Trend ya miji ya Kibongo ni kwamba pesa ikifumuka watu wanaanzisha ka-mji ka kishua wanafunga kuta na mageti makali. Watoto wanalelewa kishua kila kitu kipo.
Wazazi Wakizeeka na kuaga dunia watoto wanaishi kwenye majumba mazuri lakini ukute hawana kipato.
Mwisho wa siku wanauza majumba au wanaishi humo wakiendesha biashara haramu nao wanaaga dunia nyumba zinakaliwa na wajomba na mashamgazi ndo hao mnaowaona Masaki.
Ama kweli maisha yana badilika sana ,ulichosema ni kweli kabisa .kipindi cha nyuma miaka ya 2000 huko,kuna ki mji kilikuwepo shinyanga na walio kianzisha wengi ni watumishi wa shirika moja hivi.
Wale wazee walifirisi shirika hilo ,na wote walikuwa wamejenga sehemu moja ,nyumba zote zilikuwa na kuta na mageti ,nyasi zilimea kwa kumwagiliwa maji ya kutosha(garden)
Miaka imeenda wazee wakaanza kuugua na kufa mmoja mmoja,inasemekana ukimwi uliwapiga KO ya hatari ,kipindi kile hakua cha ARV wala nn,walikuwa wana share totozi ,si unajua mambo ya pesa.
Nyumba zilibaki na watoto tu ,nyasi zilikauka kila mji.hali ili badirika sana ,baba na mama hawapo ,unazani famia itakuwaje?
Si mji ule tena ambao ilikuwa ukipita unasikia sauti nene za music taratibu na harafu ya vinono vikikaangwa.
Nyumba ziliuzwa na wajomba na mashangazi baada ya wazazi kuondoka gafla na kukosekana mwelekeo wa malezi.
walio baki ni wachache sana ambao hata leo hii uzao wao upo pale