Kuna mtu amewahi kupata kazi ya maana kwa kutumia waganga wa jadi?

Mie wa kwanza...
Nilipitia maisha magumu sana nilivyomaliza chuo

Lakini huwezi amini kuna siku nilitafuta PC yangu usiku nikaanza ku update CV yangu nakumbuka ilikuwa kuanzia saa 5 za usiku hata usingizi sikuwa nao ...

Ilivyofika saa 8 usiku nikachukua udhu nikasimama kwenye nkeka na kuanza kumlilia Allah hadi saa 11 Alfajiri nikawahi wa kwanza mskitini nikapiga rakaa 2 za kabla ya sala ya Alfajiri au Subhi.

Finally nilikaa 02 tu nikapigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ameagizwa anipe nafasi kwenye kampuni moja ya minara ya simu hapa nchini...


Mganga tena mwaminifu ni Allah pekee achana na hao wengine ni watafuta rizki kama viumbe wa Allah wengine.
 
Tumesema wafia dini za kuletewe anzisheni uzi wenu..mbona mnapenda kuingilia nyuzi za mambo ya kiasili..viherehere tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Achana na waganga matapeli wa dar hao.

Njoo huku kwetu morogoro nikupeleke kwa wataalamu huko ifakara ndani ndani.

Vijana msione watu ni mawaziri mkadhani ni bahati, ile ni kazi ya ndumba
Mhhh mkuu ifakara Kuna waganga tangu lini labda ilonga
 
Ukiamini "maisha ni mchezo" hata waganga wa kweli wapo. Sitakutajia majina ila watu wengi waliofanikuwa wamepitia kwa kalumanzila.
 
Nina shuhuda mbili ambazo sometimes huwa zinanipa msukumo wa kuamini haya mambo.

Kipindi cha Mzee Kikwete kuna waziri mmoja nilikutana naye kwa mganga wa jadi. Mimi nilikuwa na tatizo la kiafya ingawa nilipigwa tu hela zangu maana baadae sana ikaja kugundulika ni TB wakati yye alisisitiza nimepigwa msumari .

Sasa yule muheshimiwa alikuwa mbunge hivyo alikuwa anautaka uwaziri . Yule mtaalamu akamwambia utaupata bila shida na kweli bwana mkeka wa mawaziri ulivyotoka tu jamaa akapewa wizara nyeti sana sitoitaja watu mtaunganisha dot.

Ya pili kuna shemeji yangu ni mjeda wa kuvaa combat alikuwa na msala huku bara hivyo alitakiwa kuhamishiwa visiwani Zanzibar . Akaenda kwao kurekebisha michongo matokeo yake amepelekwa Dar badala ya Zenji. Na yeye alikuwa hataki kwenda zenji.

Hivyo mkuu usidharau nguvu za kitamaduni. Ila mimi nahisi zinakupa majibu chanya iwapo utakuwa na imani nayo tofauti na hapo utakuwa kama mimi tu.
 
Ulimlipa Million ngapi
 
Endelea na story Bro
 
Haya mambo yapo kuna jamaa angu alitafta kazi mda mrefu bila mafanikio interview nyingi lakini wapi, kuna siku tulienda kwa babu mmoja, alimpa dawa moja ivi ilikua kama unga akamwambia siku akienda kwenye interview, aweke ile dawa chini ya ulimi afu asiongee chochote mpaka wale wanao mpigisha interview waanze wao kuongea. Wakianza tu ameze ile dawa ndo aongee, akafanya hivo alifaulu ule usaili akapata kazi mpaka saiv maisha yake yemesimama hatari Kiukweli aya mambo yapo
 
Unapoona mganga anatoa pesa yake mfukoni kwenda kuchapisha mabango ya matangazo ambayo kayazungusha mji mzima kwenye nguzo ili apate wateja utagundua dhana ya mganga kumfanya mtu afanikiwe kwa ndumba ni uwongo na utapeli
Umeona eenhh?!!!.Upo sahihi kabisa.
 
Achana na waganga matapeli wa dar hao.

Njoo huku kwetu morogoro nikupeleke kwa wataalamu huko ifakara ndani ndani.

Vijana msione watu ni mawaziri mkadhani ni bahati, ile ni kazi ya ndumba
Hamna lolote
 
Mkuu.umenikumbusha kuna kipindi bro wangu alikua na kesi ya roberry..tukaenda huko morogoro kwa mtaalamu..at the beginning bro alikua kapigwa 30 yrs..surprisingly bro akachomoka kwenye rufaa kama babu alivyotuahidi.
Ni MUNGU tu ndo aliwasaidia na wala sio huyo mzee.
 
Wewe utakuwa kibaraka wake au agent unataka upate ulaji na wewe.
 
Tupeko connection mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…