Mexico Kundi za DRUGS DEALER ndo ishu ila ukiamua kuishi kwa hamsini zako bila kuingilia Anga zao hakuna tabu utapata
Ila sasa SOUTH kuna VITA aina nyingi sana ambavyo vinaweza kukutoa UHAI wako muda wowote
Mexico Kuna biashara haramu na uhalifu wa kila aina , hao drug cartels wanamiliki territories na wanafanya uhalifu kama utekaji ,ujambazi ,human trafficking ,biashara haramu ya viungo vya binadamu , black mail nk
Kiufupi ukiona hili neno "Cartel" ujue ni organized crime gangs
Cartels za Latin America zinafanya kila biashara haramu siku hizi
Wewe unaweza ishi sehemu yenye ujambazi ,au utekaji ili walipwe ransom ,au utekaji na mauaji ya watu ili kupata viungo kama maini , mapafu ,figo nk ? ,bila shaka hautakuwa safe kwa namna yoyote ile kukaa eneo hili , mfano kwa sasa hayo magenge ya wahuni yanatoza ushuru mpaka wale wahamiaji haramu wanakimbilia Marekani kwa kupitia porini au miji ambayo hao wahuni wanaishikilia kama territories zao , Newyork times waliwahi andika mwaka huu kwamba hayo magenge yamepata zaidi ya dollar billion moja kama makusanyo ya hizo tozo za wahamiaji wanakimbilia Marekani
Sasa imagine hicho ni chanzo kimoja tu cha mapato , bado hawajauza cocaine na madawa mengine , hawajafanya kidnapping nk , bila shaka hao wahuni watanunua silaha nzito ,vifaa na kuongeza nguvu kazi zaidi na kujitanua na kuwa hatari zaidi .