sana Godwin peter . Japo sijajua tatizo lako ni nini lakini naweza ku-feel jinsi unavyojisikia kwa majibu unayopata hapa. Ni hivi: Nadhani maisha ya umaskini tunayozaliwa nayo na kukulia yanatufanya watanzania wengi kukosa empathy na kujikuta tuna-behave kama wanyama. Nimesoma post yako ya leo na hiyo ya zamani, lakini sijaona jambo lolote baya la kufanya wengi waandike kashfa namna hii. Usijali sana kwani kama nilivyosema watanzania wengi tuna roho mbaya na ubinafsi na mbaya zaidi hatutumii hata walau dakika moja kutafakari jambo. Huwezi kukutana na mtu kama dr ukaongea naye? Utafute dr ambaye anaaminika na siyo hawa wa uchochoroni. Sehemu kama Agakhan ni nzuri kama una uwezo. Vinginevyo utafute mtu mwenye busara na upendo umweleze tatizo lako. Njia nyingine nzuri ni kutafuta forum za kimataifa (tumia Google)zenye kutoa advice kuhusu mambo mbali mbali ya kiafya. Huko unaweza kukutana na watu wenye huruma na upendo na siyo kaka sisi wabongo. Pia kuna madaktari wengi wa kuaminika wenye Blogs, na husaidia watu kwa ushauri. Unaelezea tatizo lako, na jinsi unavyokutana na kebehi na matusi unapojaribu kutumia local expertisees.
 
Habarini za humu wadau,mimi ni kijana naishi hapa jijini Dar, nina kazi na ninaishi katika harakati zangu za kila siku.

Sasa kuna mambo ya ujana nilikuwa nafanya sasa hivi yananifikirisha sana, ninawaza sana sina amani nakuwa mnyonge pia
Ni kwasababu haujaeleza ni mambo gani. lakini yawezekana ni makubwa sana ndio maana hujaweza hata kuyaanika. Napenda nikueleze kwamba, lipo tumaini katika kila jambo linalokusumbua, tumaini letu ni kwa Yesu, yeye alimwaga damu, alilipa garama ya mambo yooote yanayotusumbua. Isaya 53 inaeleza, pamoja na mambo mengine kwamba, alidharauliwa mno (akawa amebeba dharau ili wale wamwendeao wasidharauliwe), alikuwa na huzuni na masikitiko (ili kuyabeba masikitiko na huzuni za wale watakaomwendea), aliteswa na kuumia mno kimwili na kiroho kwa ajili yetu, yote aliyafanya au alifanyiwa kama kafara la ukombozi wetu. tumekombolewa kutoka kwenye huzuni, masikitiko, na mateso ya kila namna, Yesu Kristo aliyabeba.

Mathayo 11:28 - 30 inasema, Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.

Hapa duniani, unaweza kupitia maisha yanye majonzi, dukuduku, au kitu chochote kikausumbua sana moyo wako, Yesu anasema, tumtwishe yeye fadhaa zetu zote, maana yeye anajishughulisha sana na mambo yetu. Unachotakiwa hapo ni KUOKOKA TU, kabidhi maisha yako yote kwa Yesu, yeye atayabema hayo masumbufu yeyote uliyo nayo, ameahidi kufanya hivyo na atafanay kwasababu hajawahi kudanganya na hatakuja kudanganya. watu wengi huwa tunakuwa wabishi, hatupendi kuokoka, tunaona kama kuokoka ni ushamba, tunaona kama ni umasikini, ajabu yake, hiyo ndio njia pekee ya kweli na uzima na ya kukuweka huru. wale waliogundua na kuifuata, wanajua kuwa wamepoteza muda mwingi kwa maisha mengine.

Nilishawahi kuwa na mizigo ya umasikini, magonjwa makubwa yanayotisha, nilimtwisha yeye fadhaa zangu zote, kwa maana yeye huwa anajishughulisha sana na mambo yetu (yetu akina nani? wale waliokabidhi maisha kwake, sio watu wote dunaini hata wale wasiomwamini au wale wanaoshinda kwa waganga na wanaokataa wokovu wake, hiyo "yetu" inamaanisha wale waliokabidhi maisha kwake, ukikabidhi maisha kwa Yesu atajishughulisha na mambo yako na utakuwa ushuhuda).
 
Dogo umezingua
Habarini za humu wadau,mimi ni kijana naishi hapa jijini Dar, nina kazi na ninaishi katika harakati zangu za kila siku.

Sasa kuna mambo ya ujana nilikuwa nafanya sasa hivi yananifikirisha sana, ninawaza sana sina amani nakuwa mnyonge p
 
Habarini za humu wadau,mimi ni kijana naishi hapa jijini Dar, nina kazi na ninaishi katika harakati zangu za kila siku.

Sasa kuna mambo ya ujana nilikuwa nafanya sasa hivi yananifikirisha sana, ninawaza sana sina amani nakuwa mnyonge pia
Uliliwa kiboga?
 
Habarini za humu wadau,mimi ni kijana naishi hapa jijini Dar, nina kazi na ninaishi katika harakati zangu za kila siku.

