Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

💯
 
Wale wazungu expertise magari yao zilikuwa TX,watoto wa kinondoni wale janja janja wote unawakuta sokoni tx kinondoni,tunasubiri kuwapokea wazungu kuwabebea mizigo nk
Wanatu tip [emoji1] haya maisha bana

Ova
Kumbe pale TX kitambo eeh?
 
Aisee
Umenikumbusha mbali sana, kweli tumezeeka
Haile Sellasie road ndio nyumbani kabisa ilikuwa miaka hiyo kabla hujafika Mhalibwa grocery, hebu fikiria ndio lilikuwa duka pekee, ukiacha Supermarket ya Morogoro stores.
Enzi za kina Rob D, na Nigga one (RIP) ndani ya mtaa
Wakati huo basi ni moja tu la UDA, mitaa kimyaaaa
Kibibii ya Tryphone Maji peke yake ndio alikuja kupewa leseni ya daladala
Mitaa mingine unajikuta ni wewe peke yako barabara nzima
Nilikuja kwenda na familia miaka kadhaa niwaonyeshe madogo wangu nilipokulia, duuh..hadi aibu kama uswahilini tu mabaa na bodaboda, wamasai wametapakaa mtaa mzima, tulipokuwa tunaishi sasa mbele kuna Pub, nilishindwa hata niwaonyeshe nini watoto wenyewe hawajazaliwa bongo ni ilikuwa kituko tu

Masaki kumechafukwa na kuvurugwa haswa, sio tena residential area ya kishua
 
Ulipotaja hapa tu kaka umemaliza "Mhalibwa grocery" kulikuwa na mshkaji mmoja mnene mnene hivi ndo palikuwa kwao krb na zile flat za TIB baadae kidogo kuna duka jingine lilifunguliwa kule krb na kwa mzee Nimrod Mkono krb na Oysterbay Hospital.So sad!!!!
 
Ilikuwa ndo njia yetu tukielekea kule Masaki mwisho na baiskeli zetu za BMX across Europa Mini-Supermarket mwisho kbs kule kwenye kambi ya jeshi kucheza basketball kwny ile court ya jeshi.Pande zote ni ushua mtupu!.
 
Tujuane wale tuliokuwa na membership card kwa ajili ya kuazima movie pale Morogoro Stores na kule Europa😂 usiombe kukutana na tapes za NTS zinachagua deck vibaya mno, dah tenkolojia hii eti kuna kipindi tulikuwa tunasubiri tape iwe rewinded inategemea na urefu wa movie yenyewe, mara deki imekula mkanda 😂😂😂.
 
Saiv kuna dada poa wanajiuza kuanzia saa moja wanasima upande wa garden
 

Hakuna kitu kinaudhi mtu kujenga frame za biashara katika nyumba ya kuishi. Basi iwe hata moja ya mwenye nyumba, anaweka sita. Tena unamkuta mtu msomi kabisa.

Watu mpo mtaa umetulia ghafla vimigahawa, bar, studio ya kuingiza nyimbo kwenye simu, movie. Inaanza vurugu tu.
 
Sema Mbweni sasa hivi ni habari nyingine na mji unakuwa kuelekea Bagamoyo, natamani Dar na Pwani ingeunganishwa uwe mkoa mmoja tu uitwe Dar ili watu wasogeesogee huko, na waondokane na ile dhana ya kutaka kuonekana hawaishi Dar wanaishi nje ya miji
Hapana, isiunganishwe, ila Kibaha na Bagamoyo zipandishwe hadhi ziwe manispaa zinazojitegemea
 
Wakati maduka mawili, chang'ombe ndio ushuani ya ukanda wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…