Kuna shida gani kati ya Makonda na Mchengerwa?

makonda for kigamboni, kigamboni mpya na makonda, mtendaji asipoziba korongo makofi
 
Mkuu mimi nina maoni tofauti na yako kama ifuatavyo;
1. Mkuu wa mkoa hakufanya sawa kuchochea vitendò vya wananchì kuwadhihaki viongozi kama walivyofanya.
2. Waziri alikuwa sawa tu kumkumbusha mkuu wa mkoa kwenye maadili ya uongozi kuwa badala ya kuchochea vurugu ni vizuri wananchi na viongozi wakatafutà Suluhu bila machafuko.
3. Kiuongozi waziri wa Tamisemi ni boss wa mikoa, wilaya, Tarafa, kata, mitaa, vitongoji, mpaka vijiji. Kwa maneno mengine waziri wa tamisemi ndio anasimamia Tanganyika ( naingiza jokes kidogo kwa kusema kuwa waziri wa Tamisemi ndio rais wa Tanganyika hata bajeti yake ni kubwa kuliko wizara zote). Kwa hivyo Mchengerwa ni boss wa Paul.
4. Kuhusù Nepotism hapa sijui sana lakini kama jamaa ana vigezo vyote vya kuwa waziri basi Acha awe waziri kuoa mtoto wa rais kusimnyime fursa zingine kwa sababu yeye ni mtanzania kama mimi na wewe tu mkuu.

5. Mkuu wa mkoa ni manipulative leader yaani anachofanya anataka kusepa na kijiji na kuzoa umaarufu yaani anafanya yaleeeee ya Shujaa wa Africa.
 
Sawa wasalimie Otawa
 
Naunga mkono hoja,
Makonda ni jembe kazi
P
 
👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏
 
Mkwe vs Mtoto pendwa.....tuone mwisho wake....
Mkwe hana maana! Amwache Makonda ainyooshe Arusha.
Asilete kiburi cha kuitwa mkwe wa rais.
Mimi nakubaliana kwamba hicho cheo hakutakiwa kuwa nacho kwasababu akifanya makosa mama mkwe ataona haya kumuwajibisha mkwewe kwasababu akiwajibishwa binti wa rais atanuna kwanini mumewe anaonewa.
Mfano mzuri ni mkuu wa majeshi wa Uganda Muhoozi Kaenerugaba!
Upuuzi na upumbavu mwingi anaoufanya mitandaoni huko Twitter kama sio mtoto wa rais angekuwa alishatumbuliwa zamani lakini Museveni anashindwa hata kumkemea kwa sababu ni mwanae na anamwandaa kumrithi.
Kwa kumalizia kwamba kwa mtazamo wangu watoto wa viongozi wakubwa wa nchi pamoja na wakwe zao au shemeji zao hawapaswi kupewa vyeo vikubwa serikalini kwa sababu inakuwa vigumu kuwawajibisha pale wanapokosea.
 
Hamna shida yeyote kabisa, and everything is normal, Makonda alihimiza uwajibikaji, Mh mchengerwa alieleza tu utaratibu wa kufuatwa katika kuwajibika, Kama Waziri anayehusika na TAMISEMI lazima akikishe taratibu zinafuatwa.
Makonda na Mchengerewa ni team Samia.
 
Acha chuki ndugu, mara unadai kuwa mchengerwa kapata through nepotism, mara hujui kapataje uwaziri, Dr gani ambaye huwezi kupangilia taarifa yako!!! Au umetumwa? Ne serious brother, acha wivu ambao hauna tija Kwa wenzako.
Umeona eeh! Siku zote nikiona wanaomsifia Makonda akili yangu huwa inanituma huyu mtu atakuwa ameongwa kuandika huu upumbavu.Mwenye akili timamu sidhani kama anaweza kumweka Makonda kwenye list ya viongozi bora, na ukiona kiongozi anapenda kujianika kwenye mitandao kupita kiasi jua hakuna kitu.
 

Makonda anajiona yeye ndiye mtoto wa Mama kwa ego yake. Mchengelwa mkwe mwenye majigambo
 
Ya kusema RC siyo mwanasiasa haileti maana wakati huwa tunaona wakivaa zare za chama. Kama RC siyo mwanasiasa kuvaa sare ya chama inamaanisha nini?
 
ifike sehemu tuache kubebelezana diwani anapita na landcruiser anawaacha wananchi wanahangaika na wanajua kabisa uwezo anao hata kwa kutumia pesa yake mfukoni, kwanini wasimzibie njia, kama watu nchi nzima hawawajibiki wacha waliwe makofi nchi nzima
 
Mchengerwa hana mandate juu ya mkuu wa Mkoa, RC ni presidential appointment na Waziri ni presidential appointements hivyo wote wapo sawa mbele ya boss.
Hapa umechemka. Kwamba wote wameteuliwa na Rais, haina maana wako sawa mbele ya Rais. Hata Waziri mkuu naye anateuliwa, utasema yuko sawa na RC?

Huwezi kumfananisha RC na Cabinet member.
 
Huyo mchengerwa aliye sama Raia kwake ni mavii tu ndiyo unamtegemea kujali utendaji😅😅😅😅
 

MCHENGERWA ni Mkwe mwenye Kifua Kipana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…