Sasa kuna mambo ya ujana nilikuwa nafanya sasa hivi yananifikirisha sana, ninawaza sana sina amani nakuwa mnyonge pia
Naomba nikupe ushauri Mkuu, unaweza udharau au chukulia poa ila una maana kubwa sana. Ipo hivi kwenye hii dunia ya macho kuna dunia nyingine ya kiroho.
Sasa chochote kinacho tokea kwenye dunia ya macho ya nyama basi ujue kilisha anzishwa kwenye ulimwengu au dunia ya roho, na ukumbuke kuna roho safi ma roho chafu 👻.
Ukiwa karibu na Mwenyezi Mungu basi kaa ujue roho safi zitakupambania na Mambo yako yata enda maana ume karibisha roho safi katika ulimwengu wako wa roho, na ukiwa mtu wa kufanya mambo ya hovyo yanayo mkufuru Mwenyezi Mungu basi utakaribisha roho chafu na hizi ndiyo zitakazo ku control, kazi ya roho chafu ni kuharibu na kufanya uende kinyume kabisa na mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Kuna tabia tuna zilea au tabia tunazo pitia katika makuzi aidha kulelewa kama ulivyo sema ume kuwa uki lelewa na wazazi wa kike sana kuliko wazazi wa kiume, sasa hizo tabia siyo japo sasa hivi tuna ona ni kawaida ila siyo tabia nzuri ndiyo maana Mwenyezi Mungu kwake familia ni Baba, Mama na Mtoto au Watoto.
Familia imara ni silaha kubwa sana kwa shetani 😈, tunaweza mshinda shetani kwa kuwa na familia iliyo imara, Kunapo tokea migogoro kwenye familia basi shetani hushika hatamu ya iyo familia na ata anza angamiza watoto pole pole tangu wakiwa wadogo, mpaka wakija kuwa wakubwa utasikia mtoto huyu anasema mimi nataka kuwa tuu single Mother nimlee mtoto wangu basi, mtoto mwingine ata anza kusema kama hivyo unavyosema wewe kwa sababu tuu umekosa malezi ya baba sasa una anza kuwa inspired na wanaume wenzako wakati wewe mwenyewe ni mwanaume , kuna vitu ulikosa ulipokuwa mdogo, watoto huwa wana nyonya tabia toka kwa wazazi wao, wa kike atanyonya tabia za mama na wa kiume toka kwa baba, sasa mtoto wa kiume muda wote ame kuwa akilelewa na wazazi wa kike tuu unahisi huyu mtoto atanyonya tabia za mwanamke au mwanaume ?! NAOMBA JIBU KA HILI SWALI WADAU.
Kwa mtazamo wangu na jinsi nilivyo ona kwenye jamii, sisi wazazi tusipende kuchukulia suala la familia kama suala jepesi na kuachana ni kitu rahisi kama kunywa maji, wana sayansi wa saikolojia wanalijua hili kuwa mtoto wa kiume akilelewa na mama pekee basi atakuwa na elements za kike ndiyo maana huko kwa wazungu suala ka talaka ni suala jepesi sana, na wana pendelea sana mwanamke kuliko mwanaume mahakamani utaisikia mtoto alelewe na Mama mpaka atakapo kuwa na miaka 18 sasa ishu kama hizi kama ufikirii mbali utafurahia sana ila ukija angalia kwa undani ushoga na usagaji ndiko unapo anzia huko, BABA ana play part kunwa sana kwenye malezi ya mtoto sana tena sana. Sasa we unasem mtoto au watoto walelewe na mama tuu mpaka miaka 18, ukija chukua mtoto hiyo miaka 18 u a kuta tayari ana elements au tabia za aina fulani fulani sababu amekosa malezi toka kwa mzazi wa jinsia fulani.
So Mkuu rudi fanya kuungama au toba mshurikishe Mwenyezi Mungu akupe mawazo tofauti na hayo uliyo nayo maana hapo 😈 amekukalia kitako3muda wote kukupa mawazo ya aina hayo uliyo nayo sasa hayo mawazo na matamanio ya muda mrefu ambayo yametokana na malezi sasa yame enda kuwa tabia mpaka una jiona una tabia.
Badilisha ulimwengu wako wa Roho mkuu, mapepo hayo yamejaa huko kwenye ulimwengu wa 👻 roho .
Muombe Mwenyezi Mungu akupe Msichana aliyeshiba kiimani uwe u a sali naye kanisani.
Huo ni mtazamo wangu kwako Mkuu.
 
Wala hata. Si wamejikubali wenyewe?
Huwezi jikubali kwa kupingana na nature. Never! Sema kwa nje wanajidanganya.
Ukitaka kujua hawajikubali na wapo kwenye mateso makali. Asilimia 90% hutumia madawa au pombe kama sehemu ya kudhibiti hisia mbaya na kujifariji.

Huyu jamaa sidhani kama ni shoga, huyu ana mashaka kuhusu jinsia yake, hajui aegemee wapi

Pale kwenye LGBTQ yupo kwenye 'Q' queer/questioning

AU ana issue nyingine labda alipigwa tukio zito akapoteza network kabisa, mambo ni mengi

Sasa sijui hapo anasaidiwa vipi, aende kwa psychologist

Kwa mwanaume jambo kubwa ambalo atashindwa na kuogopa kulisema ni hilo wadau wanalolihisi.
Sasa mtu anatumia ID fake, Hakuna anayemjua nini kinamshinda kusema anachokabiliwa nacho?
 
Habarini za humu wadau,mimi ni kijana naishi hapa jijini Dar, nina kazi na ninaishi katika harakati zangu za kila siku.

Sasa kuna mambo ya ujana nilikuwa nafanya sasa hivi yananifikirisha sana, ninawaza sana sina amani nakuwa mnyonge pia
Huu ndio msongo wa mawazo au kuchanganyikiwa? Umeandika nini hapa?
 
Habarini za humu wadau,mimi ni kijana naishi hapa jijini Dar, nina kazi na ninaishi katika harakati zangu za kila siku.

Sasa kuna mambo ya ujana nilikuwa nafanya sasa hivi yananifikirisha sana, ninawaza sana sina amani nakuwa mnyonge pia
Ni bora kuweka bayana ili uweze kusaidika mficha uchi hazai
 
Back
Top Bottom