Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Sawa umeeleweka kaka,vp Mbowe ni #GAIDI ?.

najua wewe ni msomi tena mwenyewe taaluma nzuri.

Jaribu siku moja utuletee bandiko juu ya hilo kaka.
Najua we ni kada, hivyo uweke ukada pembeni, utumie taaluma yako kudadavua swala la Mh Mbowe.
Santé.
 
Wanabodi,

Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa!, ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!.

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere!. Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?.

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!.
Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea...

Ni kama Mwalimu kabisa!.
Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.
Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga!, akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga".

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?.
Paskali
Update

Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.
Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere!. Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!.

Huku ni kumdhalilisha Baba Wa Taifa hili kwa kiwango kichopitiliza, muwe na heshima japo kwa Waasisi wa Taifa hili enyi vijana, acheni njaa za kijinga, hata ungepewa vyakula vyote vya dunia hii huwez kuvila ukavimaliza na kile kidogo utakachokula hapo utaenda choon unakitoa na bado utataka tena na tena. Msiendekeze matumbo yenu.
 
Duuuh!!!!!!...... Nyerere na Polepole wamefanana!!!!, kweli?
Naona kweli uzee unakujia vibaya.
Huyu aliekua tume ya Jaji Warioba anahubiri katiba mpya, alipopewa madaraka akabadilika akawa hataki katiba mpya, akaungana na Prof alieokotwa jalalani kukana waliyokuwa wakihubiri na Mzee Warioba.
Huyu ambae watu waliotoa maoni wakati wa utawala wa mwendazake aliwanyamazisha leo yeye hataki kunyamazishwa.
Huyu ambae alikua anatuuliza kama tunaijua vi eit.
Huyu ambae Membe alipotoa maoni yanayopingana serikali iliyopo madarakani alitoa karipio na vitisho lukuki.
Na mengine mengi siwezi orodhesha hapa.

Leo ndio umfananishe na Mwalimu!!! this is a shit joke!

Namuona ana hoja inayohitaji majibu lakini sio kumfananisha na Mwalimu
 
Ni kweli kabisa. Polepole ni kichwa kuliko vilaza wote pale safu ya CCM ukianzia Samia,katibu mpaka katibu mwenezi wa sasa.
 
Huyu Polepole ambaye leo anaona TCRA inaingilia uhuru wake ndiye huyo huyo Polepole ambaye aliwaambia TCRA wafanye kazi yao kwa anayemsumbua mnyoosha nchi. Ilifikia hatua Polepole aliona ni dhambi kubwa sana kumkosoa Magufuli. Au Paskali umesahau? Huyo Nyerere unayemfananisha naye ni wa mchongo!
nadhani anamaanishq steve nyerere
 
Julius Kambarage Nyerere=Polepole?

Polepole akifa naye ataitwa hayati siyo marehemu???
Hayati na marehemu wana hadhi tofauti ujue!

Everyday is Saturday................................😎
Ungejua neno hayati ni neno la kiarabu, na washahili walilitohoa kimakosa kumaanisha mtu aliyekufa, ila neno hayati ni neno la kiarabu al hayyat likitamkwa sawa na kiswahili hayati likiimaanisha 'maisha' ...
 
Je anayoyazungumza haya huyo Polepole kwanini hakuyazungumza awamu ile akiwa na position kubwa?

Je ni kweli mabaya mengi tu ya awamu ile hakuyaona?

Dosari za kwenye chaguzi zote mbili Serikali za mitaa (2019) na uchaguzi "uchafuzi" mkuu (2020) Polepole hakuziona kama hakuwa sehemu ya ulaghai ule?

Polepole hakuona mwenendo wa wanasiasa/wanaharakati wenye mawazo kinzani na boss wake wa wakati ule walipokuwa wakizimwa na hadi wengi kukimbilia ng'ambo??

Polepole hakua sehemu ya maamuzi juu ya katiba mpya ila ghafla akabadilika kama kinyonga na kuwaacha watanzania midomo wazi??

Polepole huyu huyu alishuhudia sheria kandamizi za kimtandao ila hakuongea bali alikua akishushia mvinyo na kupongeza "one man show" ya boss wake..?

It's not over until it's over...Karma is a bitch
AMEN
 
Hata wewe sio wa KUKUAMINI.
watoto waliozaliwa baada ya MAGUFULI kufariki ndo watamuelewa na kumuamini Pole pole.
 
Hizi ndo low mind.

Mambo ya mtu binafsi yanakuhusu nini? Hao warembo uliwaona. Au dada zako ndo walikuwa wateja ? Tujifunze kujadili hoja na si maisha binafsi ya Mtu.
Pamoja na yote ndugu yangu, TUWE WAKWELI. Mtu mwenye matendo machafu/maovu iwe ya binafsi au la, hafai.
Hana tena sifa wala kingine cha kumfanya awe wa kuheshimiwa/kutiliwa maanani. Huo ndio unafiki unaotukwamisha watz wengi.
 
Back
Top Bottom