Kuna Upigaji mkubwa sana kwenye Miradi ya Ujenzi hasa Barabara

Hata design pia inaweza isiwe shida, design inaweza kuwa nzuri Ila mjenzi akajenga vibaya
 
Unajuaje barabara flani imejengwa chini ya kiwango?
Ukipita barabara haina njia za watembea kwa miguu na waendesha baiskeli hiyo barabara imejengwa kwa viwango vya juu vya ubora?

Ukipita barabara unaona hakuna hata mifereji ya maji , taa za barabani kuwezesha watu kutembea vizuri usiku au haina hata upana unaotakiwa kwa magari kupishana vizuri kuepusha ajali unadhani hiyo barabara itakuwa imejengwa kwa viwango au ubora sahihi??

Hapo hatujasema barabara hizi ambazo Inajengwa mwezi huu ikinyesha mvua tu imeshaanza kumeguka
 
Hii ni mitaa ya jiji la ethiopia cheki barabara ...hapa utagundua kuwa huyu mpumbavu chura kiziwi anatupotezea muda nchini kakuna cha ubunifu wala cha maana anacho fanya.


View: https://youtu.be/bvBs_fQm-qA?si=gij5uD9cA4hKYvQH
 
Mkuu hizo barabara unasema zinajengwa hovyo ni zipi? Ungetoa mifano
Pia unajuaje barabara flani imejengwa chini ya kiwango?

Na unalinganisha ubora wa barabara wa wapi na wapi? Au unalinganisha Europe na Tanzania? Au unalinganisha Kenya na Tanzania au Uganda na Tanzania? Be specific kwenye hii mada
 
Barabara nyingi sana. Karibu asilimia 70 ya barabara zetu.

Juzi nilikuwa Dodoma. Nikasema nifanye mazoezi njia ya Waziri Mkuu hadi Martin Luther nimeishia kugongwa na pikipiki tu maana barabara yote haina njia za watembea kwa miguu na baiskeli.

Nenda njia ya Milocheni hadi Kawe Dar kama utaona sehemu ya watembea kwa miguu, nenda njia ya makumbusho hadi Tandale, hakuna kabisa
 
Mkuu ubora wa barabara sio lazima uwe na njia za wapita kwa miguu. Mfano Trunk roads unataka ziwekwe njia za wapita miguu?

Kuna uzuri na ubora, kitu linaweza kuwa kizuri lakini sio bora. Mfano raba inaweza kuwa nzuri inavutia lakini sio bora, ukivaa ndani ya wiki tu imechanika. Na Kuna nyingine unakuta ni bora lakini sio nzuri na haivutii
 
Ubora wa barabara sio lazima njia za wapita miguu, zipo barabara zenye hizo njia lakini zimeharibika ndani ya muda mfupi. Na zipo barabara hazina hizo njia zimedumu kwa miaka mingi.
 
Wanaishi kwa kujiangalia wao na familia zao. Neno maslahi mapana ya nchi na wananchi lipo midomoni mwao tu wala sio kwenye uhalisia na utendaji wao
Eeh naingia kweny siasa ,siwezi acha wajinga wanitawale,nchi haiwezi endeshwa kienyeji halafu watu weny maono tunakaa kimya.
 
Hiv barabara Ina mwaka mmoja tu ,then unakuta mashimo ?,what comes on your mind?
Swali zuri, sasa hiki ndio alipaswa kukisema huku akieleza ni percentage ngapi ya barabara zinazojengwa/zilizojengwa zimekaa muda mfupi na kuharibika. Hapo ndio utakuja na hoja kuwa barabara hazina ubora.
 
Tanzania ikiwekwa "Deathrow" au sheria ya kufumuliwa ubongo na risasi kisha ikasimamiwa vizuri ndani ya miaka 20 ijayo bongo patakuwa kama Japan 🤣.

Uadilifu sio swala la negotiation, ni swala la compliance tu! Mtu ambaye anaona hauwezi uadilifu akae pembeni au akubali kufa.
 
Kweli kabisa
 
Swali zuri, sasa hiki ndio alipaswa kukisema huku akieleza ni percentage ngapi ya barabara zinazojengwa/zilizojengwa zimekaa muda mfupi na kuharibika. Hapo ndio utakuja na hoja kuwa barabara hazina ubora.
So vitu Kam hivyo ndio vinaleta picha uenda Kuna wizi ufanyika,na mm huwa siamini kwamba hizo pesa za miradi huenda hupelea na zisitosheleze..,hyo n big No,kitu iliyopo uadilifu n tatizo kwa viongoz weng wa umma
 
Mkuu nimetoka sababu. Anayejenga ni serikali mkadarasi ni mtekelezaji tu. Na siyo vyote ni upigaji
 
Kila mmoja anakula kwa urefu wa kamba yake. Pia fuatilia ukwasi wa wasimamizi wa ujenzi wa barabara na majengo utashangaa, wana mali isiyoelezeka kumbe ni wizi wa rasilimali za umma.
 
Kuna kitu huelewi.
 
Huo ni ukweli mtupu
Aaah wapi stori za vijiweni
Nimejenga Nzega....Tinde....Isaka halafu Tinde... Maganzo.......gongo tulikunywa nyuma ya Kishosha Guest House na kina Shambenga.....
SUMBAWANGA Laela to Luiche Bridge Camp ilikuwa Kihanda....karibu na Mpui.....
RUVUMA kuanzia Songea mpaka Namtumbo Camp ilikuwa Utwango karibu na Namabengo... Tanzania 🇹🇿
Sasa wewe hii Tanzania yangu umeshiriki kujenga kipi zaidi ya fitna chuki na majungu?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…