Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Kufulia kunaleta akili ya ziada, kuna zile hela huwa zinaanguka chini ya kitanda hasa sarafu 100, 200 au 500 sasa ukitaka kujua thamani yake siku ufulie mazima huwa zinatafutwa kila kona ya chumba.. unapitia nguo moja moja kujua kama kuna akiba yoyote hapo orodha ya watu wa kukusaidia inazidi kujipanga kichwani na sababu za kuwapa.. "ipo siku tu.."
 
PESA PESA PESA Dah Sijui nani alievumbua haya mambo

Nilishinda siku 6 bila ya kula chakula chochote. Ulikua ni mwendo wa kunywa maji tu dumu za kuogea nilizimaliza zote. mwisho niliumwa na tumbo vibaya mno, ilikua ni michubuko tumboni.
Kwamba ukae siku sita bila kula chochote halafu usife?
 
hahhh yaani kasheshe mkuu
 
Cha muhimu maisha yaendelee, tungekuwa wezi, akili ingekimbilia kwenye kuiba ili kutatua tatizo.
 
umenikumbusha wakati nasoma advance likizo nilikuwa nabaki hapo mkoani kwa ndugu. tuition walikuwa wananilipia ila kuna likizo waliishiwa mama akaniomba nimkope [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaah
 
Andika vizuri khaaah
 
Alafu katu Haina taarifa, shida huingia shida Bila hodi sio kwa mkubwa wala mtoto wote shida. Pia haikosekani hata ikiwa siku ya harusi, si masikini wala matajiri wote shida. Kikubwa marufuku kukata tamaa.
 
Alafu katu Haina taarifa, shida huingia shida Bila hodi sio kwa mkubwa wala mtoto wote shida. Pia haikosekani hata ikiwa siku ya harusi, si masikini wala matajiri wote shida. Kikubwa marufuku kukata tamaa.
 
Hivi ni lini Tanzania iliishiwa pesa? na ilichukua hatua Gani? Kufulia Kwa nchi sio mchezo kama Tanzania ikifulia Kuna rasilimali nyingi za kuzipush kuanza na zile pembe za ndovu za kwenye Royal tour.
 
Daaaaah sa c mrudiane tu mnakwama wap ujue ndo ashakuombamsamaha hivo!
Maisha yanapiga Mwaisa mpaka Maji tunaita Mmma.
 
Sitaisahau Manzese Argentina, pale kulikua na mzee mmoja ana uza maandazi mia na chai mia, usiku kibao nimelalia mia tano, kuna wakati unakua una mia tano tu mfukoni, unasema hii jero ntaenda zangu jioni kwa mzee nile maandazi manne na chai moja. Enzi izo nilikonda kama mbwa, hali mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…