Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Hakuna Baba anaweza kufanya huo ujinga, kina mama ndio wanaoharibu hawa Watoto wa sasa hivi, Toto linadekezwa mpaka umri limebarehe unalidekeza tu linakuwa jinga kabisa.
Yupo baba mmoja alimpeleka binti yake chuo kikuu kile kipindi cha kusajiliwa. Yaani ilikuwa ni kituko mzee anazunguka na binti yake kila mahali mpaka wale Auxiliary Police wakamuambia mzee hapa ni chuo kikuu muache binti yako afanye hizi taratibu mwenyewe kama wenzake. Mzee alijishtukia sana aisee! Ilikuwa ni mwaka 2015.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
HAKUNA UMUHIMUUU LABDA KAMA TOTO ZEMBE ZEMBEEE LIPELEKEE...!! mimi kuacha kupigisha pindi nipate helaa na kwenda Jkt iliniumaa sanaa yanii mnooo namind mpaka leooo[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
Mkuu viposho vya miezi nitatu tu ndio vikuume mpaka leo !!..ndio maana hasira zote ukaishia kuchakata kimasihara.
 
Mkuu viposho vya miezi nitatu tu ndio vikuume mpaka leo !!..ndio maana hasira zote ukaishia kuchakata kimasihara.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Yani inaniuma bado kuacha Hela za maana nikaenda kuteswa na kulipwa elfu 50 yenye makato nikawa naambulia elfu 35.. Huu ujinga mwanangu hafanyi[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
 
me
Kama kijana aliyemaliza A level anaweza kukwepa kadhia ya kuripoti JKT bila kukumbana na serious consequences kuhusu future yake sidhani kuna mtu angeripoti kambini. Ndiyo hoja yangu ya msingi.

me nilipangiwa na sikwenda, hamna serious consequences zozote
 
Watu mnaropoka upuuzi humu.....
Millitary service inatakiwa iwe lazima kwa watu wote tena mwaka 1.
Amani hii inawazuzua mnahisi mnastahili sana sio?
If tunafanya mobilization, tutamobilize nini? Mtu asiye na A wala B ya millitary service?

Nchi ambazo wanaelewa haya mambo washapata tabu kadhaaa huwezi kuwaona wakiongea Shombo kuhusu millitary service.
 
Nafasi nyeti Zipo huko BOT na Sio hizi upolisi na jeshi
Sio kweli. Kwenye sekta binafsi wapo wanaotoa ajira kwa vijana lakini mojawapo ya sharti ni aliyepitia JKT e.g. kampuni za migodi lakini pia kwenye Tasnia ya Usanii huwa wanahitaji aliyepitia JKT kuigiza katika nafasi ya askari au mlinzi.
Kwenye jeshi (majeshi yote) kijana F6 science subjects na aliyepitia JKT huwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata scholarships. Siku hizi jeshi ni la kisomi zaidi (lipo ki-digital) na sio kwata na kubeba mtutu tu.
Huko BOT kuna unyeti gani ilhali walioajiriwa huko tuko nao huku?
 
Unajua salary scale ya Mtumishi wa B.OT?
 
Habari zenu Wana JF,

Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.

Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?

Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?

Asanteni kwa msaada.
Bila shaka ushapata majibu, mdhara makubwa ni mateso tu,

pia kuna baadhi ya watu hupata changamoto za kiafya kutokana na ukali wa mazoezi

wanawake hukazwa sana na wasimamizi wao

ila haina madhara katika kuendelea na elimu ya juu au ajira isipokuwa ajira za sekta ya ulinzi

NB: Wanafunzi wanaomaliza ni wengi mno na kambi zipo chache mno.

hata nusu ya wanafunzi huwa haifiki (wanaochaguliwa)

Hivyo hawawezi kuweka kigezo cha kwenda JKT ni lazima katika kwenda vyuoni au ajira kwa sababu wenyewe hawawezi kuwapeleka wote
 
Nafasi nyeti Zipo huko BOT na Sio hizi upolisi na jeshi
Jua kwamba nafasi yoyote nyeti Tanzania hii inahitaji vetting. Sio BoT, Sio TRA, Sio EWURA.

Yani ukiona serikalini mtu yoyote anaitwa Manager, Mkurugenzi, etc....jua ni mtu wa system. Sasa ndio huwezi tena ingizwa system kizazi hiki kama hujapita JKT.
 
Uongo huu , kuwa mkurungezi unahitaji kuwa umepita Jkt au Elimu yako na network mfano mkurugenzi wa TPC kapita jkt au upo unaota Mkuu
 
me

me nilipangiwa na sikwenda, hamna serious consequences zozote
Nanukuu: "........hamna serious consequences zozote" Vp Ulikwepa kwenda JKT kwa sababu ya uoga au ?
Hapo unaposema hamna serious consequences... manake indirectly unakubali kuna consequences lakini ww unazi-degrade kuwa sio serious. Hapo ujue inaweza ikawa sio serious kwako lakini kwa mwenzio ikawa ni Lethal.
Kila mtu ana mapito yake na usisafirie nyota ya mwenzio. Nikupe mfano: Wewe unaweza kwa bahati mbaya ukapoteza Tzs elfu tano na isikusikitishe sana, lakini yupo ambaye akipoteza Tzs elfu tano tu kwake inakuwa ni kama msiba vile. Kuna kutofautiana mkuu.
 
