Kuna shida gani kati ya Makonda na Mchengerwa?

Wewe Dr. wa nini umeshindwa hata kuandika kwa dondoo Makonda kafanya nini na Mchengerwa kafanya nini?
 
Mimi ni shabiki pro wa Makonda yangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni. Waziri Mchengerwa yupo sahihi kwasababu ndiye anayesimamia TAMISEMI yenye jukumu la kukarabati barabara, usimamizi wa elimu, afya nk huko mikoani.
 
Mkuu Mchengerwa ni Waziri hapa Tanzania yupo juu ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya.. Kiutumishi Tamko la waziri linafunga mjadala..
Kama una shida binafsi na Waziri much better communicate with him and fix the matter... kukaa kwako Ottawa, Canada haitusaidiii
 
😆😆
 
Megalodon hujui kuwa waziri wa TAMISEMI ndo boss wa wakuu wa mikoa? Wewe na Makonda ni wajinga mno. Kauli ya Makonda iko kinyume kabisa na utawala wa kisheria. Wananchi wakiwafanyia hivyo madiwani na watendaji wengine wa chini unadhani kutaendelea kuwa na amani? Kauli ya Mchengerwa kama waziri iko sawa. Makonda ni mtu wa kuropoka mno.
 
Wananchi wakifanyiwa je ?
 
Ukumbuke Kuna mmoja hapo ambaye ni mkaza mwana wa Saa100 hapo
 
Mpe basi huo uwaziri wa Tamisemi huyo Makonda kama anafaa.
 
Mchangarwe ni Rais ajaye upende usipende.
 
Mkuu nimewasikiliza.
Kwa maoni yangu Makonda hakua sahihi. Lakini pia waziri wa TAMISEMI ndo immediate boss wa RC/DC. Hivyo waziri wa TAMISEMI anaweza kuelekeza RC Kufanya jambo fulani. Shida ya makonda hataki kuwa "mdogo".
Yaani mleta mada anamuwekea DHAMANA Bashite!!..yule hana A,B , C za Uongozi...ngoja Mama aendelee kumkumbatia..kuna siku isiyo na jina,ataleta AIBU kubwa nchini
 
Kitu hujui uliza! Mshahara wa Makonda nani anauomba Bungeni? Jibu Mchengerwa. Pamoja na Mkuu wa Mkoa kuwa mwenye mkoa, kama Rais Alivyo na nchi, bado yupo chini ya TAmisemi
 
Duu!
 
Mwandiko na mtiririko wa Uzi wako haviendani na mtu anayejinasibu kuwa daktari.
Hata kama ma daktari wanaandika kwa kucharaza, huu wa kwako ni majanga.
Kingereza usiombe kiswahili ndio kabisa.
Nawaonea huruma wagonjwa wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…