Kuna siri gani kati ya mabasi ya mikoani na hizi hoteli wanazosimama kulisha abiria?

Umeandika vitu ambavyo havipo...

Nimetoka Dar es salaam kwenda mbeya Kama mfanyabiashara/ mfanyakazi nimelala lodge Kwa siku mbili siku ya kurudi kutoka mbeya atanipikia nani ili nibebe chakula!

Na sio Kila mtu anaweza kubeba mahotpot safarini
Pole. Unatakiwa kuridhika na hali halisi unayokutana nayo. Maana siyo rahisi kupata kila kitu unachokipenda kwa ubora unaoutaka wewe.
 
Mimi nimeshaacha kununua vyakula na vinywaji,huwa nafungasha toka home au stendi kabla sijaondoka,mana wale wauzaji wa hizo hotel huwa wanatafuta super profit.
 
Pole. Unatakiwa kuridhika na hali halisi unayokutana nayo. Maana siyo rahisi kupata kila kitu unachokipenda kwa ubora unaoutaka wewe.
Hii ndio sababu nikiwa natokea nyanda za juu kusini napenda kupanda basi za abc- nashukia kwenye hotel yao pale morogoro kula.

Mazingira yapo safi japo Bado gharama haziendani na vyakula
 
Mimi nimeshaacha kununua vyakula na vinywaji,huwa nafungasha toka home au stendi kabla sijaondoka,mana wale wauzaji wa hizo hotel huwa wanatafuta super profit.
Ni kweli, vyakula vya huko vinauzwa thrice the price. Nilishaachaga huo ujinga. Maana gharama ya njiani unatumia mara tatu ya kawaida na still hata quality hupati unaishia kuumwa tumbo. WTF? Unanunua ugonjwa bei ghali?
 
Hao waarabu wanauza vyakula vimechacha walikua na ingine mombo imekufa ...wamefungua ingine mombo nayo haina wateja,uhakika wa chakula kizuri njia ya arusha ni korogwe tu unakula kitu fresh
 
Haswaaa
 
Kuna hapo nangulukuru aiseee chipsi vijiko viwili tu ni 2000 tsh. Kuna siku kidogo nisuse ila nikaona sio kweli basi nikachukua kinyonge tu.
Haha ukakumbuka kwamba hata ukisusa huwakomoi ukaona ubebe tu, maana wale hawabembelezagi mtu wanakutajia bei zao huku wanaendelea na shughuli nyingine, unataka nunua hutaki acha
 
1. Dereva na kondakta hula chakula bure
2. Dereva hupewa posho
3. Woteli huingia mikataba na wenye mabus
4. Hotel za wenye mabus mfano Dar express, kilimanjaro hawa wana hotel zao wenyewe.

Njia ya kaskazini huongoza kwa hotel nzuri, barabara zingine hotel za hovyo mno
 
Hii ndio sababu nikiwa natokea nyanda za juu kusini napenda kupanda basi za abc- nashukia kwenye hotel yao pale morogoro kula.

Mazingira yapo safi japo Bado gharama haziendani na vyakula
Yeah kwa Morogoro sehemu nzuri za kula na kuchimba dawa ni hapo Cate hotels na pale Msolwa kituo cha mafuta, ila Msamvu ni upuuzi mtupu na huko ndiko mishikaki ya paka na mbwa, na vikorokoro vingine vya ajabu ajabu hupatikana sana
 
Kwani route nyingi hawajifunzi kuwa na hotel bora kama kaskazini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…