Uongo huu , kuwa mkurungezi unahitaji kuwa umepita Jkt au Elimu yako na network mfano mkurugenzi wa TPC kapita jkt au upo unaota Mkuu
Kwanza kabisa huwezi kufanywa mkurugenzi Postal Bank bila kuwa kitengo. Basi kama sio kitengo lazima ufanywe hivyo.

Pili utaratibu ulibadilika Magu alivyoingia madarakani, utaratibu huo ndio unafanya kazi sasa, hawa vijana wa sasa hawawezi kwenda kitengo bila kupita JKT.

Effect yake sio ya leo, ni miaka 20 ijayo. Maana mtu anayetoka JKT leo hadi aende chuo miaka 3, aanze kazi, appande vyeo hadi kufikia ukurugenzi si chini ya miaka 20.
 
Unajua salary scale ya Mtumishi wa B.OT?
Mkuu, kwa kweli sijui. Lakini unyeti wa nafasi ya Mtumishi au mtu yeyote haitegemei salary scale yake au anamiliki fedha kiasi gani bali anayo nafasi gani kihuduma katika Jamii. Usishangae ukijagundua kwamba kumbe hata wanasiasa Mbunge na Diwani wa Kata wanapata fedha nyingi.
 
Habari zenu Wana JF,

Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.

Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?

Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?

Asanteni kwa msaada.
Kutokana na kundi kubwa la wanafunzi wengi ambao hawajui maisha ya kawaida ya uraiani kufaulu vizuri na kujiunga Elimu ya juu
Naunga mkono 100% wote waliomaliza Elimu ya kidato cha Sita wenye Afya njema wapite jeshini ili wakajue hali halisi ya maisha yanayoendelea huko nje. Kuna wengi hawajui kuwa kuna wanafunzi wanakaa chini darasani, wanakosa mlo wa mchana, hawawezi kulipia matibabu hata 20,000. Hayo mafunzo yanawapa mwanga ya kinacho endelea huko nje....
Kama una Afya nzuri kuna sababu gani inakufanya usiende jeshini sijui kwa miezi 6 tu?
Unaweza kukosa mengi huko mbeleni.....
 
Kijana, nenda JKT.
Siku zitakuja mbeleni, very soon, kuna fursa zitatokea na kwa makusudi kabisa, watasema aliyepita JKT ana "added advantage"
Hakuna madhara ya kupitia JKT, bali kuna faida.
Achana na haya matutusa yajazane ujinga tu! Yaani jitu linakurupuka kabisa kusema eti hakuna madhara? Juzi serikali imetangaza nafasi za Uhamiaji, Polisi, JW, TAKUKURU, TANAPA, Magereza, Zimamoto zote hizo Kigezo kikubwa kilikuwa awe amepita JKT! Ipo siku vijana watalia kilio cha mbwa koko! Niko hapa napambana na wife eti anamkingia kifua dogo asiende JKT! Nami nimetoa msimamo JKT lazima aende! Ukweli kuna mambo mengi atanufaika nayo mbali na hizo nafasi zenye Kigezo cha JKT! Hata ule ukakamavu tu ni faida tosha kabisa kwa kijana mdogo!
 
Kutokana na kundi kubwa la wanafunzi wengi ambao hawajui maisha ya kawaida ya uraiani kufaulu vizuri na kujiunga Elimu ya juu;
Naunga mkono 100% wote waliomaliza Elimu ya kidato cha Sita wenye Afya njema wapite jeshini ili wakajue hali halisi ya maisha yanayoendelea huko nje.
Kama una Afya nzuri kuna sababu gani inakufanya usiende jeshini sijui kwa miezi 6 tu?
Unaweza kukosa mengi huko mbeleni.....
Wala siyo miezi 6 mkuu, ni miezi mitatu tu!
 
Bila shaka ushapata majibu, mdhara makubwa ni mateso tu,

pia kuna baadhi ya watu hupata changamoto za kiafya kutokana na ukali wa mazoezi

wanawake hukazwa sana na wasimamizi wao

ila haina madhara katika kuendelea na elimu ya juu au ajira isipokuwa ajira za sekta ya ulinzi

NB: Wanafunzi wanaomaliza ni wengi mno na kambi zipo chache mno.

hata nusu ya wanafunzi huwa haifiki (wanaochaguliwa)

Hivyo hawawezi kuweka kigezo cha kwenda JKT ni lazima katika kwenda vyuoni au ajira kwa sababu wenyewe hawawezi kuwapeleka wote
Nanukuu:
"...pia kuna baadhi ya watu hupata changamoto za kiafya kutokana na ukali wa mazoezi
wanawake hukazwa sana na wasimamizi wao"

1. Wanaopata changamoto za kiafya hupata matibabu kama kama inavyokuwa Uraiani. Mtu huenda Hospitali akapata vipimo na matibabu huendele hata kama ni referal.
2. Wanawake kukazwa ni wanapenda wenyewe eti ili apate ka-unafuu /upendeleo asipewe kazi ngumu( anakuwa Selule),asiadhibiwe au apate chakula kizuri na kingi au awezeshwe kifedha. Lakini mbona hilo hata huku mitaani si lipo tu?Ukijilegeza-legeza mengi utayapata.Tuseme mwanamke kukazwa ni Hiari yake. Iko siku ya kikao cha kutoa ushauri, Maoni, dukuduku au mapendekezo. Mbona hawasemi hilo? au wanakufa na tai shingoni?
 
Back
Top Bottom