Kuna siri gani kati ya mabasi ya mikoani na hizi hoteli wanazosimama kulisha abiria?

Kuna siri gani kati ya mabasi ya mikoani na hizi hoteli wanazosimama kulisha abiria?

Umeandika vitu ambavyo havipo...

Nimetoka Dar es salaam kwenda mbeya Kama mfanyabiashara/ mfanyakazi nimelala lodge Kwa siku mbili siku ya kurudi kutoka mbeya atanipikia nani ili nibebe chakula!

Na sio Kila mtu anaweza kubeba mahotpot safarini
Pole. Unatakiwa kuridhika na hali halisi unayokutana nayo. Maana siyo rahisi kupata kila kitu unachokipenda kwa ubora unaoutaka wewe.
 
Huwa kama sio hotel ya wenye mabus basi hayo mabus wamiliki huwa wanapata comission kila baada ya muda fulani.

Yani utakuta mwenye hotel anakula deal na mwenye bus zikipita hapo kwa mwezi anampatia commission kiasi fulani.

Kiukweli kama unasafiri na nilazima ule njiani basi bora tu uandae msosi wako nyumbani ubebe take away. Otherwise ni heri ukanunua vi bites bites tu na maji maana kinachoendelea ni wizi mtupu.

Serikali iingilie kati.

Mimi nimeshaacha kununua vyakula na vinywaji,huwa nafungasha toka home au stendi kabla sijaondoka,mana wale wauzaji wa hizo hotel huwa wanatafuta super profit.
 
Pole. Unatakiwa kuridhika na hali halisi unayokutana nayo. Maana siyo rahisi kupata kila kitu unachokipenda kwa ubora unaoutaka wewe.
Hii ndio sababu nikiwa natokea nyanda za juu kusini napenda kupanda basi za abc- nashukia kwenye hotel yao pale morogoro kula.

Mazingira yapo safi japo Bado gharama haziendani na vyakula
 
Mimi nimeshaacha kununua vyakula na vinywaji,huwa nafungasha toka home au stendi kabla sijaondoka,mana wale wauzaji wa hizo hotel huwa wanatafuta super profit.
Ni kweli, vyakula vya huko vinauzwa thrice the price. Nilishaachaga huo ujinga. Maana gharama ya njiani unatumia mara tatu ya kawaida na still hata quality hupati unaishia kuumwa tumbo. WTF? Unanunua ugonjwa bei ghali?
 
Hao waarabu wanauza vyakula vimechacha walikua na ingine mombo imekufa ...wamefungua ingine mombo nayo haina wateja,uhakika wa chakula kizuri njia ya arusha ni korogwe tu unakula kitu fresh
ukipata muda kwenda kwenye majiko wanakopikia, na usafi wa hao watu kabla na baada ya kutembelea msalani, siharibu biashara za watu ila muwe makini sana na matumbo yenu. usipoharisha leo, unaweza kupata taifodi itakayoibuka kesho. kuna siku niliwahi kula chakula pale al jazeera kabla ya kitonga, nilijuta. unaweza kuomba ushukie iringa hata kama ulikuwa hauishii hapo ili upate huduma ya choo bila bughudha. kuna mwamba mmoja alishawahi kujititia kabisa tena mwanaume kwenye basi kwasababu ya kulakula safarini hiyohiyo. kwahuruma akashuka katikati ya safari basi lote harufu. na hawa wenye mabasi wabaya sana, akisimama morogoro dakika 10, ataenda kusimama sehemu moja tu kabla hajafika kituo cha mwisho cha saa 12 jioni.
 
Huwa kama sio hotel ya wenye mabus basi hayo mabus wamiliki huwa wanapata comission kila baada ya muda fulani.

Yani utakuta mwenye hotel anakula deal na mwenye bus zikipita hapo kwa mwezi anampatia commission kiasi fulani.

Kiukweli kama unasafiri na nilazima ule njiani basi bora tu uandae msosi wako nyumbani ubebe take away. Otherwise ni heri ukanunua vi bites bites tu na maji maana kinachoendelea ni wizi mtupu.

Serikali iingilie kati.
Haswaaa
 
Kuna hapo nangulukuru aiseee chipsi vijiko viwili tu ni 2000 tsh. Kuna siku kidogo nisuse ila nikaona sio kweli basi nikachukua kinyonge tu.
Haha ukakumbuka kwamba hata ukisusa huwakomoi ukaona ubebe tu, maana wale hawabembelezagi mtu wanakutajia bei zao huku wanaendelea na shughuli nyingine, unataka nunua hutaki acha
 
Je, ni kwamba hizi hotel zinamilikiwa na hawa wenye mabasi au wenye mabasi wanapata nini hapa maana unakuta mabasi yanaendelea kusimama katika hotel hizihizi licha ya hotel kuwa na;

Huduma mbovu na ghali - Vyakula ni ghali hlf vina viwango duni. Unaagiza chakula ni basi tu kupooza njaa lakini kimsingi unakula makapi! Chipsi na zile nyama choma haviivi inavyotakiwa.

Mazingira mazima hasa chooni machafu na yasiyoridhisha.

Hapa shida ni nini wakuu? Maana siamini kama hakuna wawekezaji wanaoweza kuweka mzigo huko na kutoa huduma ya kueleweka.
1. Dereva na kondakta hula chakula bure
2. Dereva hupewa posho
3. Woteli huingia mikataba na wenye mabus
4. Hotel za wenye mabus mfano Dar express, kilimanjaro hawa wana hotel zao wenyewe.

Njia ya kaskazini huongoza kwa hotel nzuri, barabara zingine hotel za hovyo mno
 
Hii ndio sababu nikiwa natokea nyanda za juu kusini napenda kupanda basi za abc- nashukia kwenye hotel yao pale morogoro kula.

Mazingira yapo safi japo Bado gharama haziendani na vyakula
Yeah kwa Morogoro sehemu nzuri za kula na kuchimba dawa ni hapo Cate hotels na pale Msolwa kituo cha mafuta, ila Msamvu ni upuuzi mtupu na huko ndiko mishikaki ya paka na mbwa, na vikorokoro vingine vya ajabu ajabu hupatikana sana
 
Kwani route nyingi hawajifunzi kuwa na hotel bora kama kaskazini?
 
Back
Top Bottom