Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Kweli mfano mm naishi Hapa mwaya street ckuiz had mama ntilie kibao kama sio masaki yan
 
Dah! Mnaongelea mambo mazito mno. Kama isingekua kufika chuo ingenichukua muda sana kufika Dar. Naishukuru elimu kunifikisha Dar bila kuwasahau HESLB. Mwisho wangu ilikuwa Chalinze wakati naenda shule Iringa. Nilikuwa nikiona kile kibao kinaelekeza Dar napatwa na mzuka balaa. Siku nimekuja Dar kwa mara ya kwanza nikamtafuta rafiki yangu na kumsihi anipeleke nione Coco Beach. Bahati mbaya kwenye siku zangu za mwanzo kabisa Dar nilipata mkasa ulionipa aibu kubwa sana... pale Mabibo hostel ukivuka barabara kwa mbele kidogo kama unaenda Buguruni kulikuwa na Bar ambayo pia ilikuwa na gesti... enzi hizo Akudo impact ndo inavuma hatari. Sasa mimi nikawa namtaka mhudumu flani ila akawa ananila hela kunipa hanipi katika kumlazimisha lazimisha kukawa kuna kubishana nae.. mara akatokea jamaa sijui ndo meneja akanichimba mkwara na kuniambia nipotee eneo lile nisionekane kwasababu naleta kero huku hata bia sinywi.
 
Hapo kwenye kilimanyege kwenye huduma
 
Hapo kwenye kilimanyege kwenye huduma
Kilima jina kwa sababu cha ghafla halafu kifupi ukipita ndani ya gari kuna ka msimumuko fulani. Sijui siku hizi kama wanatoa huduma hapo.

Hayo maeneo palikuwa na uwazi siku hizi kumejaa ma bar ukipita usiku kama unaijua masaki ya zamani na ujaenda muda mrefu panakuchanganya. Ilipo elements opposite alikuwa anakaa shushushu mmoja kanali Mnyani kulikuwa na space kubwa tu hadi ufikie gate lake.

Kulikuwa kimya sana maeneo hayo hasa kwenye hiyo cross-junction hapo ya kilima nyege halafu land niliyokuwa naijua ni nyumba ya captain Mutafungwa zile chongoma hazipo tena. Ukishuka chini kwenye walikokuwa wanakaa hakina Wasia Mushi unatembea barabarani magari kupita nadra, ukipanda juu wanapokaa kina James Lugembe ile mitaa ukipita kama humjui mtu ata bila ya kuitiwa mwizi unaweza jistukia.
 
Kabisa kiongozi!leo kimebaki tu kile kilima 😂 na pale ndo mpaka kati ya Masaki na Obey!Wakijenga upya ile barabara nafikiri kitakufa!
 
Kabisa kiongozi!leo kimebaki tu kile kilima 😂 na pale ndo mpaka kati ya Masaki na Obey!Wakijenga upya ile barabara nafikiri kitakufa!
Imearibika sana hakuna open space kabisa na land marks za zamani hazipo tena. Mie nilipotea ilikuwa usiku ata niliposhuka hapo kilima nyege sikujua wala IST sikuitambua maana mbele pale kulikuwa na kimila fulani unapanda kwenda kwa Dr Mbawala nafika sikioni nakutana na high rises nikajiuliza hapa nipo masaki kweli; hiyo ilikuwa baada ya kama 18 years natokea kijijini.

Wamepaaribu sana kumebaki jina tu.
 
VItuo vya boda boda, bodaboda wamekuwa wengi,wakati Kila nyumba Ina ndinga zaidi ya Moja
 
Hiyo sehemu imejengwa miaka ya 90's na wafanyakazi wa SHIRECU,2000's ilikuwa tayari ilishadoda.Nilipelekwa kuangalia nyumba ya kupanga unakuta jumba kuubwa hadi linatisha.Nadhani kwa sasa patakuwa hoi zaidi.
 
Upo sahihi,mwezi uliopita kuna nyumba mitaa ya Mkadini Oysterbay karibu na Qatar Charity tulienda kugonga geti akatoka beki tatu na kutuambia bosi hakai hapo siku hizi muda sana...
Dah kumbe ndo nyinyi mligonga geti nikawafungulia? Madalali matapeli.
 
Kuna mama mmoja msomi kwenye hiyo sector ya urban planning nilikutana nae short course Dodoma kwenye maswala monitoring and evaluation nilimuuliza nini chanzo cha huu utopolo wa ujenzi holela alinijibu in short ni "kuacha kila mtu ajenge"vitu hivi vinapaswa kuachia makampuni makubwa ya Real Estates then sisi tunakuwa wanunuzi tu kutokana na nguvu ya mfuko wako.
 
Wakati huo lami haileselasie inashia shule ya IST mbele kote vumbi tu

Ova
Sijui IST ya leo ila IST ya kipindi kile pembeni kulikuwa na kontena watoto wa kishua wakitoka shule wakati wengine wakisubiria kuchukuliwa wanakula pombe na mafegi kwa kwenda mbele dah wakati huo mi nasoma Obey primary school!! Watoto wa kike wazuri kinoma!Mara moja moja watoto wa mtaa tulikuwa tukiruhusiwa magetini na walinzi tuingie kwenye ile basketball court yao kupiga kikapu.
 
Longtime,kuna mtoto mmoja wa kizungu alikuwaga obay alikuwa anaitwa John bichwa kama mtu alikaa obay na masaki hyu atakuwa anamfahamu...
Wazee wake walikuwa maeneo mengi wanayamiliki huko

Ova
Kbs John alikuwa ni mtu sana pamoja na Banzi wa pale Mbuyuni Primary School!.
 
Upo sahihi,mwezi uliopita kuna nyumba mitaa ya Mkadini Oysterbay karibu na Qatar Charity tulienda kugonga geti akatoka beki tatu na kutuambia bosi hakai hapo siku hizi muda sana...
Mkadini kipindi hiko ulikuwa ni mtaa wa majaji na wanasheria manguli mfano mzuri ni mzee wetu Lubuva,Mihayo pamoja na Jaji Bahati na wengine wengi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…