Kuna sehemu hatari kuishi kama South Africa?

Kuna sehemu hatari kuishi kama South Africa?

Nchi imevurugwa ile
South Africa ina wahuni ,ila wahuni halisi dunia hii na magangwe wako kule Amerika ya kusini , lile bara almost kila nchi inatatizo kubwa la magenge ya wahuni na wahalifu wa mitaani ,vitu kama ujambazi ,madawa ya kulevya ,utekaji , biashara haramu ya human trafficking , viungo vya binadamu nk
Kila biashara chafu zinafanyika pale
 
Johannesburg watu karibia 3000 wamepigwa risasi sidhani rio au mexico city inafikia
Ila Rio kule Brasil lile jiji lina kizazi cha laana sana ,kuna video nilicheki wahuni wanavamia bus stations vituo vya polisi na wanajeshi ,wanateka na kufanya massacres kabisa live live na wanarusha kwenye mitandao
 
ila kwa pisi kali ukija tanzania mademu zetu unawaona kama masokwe
Huyu ni Mbongo au Msouth? Ukijibu hili swali ndio nitakuelewa ulichomaanisha usichokijua wapo wabongo mixing na South
Screenshot_20240322-145217.png
 
south Africa wanauwana kwa kupigana sana risasi,ila nchi za S.America wanauwana sana tena kinyama,kuchinjana,kukatana miili vipande kama mishakaki,ni vile zipo mbali hatusikii mamabo yao.
Huwa nafuatilia crime incidences zao kupitia documentaries za National Geographic ,aisee Yale majitu ni makatili sijawahi ona
Yaani waavyouana kule hata Mungu hapendi aisee
 
mwezi wa 10 last yeakr niliingia south Africa. Ila February nikarud bongo nilifanikiwa kutembelea mikoai karibu yote

South Africa kimaendeleo imezidi nchi nyingi sana za ulaya ,Asia ,na america yaani south Africa ipo mbali san kiuchumi.

Tatizo Ina raia wenye hasira sana mara nyingi ni watu wenye kinyongo na kulipa kisasi yan dakika sifuri tu unawezA kupoteza uhai

Swala la mapenzi south Africa ni next level Kuna mchezo unaitwa sleep over.
Yani unawezA kukutana bint kituo Cha tren ukaomba namba ukifika home unamuomba aje alale kwako simply anakuja kesho anaondoka then unatafuta mwingine simply tu.

Shule south Africa wanafunzi wanavaa nusu uchi kama south Korea .
Ushoga na usagaji kwao sio kitu Cha kushangaza.
Vinchi vingi vya SOUTH AMERICA ile LATIN AMERICA wanaishi GANGSTER LIFE.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
South Africa, nimeenda saana kumtibu mzazi wangu, hadi akaenda mbele ya haki. Wana hospitali nzuri saana illa gharama mno. Karibia miaka 6. Na killa mwaka naenda kwa biashara za spare parts na malori. Illa nimepunguza nakaa wiki 2 au tatu. Ni miji mingi nimetembea. Illa katika Africa na baadhi hata za nchi ulaya ipo mbaali sana kimaendeleo ni kuzuri. Tatizo kubwa usalama. Niliyo yaona live mara nne na kukoswa mara mbili. Na kuyakuta kwa watu tayari yametokea.. kusema kweli ina magenge hatari saana na hata polisi hawawezi kusaidia. Kuua ni dakika hata pesa ndogo tu. Usiku kimyaaa. Mchana we na bahati. Na wakishuku una pesa hata kidogo utafuatiliwa hata wiki kwa plan y uhakika. Na wakiamua kupora na kuua hawarudi nyuma. Ni nchi 1 Africa kwa hatari, tena meengi yanapita bila kutangazwa. South Africa very beutiful illa kwa amani na usalama HAPANA.
Illa kwa ukanda huu ipo mbali kwa mambo mengi muhimu ambayo ukijipanga na kuwa muangalifu utayapata.
 
