Kuna siri gani kati ya mabasi ya mikoani na hizi hoteli wanazosimama kulisha abiria?

Kuna siri gani kati ya mabasi ya mikoani na hizi hoteli wanazosimama kulisha abiria?

Wale wezi wezi tu mm km natoka mwanza nachukua sato wangu anakaangwa na ndizi mzuzu natia kwenye kikontena biashara imeisha hapo ni pepsi take away na kula samaki safiiii nagika dar nimeshiba kuliko kwenda kununua ma vitu bei juu ubora ziroo unakula roho inauma.
 
Huwa kama sio hotel ya wenye mabus basi hayo mabus wamiliki huwa wanapata comission kila baada ya muda fulani.

Yani utakuta mwenye hotel anakula deal na mwenye bus zikipita hapo kwa mwezi anampatia commission kiasi fulani.

Kiukweli kama unasafiri na nilazima ule njiani basi bora tu uandae msosi wako nyumbani ubebe take away. Otherwise ni heri ukanunua vi bites bites tu na maji maana kinachoendelea ni wizi mtupu.

Serikali iingilie kati.
Wameongea na madereva, Dereva anakula na kondakta wanakula bure na dereva anapata sh 10,000 kila akisimama pale,either uamue kupewa hapo hapo au yote kwa mwezi ni makubaliano yenu
 
Je, ni kwamba hizi hotel zinamilikiwa na hawa wenye mabasi au wenye mabasi wanapata nini hapa maana unakuta mabasi yanaendelea kusimama katika hotel hizihizi licha ya hotel kuwa na;

Huduma mbovu na ghali - Vyakula ni ghali hlf vina viwango duni. Unaagiza chakula ni basi tu kupooza njaa lakini kimsingi unakula makapi! Chipsi na zile nyama choma haviivi inavyotakiwa.

Mazingira mazima hasa chooni machafu na yasiyoridhisha.

Hapa shida ni nini wakuu? Maana siamini kama hakuna wawekezaji wanaoweza kuweka mzigo huko na kutoa huduma ya kueleweka.
ukipata muda kwenda kwenye majiko wanakopikia, na usafi wa hao watu kabla na baada ya kutembelea msalani, siharibu biashara za watu ila muwe makini sana na matumbo yenu. usipoharisha leo, unaweza kupata taifodi itakayoibuka kesho. kuna siku niliwahi kula chakula pale al jazeera kabla ya kitonga, nilijuta. unaweza kuomba ushukie iringa hata kama ulikuwa hauishii hapo ili upate huduma ya choo bila bughudha. kuna mwamba mmoja alishawahi kujititia kabisa tena mwanaume kwenye basi kwasababu ya kulakula safarini hiyohiyo. kwahuruma akashuka katikati ya safari basi lote harufu. na hawa wenye mabasi wabaya sana, akisimama morogoro dakika 10, ataenda kusimama sehemu moja tu kabla hajafika kituo cha mwisho cha saa 12 jioni.
 
Je, ni kwamba hizi hotel zinamilikiwa na hawa wenye mabasi au wenye mabasi wanapata nini hapa maana unakuta mabasi yanaendelea kusimama katika hotel hizihizi licha ya hotel kuwa na;

Huduma mbovu na ghali - Vyakula ni ghali hlf vina viwango duni. Unaagiza chakula ni basi tu kupooza njaa lakini kimsingi unakula makapi! Chipsi na zile nyama choma haviivi inavyotakiwa.

Mazingira mazima hasa chooni machafu na yasiyoridhisha.

Hapa shida ni nini wakuu? Maana siamini kama hakuna wawekezaji wanaoweza kuweka mzigo huko na kutoa huduma ya kueleweka.
Una hoja ya msingi. Hizo hotel ziko za aina mbili. Kuna ambazo wenyewe ni wamiliki wa hayo mabasi hivyo hupata faida ya moja kwa moja kutokana na wateja kuhudumiwa hapo. Na nyingine ni za wajanja tu wameamua kujenga sehemu za porini halafu wakaongea na madereva ili wawe wanasimama hapo. Kawaida madereva hupewa chakula na vinywaji vya bure na pengine posho ya fedha.
Huu ni uzembe wa serikali. Ilitakiwa mabasi yote yawe yanasimama stendi za umma ili wasafiri wachague sehemu na huduma wanayotaka.
 
Kama vipi rudi kwenye ule utaratibu waliotumia wazazi wako enzi hizo wanasafiri. Yaani ule usiku wa kuamkia siku ya safari, andaa chakula chako kizuri! Weka kwenye chombo chako kisafi! Safiri nacho.

Kwa hiyo wakati wenzako wanashuka kwenda kununua hivyo vyakula bibaya, na vya bei kubwa! Wewe nenda kachimbe dawa tu na kurudi kwenye basi. Njaa ikikuuma, unakula chakula chako.

Kulalamika lalamika tu hovyo wakati mwingine kunaweza kukupunguzia siku za kuishi.
 
Kauli ya kizembe kabisa hii.

Kama ulikuwa haujui basi ufaham kuanzia leo kuwa hautakiwi kuacha kulalamika kwa unachokiamini.

Ndomaana wazee wetu walipigana kupata uhuru huo unaokufanya ushike na kubofya hiyo simu na kuandika hapa bila bughudha, huko ni kulalamika. wafanyabiashara hata wale wakubwa wa kariakoo, boda, machinga wote hawa wanalalamika kwa viongozi ndo mambo yao yanatazamwa na kunyooshwa.

**Usiogope kulalamika.
 
Kama vipi rudi kwenye ule utaratibu waliotumia wazazi wako enzi hizo wanasafiri. Yaani ule usiku wa kuamkia siku ya safari, andaa chakula chako kizuri! Weka kwenye chombo chako kisafi! Safiri nacho.

Kwa hiyo wakati wenzako wanashuka kwenda kununua hivyo vyakula bibaya, na vya bei kubwa! Wewe nenda kachimbe dawa tu na kurudi kwenye basi. Njaa ikikuuma, unakula chakula chako.

Kulalamika lalamika tu hovyo wakati mwingine kunaweza kukupunguzia siku za kuishi.
Umeandika vitu ambavyo havipo...

Nimetoka Dar es salaam kwenda mbeya Kama mfanyabiashara/ mfanyakazi nimelala lodge Kwa siku mbili siku ya kurudi kutoka mbeya atanipikia nani ili nibebe chakula!

Na sio Kila mtu anaweza kubeba mahotpot safarini
 
Madereva na makonda wa hayo mabasi huwa wanapewa chakula kama offer ya kupeleka wateja kwenye hizo hoteli/ migahawa ya chipsy vijiko viwili buku 5 na nyama mbichi/ zisizoiva sawasawa. Mfano Singida pale nje ya mji karibu na mizani kama unaelekea Mwanza
 
Back
Top Bottom