Kuna siri gani kati ya mabasi ya mikoani na hizi hoteli wanazosimama kulisha abiria?

Kuna siri gani kati ya mabasi ya mikoani na hizi hoteli wanazosimama kulisha abiria?

Je, ni kwamba hizi hotel zinamilikiwa na hawa wenye mabasi au wenye mabasi wanapata nini hapa maana unakuta mabasi yanaendelea kusimama katika hotel hizihizi licha ya hotel kuwa na;

Huduma mbovu na ghali - Vyakula ni ghali hlf vina viwango duni. Unaagiza chakula ni basi tu kupooza njaa lakini kimsingi unakula makapi! Chipsi na zile nyama choma haviivi inavyotakiwa.

Mazingira mazima hasa chooni machafu na yasiyoridhisha.

Hapa shida ni nini wakuu? Maana siamini kama hakuna wawekezaji wanaoweza kuweka mzigo huko na kutoa huduma ya kueleweka.
Fungasha ugali na nguru kutoka nyumbanj. Wakitua hotelini wewe unamega tonge tartiib kwenye siti
 
Jana nilitoka safari yangu kutoka Dodoma na Bus la Shabiby tulipofika Morogoro tulipelekwa kula kwenye hotel mbovu sana, vyakula hivyo kabisa, hivyo vyoo ni vichafu sana mimi na Abiria mwenzangu tukahoji lakini hawakuwa na majibu ya kutosha

Nilichogindua dereva na wahudumu wa bus wanapata chakula bure pale.

Mbona Bus za ABC wanahotel nzuri tu, shabby ameshindwa je?

I second you mkuu, mm mwenyewe leo nimepita na shabiby aisee huduma ya pale morogoro zile sehemu za maliwato, hoteli ni mbovu sijawahi ona.
 
Je, ni kwamba hizi hotel zinamilikiwa na hawa wenye mabasi au wenye mabasi wanapata nini hapa maana unakuta mabasi yanaendelea kusimama katika hotel hizihizi licha ya hotel kuwa na;

Huduma mbovu na ghali - Vyakula ni ghali hlf vina viwango duni. Unaagiza chakula ni basi tu kupooza njaa lakini kimsingi unakula makapi! Chipsi na zile nyama choma haviivi inavyotakiwa.

Mazingira mazima hasa chooni machafu na yasiyoridhisha.

Hapa shida ni nini wakuu? Maana siamini kama hakuna wawekezaji wanaoweza kuweka mzigo huko na kutoa huduma ya kueleweka.
wenye mabasi hawahusiki hapo ila kuna utaratibu ambao dreva akipeleka abiria kwenye hoteli yeye na crew yake wanapewa chakula na maji bure pamoja na posho,na hizo hoteli zinaushindani mkubwa sana ukiona basi nyingi zinaenda hotel flani bas ujue hiyo hotel inatoa posho kubwa kwa madreva
 
Nimewahi kuumwa tumbo njiani mara mbili kwa safari mbili tofauti. Ya kwanza kutoka Mwanza naelekea Dar. Hiyo siku nilitamani basi iniache njiani ili nipate kushusha vitu vilivyokuwa tumboni, maana tumbo lilichafuka ghafla. Safari ya pili ni kutoka Mwanza naelekea Dodoma. Safari hii ni mwaka jana tu mwezi wa 11, niliumwa tumbo ikabidi niwaombe waniache njiani. Walinishusha sehemu moja sikumbuki inaitwaje lakini ni kabla ya Manyoni stand.

Baada ya kushushwa kwenye bus nikaomba wenyeji wanipe direction wapi ilipo Toi hata ya kulipia. Nikaelekezwa sehemu kuna choo cha mji flani, daah! Nilishusha vitu heavy weight
 
Inategemea unapanda bus Aina gani huwezi kulipa nauli 45000 kufika Arusha then ukapelekwa hotel uchwara

Toa mfano wa hiyo sehemu ya maana juu ya huduma. Walau njia ya arusha labda ule nyama choma. Usithubutu kula sijui wali ama ugali. Njoo kwenye bei sasa hapo ndo tatizo.

Mfano cate hotel pale moro, bei zao utadhani watu wameenda kutalii.

Moja ya sehemu ambayo binafsi naona wanajitahid kuwa fare ni ile hotel iliyopo nje kidogo ya babati. Pale nyama choma ni unyama sana. Chai yao pia ni mswanu.

Ila usile wali wala pilau [emoji1].
 
Kama mnaona vyakula bei juu pika nyumbani acheni kusumbua watu.

Basi wasisimame kwenye hizo hotel. Kama vipi wawe neutral na zile hotel zetu za stand. Wao wasimame kwenye hizo hotel zao na sisi tufikishwe kwenye hotel zetu za kiaria[emoji1]. Eti chai 2,000 andazi 2,000 huu si wizi kabisa. Wali nyama ng’ombe afu8????? Kweli?
 
Wale wezi wezi tu mm km natoka mwanza nachukua sato wangu anakaangwa na ndizi mzuzu natia kwenye kikontena biashara imeisha hapo ni pepsi take away na kula samaki safiiii nagika dar nimeshiba kuliko kwenda kununua ma vitu bei juu ubora ziroo unakula roho inauma.
Kula samaki ndani ya bus nao si ustaarabu inapelekea mende kwenye seat na carpet
 
Yani hadi soda nazo ni makapi?

Hadi kwenda kukojoa nako huduma ni duni?

We kijana TAFUTA HELA wenzako wametumia mamilioni kuwekeza kwenye hospitality industry halafu wewe unatumia bando la jero kutukana juhudi za wenzio..
Swala sio investments za wenye hizo hotel , swala lipo kwenye u ghali wa huduma zinazotolewa ukilinganisha na hadhi , soda inaweza isiwe makapi kama ulivosema lakini unauziwaje soda sh2000. Olhali mtaani ni 1000 na hapo panapouzwa wala sio 5 star hotel
 
yote kwa yote kama mnataka kukwepa gharama mjifunze kujiandalia vyakula vyenu mkiwa na safari ndefu.
 
yote kwa yote kama mnataka kukwepa gharama mjifunze kujiandalia vyakula vyenu mkiwa na safari ndefu.
Swala sio gharama , tatizo ni ubora wa hicho unachogharamia ! Kfc anauza chicken wings 4 na chips kwa 12000 ulishawahi kusikia malalamiko ?
 
Back
Top Bottom