Hasa iyo El salvador kuna makundi mawili moja linaitwa MS 13 na 18.yan kila raia anaezaliwa lazma awe kund moja kati ya hao na wana mitaa.
Halafu hao wahuni walitokana na kizazi cha kishenzi kilichozamia Marekani miaka ya 70 na 80 huko ,wakafanya uhuni Marekani na wengine wakaanza kufungwa na kurudishwa hizo nchi za Latin America na hao waliorudishwa na kutolewa magerezani Marekani kipindi kile cha Reagan ndio hao kizazi jeuri wakaendeleza umafia wao waliokuwa wanafanya kwenye miji ya Marekani hasa Chicago ,Los Angeles ,San Francisco , Newyork nk
Hayo magenge ya MS 13 & 18 yalianzia Marekani
 
Hakuna sehemu SA utafananisha na umafia wa Mexico City wale Wauza sumu wakiamua ipo mitaa hakuna mtu anatoka nje kitu ambacho SA hawajafikia huko na pia SA sehemu yeyote Polisi wanaweza kuvamia na wakatoka salama kitu ambacho Mexico ni ngumu mpaka watumie jeshi...
Wale wahuni wanazipiga mpaka na wanajeshi , yaani wanajeshi , paratroopers commandos wanakuwa supported na helicopters Ila bado mpaka leo kuna mitaa imeshindikana kuikomboa
 
Wale wahuni wanazipiga mpaka na wanajeshi , yaani wanajeshi , paratroopers commandos wanakuwa supported na helicopters Ila bado mpaka leo kuna mitaa imeshindikana kuikomboa
Wale jamaa wamesambaza watoa habari wao kila kona mpaka sehemu za ibada wakipata taarifa pana kiongozi wa Kanisa anawazungumzia kwa mabaya watakuja kumteka siku ingine ya ibada wale sio watu kabisaa...
 
Huwa nafuatilia crime incidences zao kupitia documentaries za National Geographic ,aisee Yale majitu ni makatili sijawahi ona
Yaani waavyouana kule hata Mungu hapendi aisee
kuna kuuwa na kuuwa kinyama,South Africa watu wanauwa,ila huko America ya kusini watu wanauwa kikatili(kinyama).

yani wanakuuwa hata ndugu wanaotafuta watu wao waliopotea hawajui kama huyo aliekatwa vipande na kutolewa macho ni ndugu yao au la.
 
Sasa hujatembea sehemu zingine za dunia unataka kusema South Africa ndio sehemu hatari ya kuishi.

Kuna nchi kama Haiti, El Salvador hizi ni moto wa kuotea mbali raia karibu wote washapinda.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Amezungumzia NCHI iliyoendelea KIUCHUMI na SI SALAMA kuishi
Nchi ulizozitaja haponi MASIKINI wa kutupwa hata TANZANIA tuna afadhari
 
Wale jamaa wamesambaza watoa habari wao kila kona mpaka sehemu za ibada wakipata taarifa pana kiongozi wa Kanisa anawazungumzia kwa mabaya watakuja kumteka siku ingine ya ibada wale sio watu kabisaa...
Kuna muda zile nchi za Latin America zitaongozwa na cartels za wahuni ,
Ni kama Ecuador kilichotokea mwezi uliopita
Wale washenzi Ile Latin America kuna kipindi zile serikali zote zitaanguka na itakuwa miliki ya wahuni .
Nadhani USA watapata shida sana maana watazalisha wimbi kubwa mno la wahamiaji watakaokuwa wanakimbia hizo nchi , mfano kinachoendelea sasa hivi kule Haiti na Ecuador ,watu wengi wamezikimbia hizo nchi wanakimbilia Marekani
 
Mexico sio Nchi ile unakuta karibu watu wengi wamejichora tattoo wao wanazielewa wewe ambae hauna tattoo yeyote unaweza kumuuliza kitu akakuangalia tu au akivurugwa anakuchapa risasi ile ndio Nchi niliona mtu anatumwa dukani anakumbushwa kuchukua na bastola...
Mexco ni kwenye mitaa ya wauza unga, kama wewe sio police na wala sio muuza unga haaana shida na wewe, Sasa South tu mambo ya kuchukuliana wanawake hii ni kosa kubwa.
 
Back
Top Bottom